Leo mjanja nimekamatika, naona kama nimetapeliwa Tsh. Milioni 1

Leo mjanja nimekamatika, naona kama nimetapeliwa Tsh. Milioni 1

Wakala anakuuliza kiasi unachotaka kutoa kabla ya Pin number yako kuiweka hapo kama pana ukakasi kidogo ni ngumu wakala kutoa kiasi cha fedha ambacho haujamtajia pili kama hajui pin number yako hawezi kutoa kama haupo na pia anapokuomba namba ya simu lazima utapata meseji hata kwa kuchelewa CRDB itoke hela siku nzima usipate meseji hicho kitu ni ngumu sana labda ianze sasa hivi..
Watu wengine wakiona pisi kali wanamwambia wakala abonyeze number kwa kumtajia Pin number hapo lolote linaweza kutokea..
 
Dogo hawezi kukimbia na M yako kwa sababu anashika pesa nyingi kila siku, kumbuka pesa unayotoa amezishika zote ili akukabidhi wewe hivyo kama ni mwizi angeiba hizo za boss wake hakuna sababu ya kusubiri milioni yako
 
Pole Sana, wakukusaidia ni haohao CRDB, wanaviambatanisho vyote vya wakala.
 
Dogo hawezi kukimbia na M yako kwa sababu anashika pesa nyingi kila siku, kumbuka pesa unayotoa amezishika zote ili akukabidhi wewe hivyo kama ni mwizi angeiba hizo za boss wake hakuna sababu ya kusubiri milioni yako
Wakati utasema, na ikawaje akaweka M1 badala ya laki1? Akaongezaa sifuri
 
Umenikumbusha siku nilikuwa na stress za kuuguza. Nikaenda ATM kutoka laki 2, nikachukua kadi nikasepa bila kuchukua hela. Nafika duka la dawa ndio nakumbuka. Bahati nzuri afande aligundua kichwa changu hakiko sawa. Akanitunzia
Nadhani ulimpooza afande
 
Jana tarehe 21 Feb 2025 mchana hivi kulikua na tatizo la mtandao CRDB BANK, nilipita ATM kutoa pesa lakini sikufanikiwa mtandao ulikua down Sana! Nikatoka pale nikaendelea na mambo yangu mengine, badae kidogo nikaona nijaribu tena kutoa Kwa wakala maana jua Kali nikaona tena kurud ATM usumbufu.

Wakala nikampa Kadi akauliza kiasi, nikamwambia atoe laki1, akanipa mashine nikaweka namba ya siri, baada ya pale mtandao ikawa inasumbua, nikasubiri kama DK 20 ikawa bado inasumbua, akanipa Kadi namimi nlikua nawahi nikamwambia nipe Kadi maana huku kwangu SMS haijaja pia, ila kuhakikisha isije ikawa pesa imetoka nikaenda tena ATM kuangalia salio, kuangalia salio likawa lipo Sawa hakuna pesa iliopungua, nikajaribu kutoa laki 1 ikatoka, nikaangalia tena salio kuhakikisha kiasi kilichobak, kuangalia ikawa iliobak IPO Sawa ukitoa Ile laki niliotoa pale ATM.

KWA UHAKIKA ZAIDI TENA NIKARUD PALE KWA WAKALA WA CRDB NIKAMWAMBIA ANIPE NAMBA YAKE KAMA SMS IKIJA KWANGU NIRUDI KUCHUKUA PESA, AKANIPA NAMBA NIKAPIGA IKAITA KWAKE NA SIMU ALIKUA NAYO, NIKAONDOKA.


Kichekesho ni Leo nmeenda tena kutoa pesa ATM nimetoa 250,000 ila sasa nahamaki kuangalia salio kuna pungufu ya 1M, nikashtuka Sana nikapanda boda fasta kwenda Kwa wakala WA CRDB, kwenda kafunga, simu haipatikan.

MDA huu nmewapigia CRDB nmewaelezea ishu nzima wakaniambia Jana kuna kiasi cha milion moja kimetoka kwenda Kwa Yule wakala, nikamwambia sasa ananisaidiaje maana nmepita Kwa wakala kafunga na namba haipatikani! Akaniambia Kwa sasabu ni weekend nipite Kesho au jumatatu nikimkuta niwapgie niwape waongee nae Kwa uthibitisho kua Jana imetolewa M1 kwenda Kwa wakala ila kwangu SMS haijarudi.

Kinachofanya nione wakala ni tapeli ni kiasi kilichotoka na nilichosema kitolewe ni tofauti, Leo, kafunga, hapatikani, CRDB huduma Kwa wateja wananitoa hofu wanasema akaunti ya wakala yenye jina la kike IPO vizuri na ni MTU anafanya kazi tuu Hana Kona Kona, nikawaulza mbona jina la wakala la like ila pale nilimkuta dogo mwanaume, akaniambia labda kawekwa kama mfanyakazi


HAPANA NAHISI NIMEPIGWA NIENDEE TUU POLISI KESHO AU NIFANYEJE WAKUU
Mimi nililipa 620k kwa lipa namba kwa mpesa app,ile nimelipa tu mtandao uka collapse,na meseji haijaja,nikamwambia mwenye duka ngoja nilipe kwa njia ya *150*00#,nikalipa na meseji ya mpesa ikaja.
Nimekaa dk 5,imeingia meseji nyingine kuwa nimelipa 620k,na salio limekatwa,nikamwambia mwenye duka nae akaona kweli.niliwapigia Vodafone walirudisha muamala baada ya massage 48.
 
Wakala naogopa kwanza makato pili Janjajanja nyingi sana yaani wamejaa na tamaa lakini pia mkuu ikiwa huyo dogo anashinda na mamilioni ya Hela humo ofisini kwake anawezaje kukimbia na hela kama hiyo ingawa sijawahi kuishika
 
Wakala naogopa kwanza makato pili Janjajanja nyingi sana yaani wamejaa na tamaa lakini pia mkuu ikiwa huyo dogo anashinda na mamilioni ya Hela humo ofisini kwake anawezaje kukimbia na hela kama hiyo ingawa sijawahi kuishika
Viofisi vya vinanda vya bati vile vya anaingia MTU mmoja SIO vya kuamini sana
 
Je ni lazima wakala aweke hela au wewe ndio unaweka hizo tarakimu?
Haya mjanja umeweka namba ya siri bila kuangalia unatoa ngapi?
Hapo ni kama una saini kitu usichokijua pole
Ila bongo system korofi sana
 
Hiyo ni pesa ndogo sana atakuwa anajitafutia matatizo tu.

Bora hata zingekuwa 10.
Watu wanakimbia ofisi na laki 2 mkuu as long as msala utakua kwa boss au kwa kudhani boss hatajua.
 
Back
Top Bottom