Ushabiki tu lakini hakuna hoja yoyote. Wakati wa COVID-19, Ligi ya Botswana ilisimama March 2020 kwa msimu wa 2019/2020. Msimu wa 2020/2021 hakukuwa na ligi kabisa lakini Federation ya Botswana ikaichagua Galaxy Gwaneng kuwakilisha CAF Champions. Tukaja kukutana na Galax April 2021 yaani zaidi ya mwaka mmoja tangu ligi yao isimame. Je, kuna haja ya kukumbushana nini kilitukuta pale Lupaso?Sema kati ya hivyo vitu 4 kipi sio kweli? Twende kwa hoja sio vioja
Hoja kwamba wachezaji wao wameondoka haina msingi kwa sababu Sudan ni moja ya mataifa yaliyopiga hatua kisoka kwahiyo hata Wachezaji wa Ndani na wenyewe wapo vizuri. Na kwavile ligi yao ilisimama Mwezi April 2023 kabla ya usajili wa 2023/2024, ulipofika msimu wa usajili walishajianda ku-capitalize wachezaji wa ndani. Na El Merrikh ni kama Simba au Uto ya Sudan, kwahiyo Wachezaji wengi wa ndani wanatamani kuchezea hiyo Klabu ukiondoa wale wenye mahaba ya kuzaliwa na kujikuta wanaipenda Al Hilal