Leo kwenye Mwendokasi, Mwanadada Askari Polisi ameuteka Moyo wangu. Sijui nitampata vipi?

Leo kwenye Mwendokasi, Mwanadada Askari Polisi ameuteka Moyo wangu. Sijui nitampata vipi?

Rufiji dam

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2020
Posts
4,107
Reaction score
9,671
Leo nimepanda Mwendokasi ya Kivukoni Kimara muda wa saa 6. Nikawahi mbele kwa Dereva ni sehemu naamini ukikosa seat ni sehemu salama sana.

Ndani ya gari nikawa nawaza shillingi ilivyoota matairi. Kufika Fire(faya) mtu aliyekuwa amekalia kiti akashuka nikajisemea acha nami nikae. Ile nageuka nyuma niangalie kama kuna mzee nimpe hicho kikalio aketi tobaa nikakutana na dada mweupeee sura ina vichunusi hivi. Nikajisemea haya njoo ukae.

Akakaa tukataniana kidogo akashukuru sana, akasema "umejuaje kama nimechoka?" Nikamwambia kujidekeza tu akasema hajalala toka jana nikamuuliza upo ofisi gani akajibu tambua tu sikulala. Nikajinyamazia maana kweli alikuwa amechoka.

Kumchunguza nikaona suruali aliyovaa ya dark blue nikajua huyu ni Askari polisi. Nikashindwa hata kuomba namba si unajua kwenye Mwendokasi hakuna faragha nikasema huyu akishuka tu Kimara ninae eeeh akashukia Korogwe. Nikawaza Mdengereko mie mfukoni nina buku mbili ya kunipeleka Matosa.

Nikamsindikiza kwa macho tu akavuka barabara upande wa Korogwe kama unaenda Mbezi.

Ukweli huyu Askari ni mzuri sana. Kama yoyote anayemjua mfikishie salaam. Undugu ni kusaidiana.
 
Ungeshuka tu sasa unateseka moyo kisa nauli ya mwendokasi kutoka Korogwe hadi Kimara? Hata kama nauli ya kwenda huko Matosa ingepungua sio mbaya ungetembea kwa mguu kutoka Korogwe hadi Kimara maana ni karibu tu lakini namba ungekuwa nayo.

Ila mzee wewe muoga sana. Na pakuanzia ulishapata ila umezembea sana.
 
Bora wewe ulimuona wakati anashuka ila mimi kuna siku nilipitiwa na usingizi wakati nataka kuomba namba ile kuamka amekaa babu wa samaki.Usingizi noma
Nimechekaaa kama mwehu. Daah huyu kama leo alikesha J3 ninae hata Dodoma siendi acha nimalize hili jukumu la kujenga nchi kupitia kuzaana. Tuliambiwa tuzae tu.
 
We boya ungemfatilia Hadi ujue ana kaa wapi

Korogwe na kimara kilomita 3 tu unashindwa kutembea
 
Back
Top Bottom