Kwa hiyo Mndengereko wa Mchukwi ukala kwa macho tu!Leo nimepanda Mwendokasi ya Kivukoni Kimara muda wa saa 6. Nikawahi mbele kwa Dereva ni sehemu naamini ukikosa seat ni sehemu salama sana.
Ndani ya gari nikawa nawaza shillingi ilivyoota matairi. Kufika Fire(faya) mtu aliyekuwa amekalia kiti akashuka nikajisemea acha nami nikae. Ile nageuka nyuma niangalie kama kuna mzee nimpe hicho kikalio aketi tobaa nikakutana na dada mweupeee sura ina vichunusi hivi. Nikajisemea haya njoo ukae.