Leo naomba mniulize chochote kuhusu mimi

Leo naomba mniulize chochote kuhusu mimi na pia ningependa niweke wazi kuwa sitataja jina langu wala sehemu ninayofanyia kazi
Funza mbona hunijibu nauliza hivi "Nawezaje kuita media nitoe ya moyoni hali ya kuwa mimi choka mbaya"?
 
1.Kabila gani?
2.Unaishi wapi kwa Sasa? 3.Ukifa ungependa ukazikiwe wapi?
4.Umeoa au Umeolewa?
5.Unawatoto wangapi?
6. Wanasoma wapi ?
7.Upo chama gani ?
8.Kiongozi gani unamuona anafanyakazi vizuri hata nje ya chama chako hapa Tanzania?

1.Kabila gani? Mnyamwezi
2.Unaishi wapi kwa Sasa? Dar / Moro (kibiashara) na Dodoma ila now niko Dar
3.Ukifa ungependa ukazikiwe wapi? Sijajua nadhani watakaobaki ndio watahamua
4.Umeoa au Umeolewa? Nimeoa
5.Unawatoto wangapi? Watatu
6. Wanasoma wapi ? Wawili Feza Boys Sec mmoja St. Mary (Primary)
7.Upo chama gani ? Sijuhusishi na siasa kabisa
8.Kiongozi gani unamuona anafanyakazi vizuri hata nje ya chama chako hapa Tanzania? Kiongozi anayefanya kazi vizuri ni Mh. William Lukuvi nina mfano mmoja niliwahi kutafuta hati ya eneo kwa miaka kumi mpk nikakata tamaa lakini alipoingia kwenye hiyo wizara nilipigiwa simu nikaifuate. Pia anafanya kazi yule mzee Mungu ambariki. Hati ya kiwanja ilikuwa mtihani sana hapa nchini
 
Funza mbona hunijibu nauliza hivi "Nawezaje kuita media nitoe ya moyoni hali ya kuwa mimi choka mbaya"?
Nilijibu post namba #81 ila naruduia tena
Inategemea na nini unachotaka kukiongea kama ni habari utasikilizwa. Wanahabari kazi yao ni kuuza habari kwa hiyo kama habari yako inauza watakusikiliza
 
[emoji23][emoji23][emoji7][emoji7]haya my wangu[emoji23][emoji23][emoji23][emoji125][emoji125][emoji125][emoji125][emoji125][emoji125]
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Hongera mkuu, mambo yako si haba kama unavyojipambanua, kumudu ada ya Feza Boys kwa watoto wawili si jambo la mchezo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…