LGE2024 Leo kwenye uchaguzi wa kura za maoni, usanii Mtupu

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

MeVSMe

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2024
Posts
270
Reaction score
425
Wana Jf, wazima? Leo katika pita pita zangu, nilikuwa Kigamboni.

Unaambiwa usanii sio tu kwenye uandikishwaji kwenye daftari. Nimeongea na watu kadhaa pale Kigamboni, Kata ya Vijibweni wanasema Diwani wa Kata hiyo, Zakalia Mkundi siku ya jana alikuwa anafanya kazi ya ugawaji wa Kadi na kuhamasisha watu kuwachagua watu wake anaewataka yeye mwenyewe.

Kwahiyo leo kwenye kura za maoni, tutegemee mengi sana. Hamasa, rushwa ya maneno na kadhalika vimetajwa na watu wa mtaa wa Vijibweni kuwa ndio mienendo ya diwani huyo.

Mengi yaliyosemwa ni kwamba Diwani, yupo madarakani Kwa muda sasa lakini hawaoni maendeleo isipokuwa migogoro isiyokuwa na tija, miongoni mwa migogoro iliyotajwa ni kuwataka wananchi kuondoka kwenye ardhi bila ya kuwapa fidia, wakihusisha na mgogoro wa Pipeline ya Tazama.

Wanasema Diwani alishirikiana na Halimashauri kubomoa majengo ya wakazi wa Kata ya Vijibweni bila fidia, huku wakiambiwa wamevamia.

Wana Jf, naomba wakazi wa Kigamboni Kata ya Vijibweni mtaa wa Mkwajuni na Upendo mtwambie hali halisi.

Miongoni mwa watu niliozungumza nao, amenipa ujumbe WA namna hii
 
 

Attachments

  • Screenshot_2024-07-16-21-00-20-1.png
    420.8 KB · Views: 5
Dah, ukiwafuatilia Hawa watu utajua Kuna mengi nyuma ya pazia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…