Leo mjanja nimekamatika, naona kama nimetapeliwa Tsh. Milioni 1

Leo mjanja nimekamatika, naona kama nimetapeliwa Tsh. Milioni 1

Hela yako utapata bila wasiwasi Ila usipendee kutoa hela Kwa wakala tumia zaidi sm banking
Mkuu kama ni aina ya transaction ilichopitishwa na benki basi inatakiwa iwe safe features zote na namna ya kufuatilia matukio kama haya. I mean kama wanaona wateja wengi wanapigwa kwa njia hii, basi waiondoe.
 
Mkuu, utathibitishaje sasa kuwa hukupewa hiyo 1m?
Atadhibitisha kwa kuonyesha kuchelewa kwa msg ya kutoa pesa kuingia kwenye simu yake.

Inaeleweka wakala hatoi pesa mpaka msg irudi.
Pia kuwasilisha malalamiko yake CRDB Itamsaidia.

Akizembea iitakula kwake lakini.
 
Pesa imetoka baada ya kama lisaa kimoja na nusu baada ya Mimi kuondoka Kwa wakala
Utathibitishaje kuwa uliondoka hilo saa moja na nusu ndipo pesa ikatoka?? Yaani utathibitishaje kuwa hukuwepo hapo wakati pesa inatoka?
 
Utathibitishaje kuwa uliondoka hilo saa moja na nusu ndipo pesa ikatoka?? Yaani utathibitishaje kuwa hukuwepo hapo wakati pesa inatoka?
Wenyewe wamethibitisha kua kweli kulikua na shida ya mtandao, kuna miamala ilitoka badae, sasa wewe unabishana na CRDB wenyewe? Au hujasoma ukaelewa
 
Wewe ndiye uliweka namba ya siri kudhibitisha muamala☺️
🤣🤣🤣🤣🤣 Ushawahi kutoa pesa Kwa wakala? ndio niliweka na lazima uweke, inawezekana hata hujawah kutumia hizo huduma hujui hata nini kinazungumzwa hapa
 
Atadhibitisha kwa kuonyesha kuchelewa kwa msg ya kutoa pesa kuingia kwenye simu yake.

Inaeleweka wakala hatoi pesa mpaka msg irudi.
Pia kuwasilisha malalamiko yake CRDB Itamsaidia.

Akizembea iitakula kwake lakini.
mpaka sasa hajapata meseji ya kuonesha kuwa ametoa Tshs. 1,000,000/=

Sasa kama wakala atasema kuwa muamala ulikamilika na akatoa risiti ya kuonesha muamala umekamilika na akampa fedha mteja, unathibitishaje kuwa hukupewa fedha??
 
Yani sielewi maana nmewapigia CRDB wakaniambia labda kwakua ni weekend ndio mana wamefunga, niende jumatatu kama sijafanikiwa niwajulishe, maana wanasema account ya huyo wakala IPO vizuri tuu na ni MTU anafanya miamala
Wewe subiri Jumatatu uone kama watafungua. Ukienda polisi sasa hivi utapoteza muda bure.
 
Anashindaje

Wakala nikampa Kadi akauliza kiasi, nikamwambia atoe laki1, akanipa mashine nikaweka namba ya siri

Yaani tarakimu ya pesa kaweka wakala (wewe ulitaka aweke 100,000 lakini unadhani aliweka 1,000,000)...
Akabonyeza "Enter"

Akakukabidhi POS uweke tarakimu za siri...
Ukabonyeza "Enter" kuthibitisha

Utaratibu ni kwamba unapokuwa kwenye POS ya wakala ni kama tu unavyokuwa kwa ATM,mwenye kuweka tarakimu za ama pesa au neno siri ni mtoa/muweka pesa
 
CRDB WENYEWE WANASISITIZA NISUBIRI MPAKA KESHO AFUNGUE NIMWAMBIE ANIPE PESA, KAMA ATAKATAA NIWAPIGIE KWA NAMBA YAO WAONGEE NAE, NIMEWAULIZA KUHUSU KWENDA POLISI, WANANIAMBIA TENA ILI HILI SUALA LISHUGHULIKIWE HARAKA NIFANYE WALICHONIAMBIA
 
Wenyewe wamethibitisha kua kweli kulikua na shida ya mtandao, kuna miamala ilitoka badae, sasa wewe unabishana na CRDB wenyewe? Au hujasoma ukaelewa
Nimesoma na kuelewa vizuri, mimi nakuuliza wewe maswali ili utetee vyema hoja yako.

Hapa suala la kuwahi au kuchelewa kwa muamala sio ishu, maana mfano ungesubiri mpaka huo muda fedha imetoka, si ungeichukua, je kungekuwa na mgogoro wowote?? Jibu ni hapana

Sasa kwa kuwa hukuichukua, hoja ni namna ya kuthibitisha kuwa hukuichukua. Kama kungekuwa na camera ingekua rahisi sana ila kama hakuna camera, ni kipi kitakufanya wewe uaminike na sio wakala, incase akisema kuwa fedha ilivyotoka ulikuwepo na alikukabidhi!!
 
🤣🤣🤣🤣🤣 Ushawahi kutoa pesa Kwa wakala? ndio niliweka na lazima uweke, inawezekana hata hujawah kutumia hizo huduma hujui hata nini kinazungumzwa hapa
Ndio maana umetapeliwa sababu haupo makini, unashindwa kung'amua kua haya maswali hata huko polisi utaulizwa na sisi tupo hapa kukuchallenge ili ujiandae na majibu utakayoulizwa huko.

Maelezo yako pekee hayatoshi kuonyesha kua huyo wakala kakutapeli bila kua na ushahidi.
 
Huyo dogo tu anataka kukupiga.
Iliwahi nitokea hiyo kwa wakala wa nmb,mbona alinipa pesa yangu tu bila shida
 
Nimesoma na kuelewa vizuri, mimi nakuuliza wewe maswali ili utetee vyema hoja yako.

Hapa suala la kuwahi au kuchelewa kwa muamala sio ishu, maana mfano ungesubiri mpaka huo muda fedha imetoka, si ungeichukua, je kungekuwa na mgogoro wowote?? Jibu ni hapana

Sasa kwa kuwa hukuichukua, hoja ni namna ya kuthibitisha kuwa hukuichukua. Kama kungekuwa na camera ingekua rahisi sana ila kama hakuna camera, ni kipi kitakufanya wewe uaminike na sio wakala, incase akisema kuwa fedha ilivyotoka ulikuwepo na alikukabidhi!!
Huyu jamaa ni m'bishi sana.
 
Huyo dogo tu anataka kukupiga.
Iliwahi nitokea hiyo kwa wakala wa nmb,mbona alinipa pesa yangu tu bila shida
Nahuyu namsubiria, labda asifungue na Kesho naenda POLISI, watu kama nyie ndio napenda maoni yenu maana mnajua ninachokiongelea, wengine hawaelewi kitu
 
UZI HUU NI KWA AJILI YA WANAOJUA NINACHOZUNGUMZIA NA WALIOWAHI KUPITIA, AMBAO HAMJUI KITU KUHUSU HIZI HUDUMA HUU SIO UZI WENU
 
Wenyewe wamethibitisha kua kweli kulikua na shida ya mtandao, kuna miamala ilitoka badae, sasa wewe unabishana na CRDB wenyewe? Au hujasoma ukaelewa
Mkuu pengine hujaelewa sajo anachojaribu kusema. Nadhani anasema kama huyo wakala atasema ulisubiri mpaka muamala ukakamilika na akakupa fedha zako ukaondoka, unaweza kuthibitishaje kuwa hukupewa? Na mbaya zaidi anaweza kuweka na shahidi wa uongo. Ni nadharia ya mtu kukukana kwa kitu cha ukweli. Kwa mfano mimi niliwahi kumlipa mtu fedha ya kibarua alichofanya kwa siku moja. Kesho yake akakana macho makavu na akasema hukunipa na kama ulinipa lete ushahidi. Nlikwama kwa sababu sikuandika popote ili asaini na pia hakukuwa na shahidi. Anyway, japo jambo kama hili ni nadra kutokea lakini ni vizuri kupanua mjadala.
 
Back
Top Bottom