Leo mjanja nimekamatika, naona kama nimetapeliwa Tsh. Milioni 1

Leo mjanja nimekamatika, naona kama nimetapeliwa Tsh. Milioni 1

Hold on, hizo mashine huwa hazioneshi kiasi? Hiyo ni hatari kubwa na inabidi waubadilishe huo mfumo haraka.

Nilidhani ni mashine kama tunazotumia sehemu za biashara ambazo huwa zinaonesha kiasi.
Akishaweka kiasi, akipress next inakua dot 4 tuu za Mteja kuweka namba ya siri, namba ya siri ukishaandika ukimpa mashine yeye anakua haoni namba yako ya siri,inakua ****
 
Jana tarehe 21 Feb 2025 mchana hivi kulikua na tatizo la mtandao CRDB BANK, nilipita ATM kutoa pesa lakini sikufanikiwa mtandao ulikua down Sana! Nikatoka pale nikaendelea na mambo yangu mengine, badae kidogo nikaona nijaribu tena kutoa Kwa wakala maana jua Kali nikaona tena kurud ATM usumbufu.

Wakala nikampa Kadi akauliza kiasi, nikamwambia atoe laki1, akanipa mashine nikaweka namba ya siri, baada ya pale mtandao ikawa inasumbua, nikasubiri kama DK 20 ikawa bado inasumbua, akanipa Kadi namimi nlikua nawahi nikamwambia nipe Kadi maana huku kwangu SMS haijaja pia, ila kuhakikisha isije ikawa pesa imetoka nikaenda tena ATM kuangalia salio, kuangalia salio likawa lipo Sawa hakuna pesa iliopungua, nikajaribu kutoa laki 1 ikatoka, nikaangalia tena salio kuhakikisha kiasi kilichobak, kuangalia ikawa iliobak IPO Sawa ukitoa Ile laki niliotoa pale ATM.

KWA UHAKIKA ZAIDI TENA NIKARUD PALE KWA WAKALA WA CRDB NIKAMWAMBIA ANIPE NAMBA YAKE KAMA SMS IKIJA KWANGU NIRUDI KUCHUKUA PESA, AKANIPA NAMBA NIKAPIGA IKAITA KWAKE NA SIMU ALIKUA NAYO, NIKAONDOKA.


Kichekesho ni Leo nmeenda tena kutoa pesa ATM nimetoa 250,000 ila sasa nahamaki kuangalia salio kuna pungufu ya 1M, nikashtuka Sana nikapanda boda fasta kwenda Kwa wakala WA CRDB, kwenda kafunga, simu haipatikan.

MDA huu nmewapigia CRDB nmewaelezea ishu nzima wakaniambia Jana kuna kiasi cha milion moja kimetoka kwenda Kwa Yule wakala, nikamwambia sasa ananisaidiaje maana nmepita Kwa wakala kafunga na namba haipatikani! Akaniambia Kwa sasabu ni weekend nipite Kesho au jumatatu nikimkuta niwapgie niwape waongee nae Kwa uthibitisho kua Jana imetolewa M1 kwenda Kwa wakala ila kwangu SMS haijarudi.

Kinachofanya nione wakala ni tapeli ni kiasi kilichotoka na nilichosema kitolewe ni tofauti, Leo, kafunga, hapatikani, CRDB huduma Kwa wateja wananitoa hofu wanasema akaunti ya wakala yenye jina la kike IPO vizuri na ni MTU anafanya kazi tuu Hana Kona Kona, nikawaulza mbona jina la wakala la like ila pale nilimkuta dogo mwanaume, akaniambia labda kawekwa kama mfanyakazi


HAPANA NAHISI NIMEPIGWA NIENDEE TUU POLISI KESHO AU NIFANYEJE WAKUU
B
 
Hold on, hizo mashine huwa hazioneshi kiasi? Hiyo ni hatari kubwa na inabidi waubadilishe huo mfumo haraka.

Nilidhani ni mashine kama tunazotumia sehemu za biashara ambazo huwa zinaonesha kiasi.
Kiasi kinaonekana kwa wakala wakati ana confirm jina. Kwa NMB wakala ana opt ya kuona mpk sura.. akiona sura haifanani na aliye dirishani nae ana haki ya kugoma kutoa hizo pesa.

La msingi ukihudumiwa dai risiti..
 
Ndo umesha Liwa hvyo dogo janja na ukija polisi tunakuchapa 20k ya service yan ni mwendo wa kuzitoa tu
 
Back
Top Bottom