PostGE2025 Leo Kidonda Kinatoneshwa. Maumivu ya MO29 yanaanza upya

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Quinine

Platinum Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
25,848
Reaction score
63,306
Leo Chande atatukumbusha wapendwa wetu waliouawa na polisi kwa kupigwa risasi za kichwa.

Leo tutakumbushwa yule mama wa Arusha aliyepigwa risasi ya mgongo akiwa na mimba ya miezi mitatu.

Leo tutakumbushwa wale vijana wa Mwanza waliokuwa wanaangalia mpira wakatolewa nje wote wakapigwa risasi.

Kwa mara nyingine tena leo itasikika vichwani mwetu ile sauti ya "hakuna cha nywinywi wala nywinywinywi".

Leo ni vilio kila sehemu, vilio vipya vya uchungu, ni siku ya maombolezo, siku ya kuililia mama Tanganyika.

Mungu atupe moyo mkuu.

Rest In Peace Mo29 Heroes.
 
Maoni yangu

Ripoti ya Tume ya Uchunguzi inayoongozwa na Jaji mstaafu Mohamed Chande Othman inatarajiwa kuwasilisha matokeo yake leo, Aprili 23, 2026. Swali la kama italeta suluhu au maumivu zaidi linategemea jinsi mapendekezo yake yatakavyotekelezwa na jinsi wadau watakavyopokea ukweli uliomo.

Hapa kuna mambo muhimu ya kuzingatia kuhusu mwelekeo wa ripoti hiyo:

1. Matarajio ya Suluhu
Kurejesha Imani ya Wananchi: Ripoti hii inatarajiwa kutoa mwelekeo wa kisheria na hatua za kuchukuliwa kufuatia matukio ya vurugu ya Oktoba 29, 2025. Kwa kuweka wazi chanzo cha vurugu hizo, inaweza kusaidia kuzuia matukio kama hayo yasijirudie na kurejesha imani kwa taasisi za umma.

Ushiriki Mpana wa Wadau:
Jaji Chande ameeleza kuwa tume imekusanya ushahidi kutoka kwa watu zaidi ya 63,603 kupitia njia mbalimbali, ikiwemo mahojiano ya ana kwa ana na watu 1,323. Ushirikishwaji huu mkubwa unaipa ripoti uzito wa kijamii na kisheria.

2. Uwezekano wa "Maumivu"
Athari za Kisaikolojia na Kisheria: Wataalamu wa saikolojia wametahadharisha kuwa ripoti hii inaweza kuwa na athari kubwa zaidi kuliko nyaraka za kawaida za kisheria, hasa kwa wahanga wa vurugu na familia zilizopoteza wapendwa wao.

Uwajibikaji:
Iwapo ripoti itabaini makosa ya kimfumo au ya watu binafsi, hatua za kisheria zitakazopendekezwa zinaweza kuleta mshtuko au "maumivu" kwa wale watakaowajibishwa, lakini hiyo ni sehemu ya mchakato wa haki.

3. Changamoto ya Uwazi
Kukataa Uvumi wa "Uchakachuzi":
Jaji Chande amekanusha uvumi kuwa muda wa tume uliongezwa ili "kuchakachua" ripoti, akisisitiza kuwa nyongeza hiyo ilikuwa kwa ajili ya kukamilisha uchambuzi wa ushahidi mwingi uliopokelewa.

Kwa kifupi, ripoti ya Jaji Chande ina nafasi kubwa ya kuwa suluhu ya kudumu iwapo itaweka wazi ukweli bila upendeleo na ikiwa mapendekezo yake yatatumika kuleta haki na maridhiano ya kitaifa.
 
Leo Chande atatukumbusha wapendwa wetu waliouawa na polisi kwa kupigwa risasi za kichwa.

Leo tutakumbushwa yule mama wa Arusha aliyepigwa risasi ya mgongo akiwa na mimba ya miezi mitatu.

Leo tutakumbushwa wale vijana wa Mwanza waliokuwa wanaangalia mpira wakatolewa nje wote wakapigwa risasi.

Kwa mara nyingine tena leo itasikika vichwani mwetu ile sauti ya "hakuna cha nywinywi wala nywinywinywi".

Leo ni vilio kila sehemu, vilio vipya vya uchungu, ni siku ya maombolezo, siku ya kuililia mama Tanganyika.

Mungu atupe moyo mkuu.

Rest In Peace Mo29 Heroes.

Amina.
Katika nyakati nyingi, hasa kipindi cha matukio makubwa kama ya utoaji wa ripoti ya tume, huwa tunajikuta tukiingia katika hali ya haraka—haraka ya kutoa maoni, haraka ya kuhukumu, na wakati mwingine haraka ya kusambaza taarifa bila kuzichambua kwa kina. Swali la kujiuliza ni: kwa nini tunakuwa na haraka kiasi hiki?

Kwanza kabisa, ni muhimu kuelewa kwamba kila mtu huona, husikia na hutafsiri mambo kwa mtazamo wake binafsi. Hivyo basi, kila ripoti au simulizi kuhusu tukio fulani huakisi kile ambacho mhusika ameona au kusikia, na jinsi alivyoelewa hali hiyo. Kwa sababu hii, haiwezekani kabisa ripoti yoyote kuwafurahisha watu wote. Wapo watakaokubaliana nayo, na wapo watakaoipinga—iwe ni ya kweli au imepikwa.

Hata hivyo, jambo la msingi ni kwamba kila mmoja wetu anayo kumbukumbu na uelewa wake wa kile kilichotokea, hususan katika matukio nyeti kama uchaguzi na fujo zilizo sababisha vifo na uharibufu wa mali. Hivyo, badala ya kuendelea kuzua taharuki zisizo na msingi, ni busara kuchagua utulivu na hekima katika kushughulikia tofauti zetu za maoni.

Taharuki zisizo na maana mara nyingi huwafanya watu washindwe kuzingatia mambo muhimu ya maisha yao—kazi, familia, maendeleo binafsi, na ustawi wa jamii kwa ujumla. Tunapopoteza mwelekeo kwa sababu ya mijadala isiyo na tija, tunakuwa tunajidhuru sisi wenyewe bila kujua.

Ni muhimu pia kutambua kuwa katika mazingira haya, kuna uwezekano wa watu wachache kutumia hali ya taharuki kwa maslahi yao binafsi. Tusikubali kutumika kama nyenzo ya kufanikisha ajenda ambazo hazina manufaa kwa wengi. Badala yake, tuwe makini, tufikiri kwa kina, na tusimame kwenye misingi ya ukweli na maadili.

Mwisho kabisa, tukumbuke kwamba maisha yanaendelea. Kila tukio lina mwanzo na mwisho wake. Changamoto na misukosuko yote tunayopitia leo, hatimaye itapita. Kilicho muhimu ni jinsi tunavyochagua kuishi na kushughulikia hali hizo.

Kwa hiyo, tusikimbilie mambo bila kuyatafakari. Tuchague utulivu badala ya taharuki, hekima badala ya jazba, na ukweli badala ya uzushi. Maisha ni yetu sote, na kila mmoja ana wajibu wa kuyafanya yawe bora zaidi.
 
Nafikiri wewe ni mgeni Tanzania au hujui, hii siyo tume ya kwanza kuna tume nyingi tu za kina Nyalali nk ulishawahi kusikia mapendekezo yake yamefanyiwa kazi? Kwani nini tujilishe matumaini hewa. Ni mjinga tu anayetegemea kuwa matokeo ya tume hii yatafanyiwa kazi yawe ya kweli au ya kumlinda muuaji.
 
SEHEMU YA MPITO: SAUTI JUU YA TAIFA NA FUMBO LA KUPONYWA

Kabla ya kufunguka kwa hatua inayofuata, kulikuwa na jambo zito lililonijia—si kwa kelele, bali kwa uzito wa ndani usioepukika.

Maono haya hayakuwa ya mtu mmoja, wala ya mahali pa siri pekee. Yalikuwa juu ya taifa.

Nikaona juu ya Tanzania, kana kwamba anga limebeba kumbukumbu ambayo haijasemwa wazi kwa vinywa vya wengi, lakini imeandikwa katika kilio kisicho na sauti.

Kulikuwa na rejea ya tukio—tarehe iliyopita, lakini isiyoisha ndani ya roho za walioguswa nayo.
29/10/25.

Siku ambayo ardhi ilibeba damu, na ukimya ukafunika ukweli wake.

Lakini katika maono, siku hiyo haikuonekana kama mwisho—bali kama mbegu.

Mbegu ya kilio.

Imeandikwa:

“Damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi.” (Mwanzo 4:10)

Na hapo ndipo nilipoanza kuona kwamba si kila tukio linaishia pale linapotokea. Mengine huanza kufanya kazi chini kwa chini, hadi wakati wa kujibu unapofika.

Katika picha iliyoonyeshwa, taifa lilionekana kama mjusi aliyekatika mkia—si kwa kushindwa, bali kwa kujilinda.

Sehemu inakatika ili mwili uendelee kuishi.

Lakini kilichokatika hakifi mara moja—kinatetemeka, kikitoa ishara kwa wanaotazama kwa makini.

Hivyo ndivyo ilivyoonekana.

Jaribio la kujitoa, kujisitiri, kujiponya kwa njia ya muda mfupi.

Lakini ndani yake kulikuwa na jambo jingine likianza.

Sio kwa kelele.

Sio kwa matangazo.

Bali kwa wale wanaoitwa ndani kwa ndani—wale wanaobeba mzigo wa taifa bila kutambulika.

Na hapo nikaonyeshwa muda:

Asubuhi.

Saa kumi na mbili kamili.

Mwanzo wa mwanga, lakini si mchana kamili.

Wakati ambao wachache huamka, na wengi bado wamelala.

Ndipo nilipoona kitu kikianza.

Sauti zisizo na vipaza sauti.

Maombi yasiyoandikwa.

Mioyo inayobeba mzigo bila kuonekana.

Na hapo ndipo neno lilikuja:

“Nimeyasikia.”

Kwa maana imeandikwa:

“Nimeona mateso ya watu wangu… nami nimesikia kilio chao… kwa maana nayajua maumivu yao.” (Kutoka 3:7)

Lakini pia:

“Kama watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekeza, na kuomba… ndipo nitasikia kutoka mbinguni, na kuisamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.” (2 Mambo ya Nyakati 7:14)

Hapa ndipo fumbo linakuwa gumu zaidi.

Kwa sababu si kila kilio huleta mabadiliko.

Lakini kuna kilio kinachofika.

Na kilichoonyeshwa si mwisho wa jambo, bali mwanzo wa mchakato.

Sio uponyaji wa ghafla.

Bali kazi ya polepole—kama mvua ya kwanza kabla ya mavuno.

Taifa halikuonyeshwa likianguka.

Lilionyeshwa likipitia.

Na kati ya kupita huko, kulikuwa na mgawanyiko wa wale wanaoona na wasioona.

Wapo watakaosema: hakuna kilichotokea.

Na wapo watakaojua: kitu kimeanza.

Kwa maana imeandikwa:

“Bwana hatatenda neno lo lote, asipowafunulia watumishi wake manabii siri yake.” (Amosi 3:7)

Lakini siri haifunuliwi kwa kelele.

Hufunuliwa kwa wale wanaosikiliza kati ya mistari.

Hivyo basi, si kila mtu ataelewa mwanzo huu.

Lakini wale walioonyeshwa, watajua kuwa:

Kilio kimefika.

Na kazi imeanza.

Polepole.

Kwa utaratibu usiotambulika kirahisi.

Mpaka pale ambapo matokeo yake yatakuwa wazi kuliko mwanzo wake.

Nitaendelea…

Karibu kwenye uzi huu wangu

Nafikiri wewe ni mgeni Tanzania au hujui, hii siyo tume ya kwanza kuna tume nyingi tu za kina Nyalali nk ulishawahi kusikia mapendekezo yake yamefanyiwa kazi? Kwani nini tujilishe matumaini hewa. Ni mjinga tu anayetegemea kuwa matokeo ya tume hii yatafanyiwa kazi yawe ya kweli au ya kumlinda muuaji.
Wacha tufanye subra mzee Chande atoe ripoti, halafu kuanzia hapo ndipo tuanze kujadiliana, lugha ngumu na dhana kwa sasa tuweke kando.
 
Leo Chande atatukumbusha wapendwa wetu waliouawa na polisi kwa kupigwa risasi za kichwa.

Leo tutakumbushwa yule mama wa Arusha aliyepigwa risasi ya mgongo akiwa na mimba ya miezi mitatu.

Leo tutakumbushwa wale vijana wa Mwanza waliokuwa wanaangalia mpira wakatolewa nje wote wakapigwa risasi.

Kwa mara nyingine tena leo itasikika vichwani mwetu ile sauti ya "hakuna cha nywinywi wala nywinywinywi".

Leo ni vilio kila sehemu, vilio vipya vya uchungu, ni siku ya maombolezo, siku ya kuililia mama Tanganyika.

Mungu atupe moyo mkuu.

Rest In Peace Mo29 Heroes.
nonsense
 
Watanzania tuna imani Chande
 
Wacha tufanye subra mzee Chande atoe ripoti, halafu kuanzia hapo ndipo tuanze kujadiliana, lugha ngumu na dhana kwa sasa tuweke kando.
Unajua kabisa mtoto sio wako unaenda kupima DNA unampanga dokta aseme ni mtoto wako ili umridhishe jirani, hiyo ni akili au matope.
 
Hii ripoti ya Jaji Chande nani kasema itasomwa leo? Hii ripoti wanamkabidhi aliyewatuma, huyo ndiye atachagua aikubali yote au baadhi, ayafanyie kazi maoni ya tume au ayatumbukize chooni.

Vv
 
Back
Top Bottom