Leo kwa mara ya tatu kujaribu Kitimoto nikajua kwanini haipendwi

Mkuu acha uongo,kitimoto ni maarufu Tanzania nzima dar ikiongoza. Kusema kwamba dar sio maarufu hio ni maajabu ya dunia. Wanaopinga kitimoto sio waislam pekee hata wasabato hawali. Acha kujisingizia ukatoliki mkuu
Watu wengi wanaopinga Kitimoto ni waislamu pia kuhusu Dar naongelea mazingira ya Dar Kitimoto sio maarufu sana hivo inaweza ikawa sababu ya kutoipenda sababu sijakulia nayo. Ukienda Iringa Kitimoto ni nyama maarufu na inapatikana Kila chochoro.
 

Kwanza sio lazima ule kila kitu, and secondly kitimoto sio cheap, kilo moja dar ni elf 16
 
Umelewa mataputapu, mpaka mdomo umekosa taste ? Utaijua ktmt wewe?
 
Huyu kala ile ya mafungu inauzwa buku buku pande kubwaa mara nyingi unakuta nile ya kichwa 😄
 
Huyu kala ile ya mafungu inauzwa buku buku pande kubwaa mara nyingi unakuta nile ya kichwa 😄
Ndio sababu anakuja kujambajamba hapa.

Mwambie aje Bush baby akute vipub vya kitimoto wanavyoshindana mapishi na mchicha kwa wingi offer.
 
Usha wahi kula mchemusho wa
puwa ya nguruwe, masikio ?
 
Unaweza kusema hivo Kwa beef na kuku? Nyama Gani mpaka upate mpishi mzuri ndio iwe tamu? Siwapingi nyie mnaoipenda ila ni an acquired taste kama kahawa tu. Ili upendwe Kitimoto lazima uwe na feelings nayo.
Kahawa na chai kipi bora?
 
Kua na heshima kwa mdudu kijana, yaani comments zote hamna hata moja inayokusupport ndio ujue hilo ni tatizo binafsi.

Tatizo ni kua umeanza kuila ukubwani na pia ushazoea shombo la nyama ya mbuzi na mifupa laini ya broiler ila mdudu ni hatari aisee.
 
Huyo mnyama ni kwa ajili ya kipindi Cha njaa ule ili usife .... ila walafi watakupinga
 
Iringa,mbeya,Dar na Arusha. Kitimoto ni cheap meat kuliko beef na kuku
Ni kwa sababu mdudu anapatikana kwa bei rahisi. Huu ndo ukanda wenye wafugaji wengi wa wadudu.

Mimi ninao kama 50.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…