Leo mjanja nimekamatika, naona kama nimetapeliwa Tsh. Milioni 1

Leo mjanja nimekamatika, naona kama nimetapeliwa Tsh. Milioni 1

comrade_kipepe

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2019
Posts
3,411
Reaction score
4,435
Jana tarehe 21 Feb 2025 mchana hivi kulikua na tatizo la mtandao CRDB BANK, nilipita ATM kutoa pesa lakini sikufanikiwa mtandao ulikua down Sana! Nikatoka pale nikaendelea na mambo yangu mengine, badae kidogo nikaona nijaribu tena kutoa Kwa wakala maana jua Kali nikaona tena kurud ATM usumbufu.

Wakala nikampa Kadi akauliza kiasi, nikamwambia atoe laki1, akanipa mashine nikaweka namba ya siri, baada ya pale mtandao ikawa inasumbua, nikasubiri kama DK 20 ikawa bado inasumbua, akanipa Kadi namimi nlikua nawahi nikamwambia nipe Kadi maana huku kwangu SMS haijaja pia, ila kuhakikisha isije ikawa pesa imetoka nikaenda tena ATM kuangalia salio, kuangalia salio likawa lipo Sawa hakuna pesa iliopungua, nikajaribu kutoa laki 1 ikatoka, nikaangalia tena salio kuhakikisha kiasi kilichobak, kuangalia ikawa iliobak IPO Sawa ukitoa Ile laki niliotoa pale ATM.

KWA UHAKIKA ZAIDI TENA NIKARUD PALE KWA WAKALA WA CRDB NIKAMWAMBIA ANIPE NAMBA YAKE KAMA SMS IKIJA KWANGU NIRUDI KUCHUKUA PESA, AKANIPA NAMBA NIKAPIGA IKAITA KWAKE NA SIMU ALIKUA NAYO, NIKAONDOKA.

Kichekesho ni Leo nmeenda tena kutoa pesa ATM nimetoa 250,000 ila sasa nahamaki kuangalia salio kuna pungufu ya 1M, nikashtuka Sana nikapanda boda fasta kwenda Kwa wakala WA CRDB, kwenda kafunga, simu haipatikan.

MDA huu nmewapigia CRDB nmewaelezea ishu nzima wakaniambia Jana kuna kiasi cha milion moja kimetoka kwenda Kwa Yule wakala, nikamwambia sasa ananisaidiaje maana nmepita Kwa wakala kafunga na namba haipatikani! Akaniambia Kwa sasabu ni weekend nipite Kesho au jumatatu nikimkuta niwapgie niwape waongee nae Kwa uthibitisho kua Jana imetolewa M1 kwenda Kwa wakala ila kwangu SMS haijarudi.

Kinachofanya nione wakala ni tapeli ni kiasi kilichotoka na nilichosema kitolewe ni tofauti, Leo, kafunga, hapatikani, CRDB huduma Kwa wateja wananitoa hofu wanasema akaunti ya wakala yenye jina la kike IPO vizuri na ni MTU anafanya kazi tuu Hana Kona Kona, nikawaulza mbona jina la wakala la like ila pale nilimkuta dogo mwanaume, akaniambia labda kawekwa kama mfanyakazi

HAPANA NAHISI NIMEPIGWA NIENDEE TUU POLISI KESHO AU NIFANYEJE WAKUU
 
Back
Top Bottom