Leo mjanja nimekamatika, naona kama nimetapeliwa Tsh. Milioni 1

Leo mjanja nimekamatika, naona kama nimetapeliwa Tsh. Milioni 1

Kutoa hela kwa wakala si salama sana japo Kuna mazingira yanakulazimu kufanya ivo!

Mimi Kuna wakala, brother fulani maeneo ya njia panda ya segerea niliwahi kwenda kwake kutoa hela!

Nikatoa mara ya kwanza mtandao ukagoma!

Nikarudia kutoa mara ya pili ikakubali ilikuwa ni laki 4 na 50

Zikapita wiki mbili .. Nikaenda ATM kutoa hela naambiwa hakuna hela!

Kuwapigia simu watu wa NMB wakaniambia siku Ile nilifanya miamala 2 kwa wakati mmoja!

Nilivyorudi kwa jamaa kumuelezea na kumtajia na tarehe akaona ni kweli akanirudishia hiyo fedha

Tola siku hiyo, nikiwa na miamala wa kufanya naenda kwake!
Mnawasingizia wakala bure, hata kwenye ATM unaweza kutowa pesa mashine isitowe pesa, ukitowa kadi akiingia mtu mwingine anazikuta pesa zimetoka.

Nilishawahi kuzikuta pesa zimetoka jamaa kaondoka lakini nilimuita aje kuchukuwa pesa zake.
 
Mnawasingizia wakala bure, hata kwenye ATM unaweza kutowa pesa mashine isitowe pesa, ukitowa kadi akiingia mtu mwingine anazikuta pesa zimetoka.

Nilishawahi kuzikuta pesa zimetoka jamaa kaondoka lakini nilimuita aje kuchukuwa pesa zake.
Sasa nimsingizie wakala ili nipate faida Gani mkuu? Katika maelezo yangu hapo ni kipi ambacho nime kiongea ambacho ni negative dhidi ya wakala?

Hakika mkuu una kipengele afu ni wewe dokita kabisa
 
Jana tarehe 21 Feb 2025 mchana hivi kulikua na tatizo la mtandao CRDB BANK, nilipita ATM kutoa pesa lakini sikufanikiwa mtandao ulikua down Sana! Nikatoka pale nikaendelea na mambo yangu mengine, badae kidogo nikaona nijaribu tena kutoa Kwa wakala maana jua Kali nikaona tena kurud ATM usumbufu.

Wakala nikampa Kadi akauliza kiasi, nikamwambia atoe laki1, akanipa mashine nikaweka namba ya siri, baada ya pale mtandao ikawa inasumbua, nikasubiri kama DK 20 ikawa bado inasumbua, akanipa Kadi namimi nlikua nawahi nikamwambia nipe Kadi maana huku kwangu SMS haijaja pia, ila kuhakikisha isije ikawa pesa imetoka nikaenda tena ATM kuangalia salio, kuangalia salio likawa lipo Sawa hakuna pesa iliopungua, nikajaribu kutoa laki 1 ikatoka, nikaangalia tena salio kuhakikisha kiasi kilichobak, kuangalia ikawa iliobak IPO Sawa ukitoa Ile laki niliotoa pale ATM.

KWA UHAKIKA ZAIDI TENA NIKARUD PALE KWA WAKALA WA CRDB NIKAMWAMBIA ANIPE NAMBA YAKE KAMA SMS IKIJA KWANGU NIRUDI KUCHUKUA PESA, AKANIPA NAMBA NIKAPIGA IKAITA KWAKE NA SIMU ALIKUA NAYO, NIKAONDOKA.


Kichekesho ni Leo nmeenda tena kutoa pesa ATM nimetoa 250,000 ila sasa nahamaki kuangalia salio kuna pungufu ya 1M, nikashtuka Sana nikapanda boda fasta kwenda Kwa wakala WA CRDB, kwenda kafunga, simu haipatikan.

MDA huu nmewapigia CRDB nmewaelezea ishu nzima wakaniambia Jana kuna kiasi cha milion moja kimetoka kwenda Kwa Yule wakala, nikamwambia sasa ananisaidiaje maana nmepita Kwa wakala kafunga na namba haipatikani! Akaniambia Kwa sasabu ni weekend nipite Kesho au jumatatu nikimkuta niwapgie niwape waongee nae Kwa uthibitisho kua Jana imetolewa M1 kwenda Kwa wakala ila kwangu SMS haijarudi.

Kinachofanya nione wakala ni tapeli ni kiasi kilichotoka na nilichosema kitolewe ni tofauti, Leo, kafunga, hapatikani, CRDB huduma Kwa wateja wananitoa hofu wanasema akaunti ya wakala yenye jina la kike IPO vizuri na ni MTU anafanya kazi tuu Hana Kona Kona, nikawaulza mbona jina la wakala la like ila pale nilimkuta dogo mwanaume, akaniambia labda kawekwa kama mfanyakazi


HAPANA NAHISI NIMEPIGWA NIENDEE TUU POLISI KESHO AU NIFANYEJE WAKUU

Hakuna wakala wa crdb na M-Pesa anaweza kimbia na 1m, acha wenge! Labda Kama ni muajiriwa, na Kama ni muajiriwa, mwenye office atawajibika, ingawa akikomaa unaweza usiwe na base ya kumshtaki!
 
Rudi kwa wakala pesa yako haipotei wewe utakomaa na CRDB, ndio waliompa dhamana ya kutoa huo huduma,
Pesa Yako Iko salama kabisa hata kama atakua kapiga huyo dogo aliyeajirwa bado mwenye hyo Atawajibika
 
Never, Tembea na RB mkuu akileta ujanja ujanja hio Kesho ita polisi kwa utaratibu weka mtu korokoroni...

Ushauri wangu ulishaokoa wengi na wanitumia sadaka kwa uaminifu mkubwa
Kesho nikienda hajafungua, kwanza namtafuta dada Yake ambae alimuweka kwenye kile kibanda, Leo nimefanya upelelezi mzuri nshajua naanzia wapi Kesho, huyo dada Yake nae nisipompata naenda polisi
 
Kesho nikienda hajafungua, kwanza namtafuta dada Yake ambae alimuweka kwenye kile kibanda, Leo nimefanya upelelezi mzuri nshajua naanzia wapi Kesho, huyo dada Yake nae nisipompata naenda polisi
Ushapigwa wewe usipoteze mda endelea na mambo mengine
 
Hakuna wakala wa crdb na M-Pesa anaweza kimbia na 1m, acha wenge! Labda Kama ni muajiriwa, na Kama ni muajiriwa, mwenye office atawajibika, ingawa akikomaa unaweza usiwe na base ya kumshtaki!
Namimi ndio nataka hiyo Kesho akomae, ili tuonyeshane ukenge
 
Yani sielewi maana nmewapigia CRDB wakaniambia labda kwakua ni weekend ndio mana wamefunga, niende jumatatu kama sijafanikiwa niwajulishe, maana wanasema account ya huyo wakala IPO vizuri tuu na ni MTU anafanya miamala
Hili ndilo limefanya nikuambie hutakiwi kuwaza.
 
mpaka sasa hajapata meseji ya kuonesha kuwa ametoa Tshs. 1,000,000/=

Sasa kama wakala atasema kuwa muamala ulikamilika na akatoa risiti ya kuonesha muamala umekamilika na akampa fedha mteja, unathibitishaje kuwa hukupewa fedha??
Haiwi rahisi hivyo. Kama una mpango wa kumtapeli mtu kwa njia hiyo hakikisha unaandaa na fedha ya kugharamia kesi
 
Ushauri wangu KAMA ATM INASUMBUA USITOE PESA KWA WAKALA, NI WASUMBUFU MNO
 
Back
Top Bottom