Leo nataka tuweke Ushabiki wetu wa Simba na Yanga pembeni na tulijadili hili Kiuanamichezo kwa Faida ya Soka letu

Leo nataka tuweke Ushabiki wetu wa Simba na Yanga pembeni na tulijadili hili Kiuanamichezo kwa Faida ya Soka letu

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Hivi kweli kabisa Logically hizi Klabu zetu pendwa nchini za Simba SC na Yanga SC kwa Uswahili uliozitawala na Ujanja Ujanja ( Usamjo Usamjo ) ni za Kudhaminiwa Bilioni 26.1 na Mbet kwa Miaka Mitano na Bilioni 12 na Sports Pesa kwa Miaka Mitatu?

Klabu pekee nchini Tanzania kutokana na Structure yake na high level of Professionalism iliyonayo ( iliyopo ) ningeambiwa imedhaminiwa kwa Mabilioni hayo ningeamini upesi kwa 100%, ila siyo kwa Simba SC na Yanga SC.

Kwa mfano utaniambiaje GENTAMYCINE kuwa Umenidhamini kwa Tsh Bilioni 26,168,005,000/= halafu kila mwaka unanigawia Pesa Kimgawanyo usio sawa badala ya kunipa Tsh Bilioni 5,233,601,000/= ambayo ndiyo ninapaswa nipewe?

Mfano utaniambiaje GENTAMYCINE kuwa unanipa Tsh Bilioni 12 kwa Miaka Mitatu na kwamba kila mwaka utakuwa unanipa Tsh Bilioni 4 huku ukijua kuwa Timu yangu bado haina ( haijapata ) kivile Mafanikio ya Kimataifa ambayo yangesaidia Kuiongezea Thamani?

Nisizunguke sana na GENTAMYCINE sijazoea Unafiki ukweli ni kwamba hizi Sponsorship Deals zote ni za Kupikwa ili Kuwahadaa Mashabiki Wajinga ( Ngumbaru ) na Wapumbavu ( Popoma ) ambao Masikini ya Mungu Wengi Wao uwezo wao wa Kuchanganua Mambo ni Finyu ( Mdogo ) sana na Pole yao pia.

Najua kuna mtakaosema kuwa kama hii Mikataba waliyoingia hivi Vilabu Vikubwa Viwili vya Tanzania ni vya Magumashi ( Uwongo ) mbona TRA na Watu wa Gaming Board walikuwepo?

Ukweli ni kwamba kwa Watendaji dhaifu na wepesi Kuhongwa kutoka katika hizi Taasisi tajwa hapo juu sitoshangaa kusikia kuwa nao waliitwa Kwanza Maji Mafupi ( Chemba ) kisha Wakasukwa na Kusukika kwa Ahadi ya 10% ili tu Wauchune ( Wanyamaze ) wakati hivi Vilabu viwili vikicheza na Akili za Mashabiki wao ( zao )

Kuna Mtendaji wa Kampuni Moja iliyodhamini Moja ya Klabu hizi nimemuangalia alipokuwa akiwasilisha Details za Mkataba na Usoni mwake ameonekana kabisa Dhambi ya Uwongo inamsuta na anadanganya wazi wazi baada ya Kufuzu Maelekezo ya Kuwadanganya Mashabiki, Wapenzi na Wanachama.

Hakuna sijui wa B26.1 wala wa B12 Ok?
 
Vitu vya Simba huwa vinajadiliwa sana. Ila ndiyo ukubwa wenyewe huo. Tufanye hui mkataba hauwezekani, ni nani anayepata hasara?! Na wadanganye Kwa faida ya nani?! Maumivu mengine inatakiwa myakubali tu. Maana kuna watu wako Hoi.
 
Hizo pesa sisi kama mashabiki hatufaidiki na lolote wagawe nusu nusu au yote kamili sisi hatuna haja ya kuyajua hayo..

Mpira ni entertainment na Fans tunataka burudani ya matokeo chanya na usajili mzuri katika Clubs zetu ili uweze kuwa Competitve kimataifa.
 
Mabilion ya hela kwa faida gani ambayo hiyo mdhamini anategemea kupata baada ya kuwekeza kiwango hicho?

Kama mmefikia hatua ya kujiona wakubwa mlipaswa muwe na uwezo wa ku make hiyo Bilion 5 kwa mwaka bila shida ili hata mdhamini akija aanzie kiwango cha juu

Yanga pamoja na kuchukua vikombe karibia vyote hapa tanzania lakini bado hajafikisha B2

Na hapo ukumbuke ndio mwaka ambao dau limeongezwa

Sasa Club hii ikiambiwa inapewa B4 kwa mwaka si neema kabisa hiyo?

Huwezi ukasema M100 wakati hujawahi iona hata inafananaje, na sometimes hata ujikusanye kusanye kwa miaka 10 unaweza usifikie

M-Bet tuwape heshima zao, naamini next round Yanga haitakubali kusaini mkataba wa kiwango hiki ambacho juzi walifurahia na leo wamekuwa wanyonge
 
Hivi kweli kabisa Logically hizi Klabu zetu pendwa nchini za Simba SC na Yanga SC kwa Uswahili uliozitawala na Ujanja Ujanja ( Usamjo Usamjo ) ni za Kudhaminiwa Bilioni 26.1 na Mbet kwa Miaka Mitano na Bilioni 12 na Sports Pesa kwa Miaka Mitatu?

Klabu pekee nchini Tanzania kutokana na Structure yake na high level of Professionalism iliyonayo ( iliyopo ) ningeambiwa imedhaminiwa kwa Mabilioni hayo ningeamini upesi kwa 100%, ila siyo kwa Simba SC na Yanga SC.

Kwa mfano utaniambiaje GENTAMYCINE kuwa Umenidhamini kwa Tsh Bilioni 26,168,005,000/= halafu kila mwaka unanigawia Pesa Kimgawanyo usio sawa badala ya kunipa Tsh Bilioni 5,233,601,000/= ambayo ndiyo ninapaswa nipewe?

Mfano utaniambiaje GENTAMYCINE kuwa unanipa Tsh Bilioni 12 kwa Miaka Mitatu na kwamba kila mwaka utakuwa unanipa Tsh Bilioni 4 huku ukijua kuwa Timu yangu bado haina ( haijapata ) kivile Mafanikio ya Kimataifa ambayo yangesaidia Kuiongezea Thamani?

Nisizunguke sana na GENTAMYCINE sijazoea Unafiki ukweli ni kwamba hizi Sponsorship Deals zote ni za Kupikwa ili Kuwahadaa Mashabiki Wajinga ( Ngumbaru ) na Wapumbavu ( Popoma ) ambao Masikini ya Mungu Wengi Wao uwezo wao wa Kuchanganua Mambo ni Finyu ( Mdogo ) sana na Pole yao pia.

Najua kuna mtakaosema kuwa kama hii Mikataba waliyoingia hivi Vilabu Vikubwa Viwili vya Tanzania ni vya Magumashi ( Uwongo ) mbona TRA na Watu wa Gaming Board walikuwepo?

Ukweli ni kwamba kwa Watendaji dhaifu na wepesi Kuhongwa kutoka katika hizi Taasisi tajwa hapo juu sitoshangaa kusikia kuwa nao waliitwa Kwanza Maji Mafupi ( Chemba ) kisha Wakasukwa na Kusukika kwa Ahadi ya 10% ili tu Wauchune ( Wanyamaze ) wakati hivi Vilabu viwili vikicheza na Akili za Mashabiki wao ( zao )

Kuna Mtendaji wa Kampuni Moja iliyodhamini Moja ya Klabu hizi nimemuangalia alipokuwa akiwasilisha Details za Mkataba na Usoni mwake ameonekana kabisa Dhambi ya Uwongo inamsuta na anadanganya wazi wazi baada ya Kufuzu Maelekezo ya Kuwadanganya Mashabiki, Wapenzi na Wanachama.

Hakuna sijui wa B26.1 wala wa B12 Ok?
Long live legendary I.A Rage

WanaSimba wote ni mbumbumbu - I.A Rage, 16th March 2014.
 
Hivi kweli kabisa Logically hizi Klabu zetu pendwa nchini za Simba SC na Yanga SC kwa Uswahili uliozitawala na Ujanja Ujanja ( Usamjo Usamjo ) ni za Kudhaminiwa Bilioni 26.1 na Mbet kwa Miaka Mitano na Bilioni 12 na Sports Pesa kwa Miaka Mitatu...
Product ya SAUT hii
 
Hujielewi, unawaita wajinga wanaoamini hiyo mikataba ila wewe unaeamini mikataba ya uongo hauna ushahidi wa mikataba halisi waliyoingia wadhamini wa hivyo vilabu na timu husika utuwekee hapa.

Dili la Simba SC limewafanya wengi mchanganyikiwe, hamuamini macho yenu.
 
Hujielewi, unawaita wajinga wanaoamini hiyo mikataba ila wewe unaeamini mikataba ya uongo hauna ushahidi wa mikataba halisi waliyoingia wadhamini wa hivyo vilabu na timu husika utuwekee hapa...
Mtamtukana Sana Genta Kwa sababu Tabia yake ya ukweli ni ngumu kuiiga. Mfano mdogo tu nikifuatisha ushabiki maandazi wenu unaoshangilia Kila kitu bila kuhoji; Ni lini mkataba ukathibitishwa Kwa kutengenezewa jezi?

Siyo timu hizi ambazo zinapenda kufurahisha mashabiki Kwa uongo ambapo moja ilichapisha mkataba wa awali wa Uongo na mchezaji waliyemkosa na kuusambaza mitandaoni? Mliwafanya nini mlipogundua viongozi wamewadanganya?
 
Mtamtukana Sana Genta Kwa sababu Tabia yake ya ukweli ni ngumu kuiiga. Mfano mdogo tu nikifuatisha ushabiki maandazi wenu unaoshangilia Kila kitu bila kuhoji; Ni lini mkataba ukathibitishwa Kwa kutengenezewa jezi?...
Nimeanzisha Uzi huu Kwa ajili ya Watu very Intelligent kama Wewe Kuujadili cha Kushangaza nao Umevamiwa na Wapumbavu na Wendawazimu wengi tu kama huyo Uliyemjibu na Wengine waliochangia na Watakaochangia kama Wao.

Na niweke tu Wazi kwa Wasionijua ( Wasiojua ) kuwa Mimi GENTAMYCINE ni Shabiki Kindakindaki ( Lia Lia ) kabisa WA Simba SC ila nina Udhaifu Mmoja Mkubwa wa kutokuwa Mnafiki, Muongo, Mpumbavu na Kupenda Kujipendekeza ( Kujikomba ) kwa Mtu ( Watu )

Namaliza kwa Kusema Mikataba yote ya Simba SC na Yanga SC hii ya sijui Tsh Bilioni 26.1 na Tsh Bilioni 12 yote ni ya Kimagumashi ( Uongo ) mtupu na Binafsi kwa ninavyozijua hizi Klabu Kubwa Mbili na Uswahili uliopo ni kwamba tumedanganywa Mchana Kweupe tu.
 
Wenye akili ni wachache ila wajinga ni wengi sana hapa duniani.

"Fumbo mfumbie mjinga mwerevu ataling'amua"

Tayari waliopigwa na kitu kizito washajijua na kuanza kujitetea pesa haziwasaidii chochote isipokuwa wao wanataka burudani tu [emoji847]
Niliyategemea haya Mkuu.
 
Hao ndo mashabiki wa Tanzania. Kwamba shabiki alitegemea fedha ya klabu imnufaishe na yeye binafsi? Tangu mabaunsa waondolewe kwenye hivi vilabu mashabiki wamebaki kujifariji kwamba hawana shida na uchumi wa vilabu vyao maana hauwasaidii Bali wao wanachojali ni matokeo ya uwanjani. Hivi ni vipi unaweza kupata matokeo mazuri bila usajili mzuri?

Unafanyaje usajili mzuri bila kuwa na uchumi mzuri? Huo uchumi unajengwa na Nani kama siyo wewe shabiki au mwanachama wa timu husika?

Ukiwa hivyo unakuwa na tofauti gani na mwanachama wa Chama cha siasa ambaye anafurahia Ushindi wa Chama chake wakati hashiriki kupiga kampeni??
 
Product ya SAUT hii
Yenye Mchanganyiko wa Akili Kubwa ya Kuzaliwa ( Kurithi kutoka kwa Mababu, Mabibi na Wazazi wangu Wapendwa ) na ile ya Kuongezewa na 'Genius Lecturers' kutoka The Genius University of Tanzania ( SAUT Mwanza ) nilikopita 2006 - 2009 na Kuiva vyema.
 
Hela ndogo hiyo kwa makampuni ya kubet. We hujawahiliwa 1M kwenye kubet labda kwa siku 1

A) 5B =5000M kwa mwaka

5000M ÷365 =13.7M kwa siku moja
B) mikoa ya bara iko 26
13.6M÷26=523,000.

Kwamba mkoa mzima siku nzima waliwe 523,000 kwenye kubet kwa kampuni husika. Inawezekana sana

C)wilaya za bara zafika 100

13.6M÷100=136,000

Kila watu waliwe 136,000 jumla kwa siku nzima kwa kampuni husika

Kwa hiyo msihisi hiyo hela ni nyingi kihivyo.
 
Mtamtukana Sana Genta Kwa sababu Tabia yake ya ukweli ni ngumu kuiiga. Mfano mdogo tu nikifuatisha ushabiki maandazi wenu unaoshangilia Kila kitu bila kuhoji; Ni lini mkataba ukathibitishwa Kwa kutengenezewa jezi?...
Sijui niwaite wajinga mara ngapi ili mjielewe kuwa nyie kweli ni wajinga.

Unaposema mkataba wa Simba SC ni feki, tuwekeeni huo original tuuone, mna upeo mdogo ndio maana mnamshangilia mjinga mwenzenu.
 
Back
Top Bottom