Leo nakutajia na kukuelezea aina 4 za kuku Asili(kienyeji pure) Kwa kina

Leo nakutajia na kukuelezea aina 4 za kuku Asili(kienyeji pure) Kwa kina

Mkuu nadhan kwenye utafiti wako umewatambua kuku kutokana na rangi zao na sio vinginevyo kwa maana umetumia uzoefu wa mazingira yako.
Mkuu kwa huku tabgu tunazaliwa hayo ndo majina waliyokuwa wanaitwa siku zote hadi. na hata baadhi ya vitabu vya kuku asili vimetaja vivyo hivyo. Aina zipo nyingi sana mkuu nadhani kam,a ningejikita kwenye rangi pekee usingekosa rangi nyekundu,kijivu,nyeusi nk.
 
Je wanaingiliana kwa jamii zao tofauti?na mbegu gani na tabia gani hutokea kama kuchi akimpanda na kutoa mbegu na Rangi ya kanga
Kama ujuavyo atachukua nusu kwa baba na kwa maa nusu. kwa kuchi hasa mara nyingi manyoya huwa ni machache na pia simama yake hawezi simama kama kuchi halisi na hawezi simama kama rangi ya kanga. akiwa jike mara nyingi kwenye utagaji atakopi kwa mama.
 
Hivi Wakuu jogoo la kucho linaweza likarutubisha mayai ya aina nyingine za kuku?
Ndio mkuu. hasa ukitafuta jike la horasi ni ngumu sana kuja kumtofautisha na kuchi og otherwise uwe una uelewa wa kina. Au kwenye mdomo afanane na jike hapo ndo utaweza kumtambua kwa upesi zaidi
 
Asante mkuu kwa maarifa, Katika hizo aina zote tajwa hapo juu ni aina ipi inapendwa sokoni lakini pia haivamiwi na magonjwa kwa urahisi.
Hao wote wananunulika vizuri sana mkuu na kwa magonjwa wote wana stahimili vizuri mno. kuchi soko lake ni wachache kulingana na bei zake ni ngumu kwa mtu anayeenda kula tu anunue kwa 250k naamini hata wewe huwezi hiyo hela ni wastani wa mbuzi2 kabisa.

mimi napenda singamazi na horasi maana hawaitaji hadi uwe na majike mengine ya kuatamia kama kuchi.
 
Mimi namba mwenye picha ya kuku hai wa Ile minofu mikubwa naiona inauzwa uswahili, Buguruni, Vingunguti, Mbagala. Kipande kinaizwa hadi elfu 6 najiuliza huyu kuku yukoje?
Mkuu wengi huwa ni horasi maana ni warefu sana na huwa hawanenepi sana ila nyama yao ikipikwa huvimba ama kuumka. Kuna wengine huwa warefu sana kiasi kwamba baada ya muda flani tu uzito ukizidi huteguka na kushindwa hata kutembea. Nina jogoo nikipiga p[icha yake nitakuwekea mkuu japo nashukuru hajarefu sana kushindwa kuhimili mwili wake
 
Back
Top Bottom