Kama Rais Samia alianza dk za mwanzo tu za mchezo kuupiga mwingi sana. Wapinzani tulifurahia na kauli mbiu Mama anaupiga mwingi. Kipo wapi?
Ujinga ule ule wapinzani wameubeba na kuanza kumpamba kijana muasisi wa bao la mkono kuwa kwa kuhoji deni la Magufuli anaupiga mwingi. Unajiuliza huu unafiki wa Nape mpaka leo wapinzani hawajifunza?
Si kila anayemshambulia Magufuli leo ni Mzalendo. Muulizeni Alikighu? Alikwii? Alikuwa wapi? Wakati ninyi mnapinga mambo mbalimbali yeye alifanya nini? Huyu si ndo alienda kuomba msamaha huku akicheka cheka ili abaki na Ubunge? Na kuwaponda wenzie kwa Magufuli?
Leo anaupiga mwingi? Si lazima kila sehemu mtie mkono mambo mengine mngeyaacha tu. Mimi nimejikuta sasa namwelewa Magufuli kuliko hata zamani. Hawa watu wanafiki ni wabaya kuliko hata akina sabaya ambao walijipambanua mapema wao ni watu wa namna gani.
Shauri zenu. Kuna siku Nape ataongea tena maneno mtamshukia kama Kipanga.