Leo natangaza rasmi kuacha kushabikia soka la Tanzania

Leo natangaza rasmi kuacha kushabikia soka la Tanzania

Chaliifrancisco

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2015
Posts
26,021
Reaction score
79,710
Leo hii tarehe 26/10/2021 mimi Chaliifrancisco nikiwa na akili timamu kabisa natangaza kusimama kufuatilia na kushabikia mpira wa hapa kwetu Tanzania. Kama nitakuja kushabikia tena sijui lakini itategemea na tathmini nitakazofanya mwenyewe nikiridhishwa nitaamua.

Sababu zilizofanya nifikie uamuzi huu ni kwanza kutokana na jinsi team zetu za hapa nyumbani zinavyoshindwa kufanya vizuri kimataifa kutokana na hujuma za baadhi ya watu (viongozi) mfano ni team ya Biashara Utd kushindwa kusafiri kwenda Tripoli kwaajili ya mechi ya marudiano katika kombe la Shirikisho.

Kumekuwa na tetesi kuwa viongozi walipokea rushwa ili wakwamishe team kwenda Libya. (Hata kama sio za kweli lakini kitendo cha kushindwa kupeleka team ni upuuzi usiovumilika kabisa).

Uongozi wa club walishajua watashiriki michuano hiyo tokea mwisho wa msimu na maandalizi yalitakiwa yawepo hata kwa kupitisha bakuli kama Yanga lakini wamezembea. Na kama ni kweli walivuta mlungula basi ni fedheha sana kwa soka letu. Hawa watu wafungiwe maisha na TAKUKURU wakamate wapige miaka 50 ndani.

Sababu nyingine ni team kutofanya vizuri kutokana na uzembe/kubweteka (complacency)

Mfano ni Simba msimu uliopita walibweteka sana na kuidhrau Kaizer Chiefs matokeo yake kila mtu anajua kilichotokea. Kiuhalisia kweli Simba alikuwa na nafasi nzuri zaidi ya kusonga mbele lakini complacency ndio tatizo.

Kitu hicho hicho kimejirudia tena msimu huu (weekend iliyopita). Haiingii akilini team ishinde ugenini goli 2 halafu kocha ashindwe ku manage mchezo wa marudiano nyumbani na team inafungwa 3 na kutolewa. Hii haikubaliki.

Kitu cha pili ni huu uamuzi wa club ya Simba kuamua kumtupiga virago kocha Didier Gomes. Hebu angalia CV (takwimu) za kocha huyu tokea ametua Msimbazi.
IMG-20211026-WA0014.jpg

Hivi ni wapi tutapata kocha mwenye uwezo kama huyu? Simba wametumia kigezo gani kuachana na huyu kocha? Kwa takwimu hizi ni ngumu kupata kocha ambae anaweza kufikia angalau robo tatu ya alichokifanya Da Rosa.

Mimi kutokana na habari hii ya kuondolewa Da Rosa ndio kumenifanya sasa nifikie maamuzi ya nilichokuwa nakifikiria cha kuachana na soka la Tanzania ambalo halina tija.

Yani ili uweze kuelewa soka la Tanzania lazima uwe na ukichaa fulani. Ukiwa mtu smart kama mimi hili soka la bongo halikufai.

Until then. I rest my case.
 
Nimesoma wote kabla ya kuweka comment...

Hizo habari za Biashara mi naona umeweka kama kisingizio tu...

Mwishoni maa uzi ukamwaga sumu zako za Simba...
Yes zote ni sababu za msingi kabisa zilizofanya niamue hivyo. Nimekuja kuona soka la bongo ni michosho tu ngoja mimi ni focus tu kwenye mpira wa mabeberu hamna namna.
 
Yes zote ni sababu za msingi kabisa zilizofanya niamue hivyo. Nimekuja kuona soka la bongo ni michosho tu ngoja mimi ni focus tu kwenye mpira wa mabeberu hamna namna.

Hata huko utapigwa na muhaho tu...

Ona mashabiki wa Barca, Madrid, Man U, Juve wanavyotia huruma sasa, utafikiri hizo timu hazikuwahi kuwa giants of Europe...

Kula yamini tu komaa na Simba hadi kieleweke, miaka michache ijayo itaeudi kuwa ya neema kama ilivyokuwa miaka ya kina Chama, Mafisango, Masatu na kurudi nyuma zaidi...
 
Hata huko utapigwa na muhaho tu...

Ona mashabiki wa Barca, Madrid, Man U, Juve wanavyotia huruma sasa utafikiri hizo timu hazikuwahi kuwa giants of Europe...
Bora huo wa huko sio wa kijinga kama huu wa kwetu hapa bongo. Angalau watu wanajielewa na hawafanyi makosa ya kujirudia rudia.
 
Naona unalaumu kocha Gomes kufukuzwa ,na umesema sababu za Simba Mara nyingi kutolewa ni kubweteka kama walivyofanya kwa kaizer wakatolewa na Sasa na Galaxy pia ni samething ,huoni kwamba hiyo sababu zinatosha kumfukuzisha kocha
 
Umeanza kupenda team ukubwani wewe, mimi Simba hata ishuke daraja sihami
Soma vizuri mkuu. Sijasema nimehama, nimesema "nimesimama kushabikia". Mimi sijaanza kushabikia Simba leo, lakini kwakweli kwa mambo ya hovyo haya sio lazima niendelee. Kwasasa acha nikae pembeni nitarudi nikijiridhisha kuwa sasa watu wanatumia akili.
 
Kocha anayekisia wacha afurushwe tu, kocha hataki kubadilika yaani kwasababu plan A ilimpa matokeo basi yeye anastick hapo hapo kwenye plan A ikiwa plan B inaonekana inafaida

Mfano pale Liver, Matip kaanza karibu kila game lakini angalia Klopp akambench na Man Utd, kamuanzisha Konate ambaye hata game tatu hajacheza tangu mwezi may!

Simba ni timu bora sana tukimpata kocha anayejuwa kutumia resources zilizopo, nakuhakikishia tu kuanzia kesho ushindi wa goli tatu unarejea.
 
Naona unalaumu kocha Gomes kufukuzwa ,na umesema sababu za Simba Mara nyingi kutolewa ni kubweteka kama walivyofanya kwa kaizer wakatolewa na Sasa na Galaxy pia ni samething ,huoni kwamba hiyo sababu zinatosha kumfukuzisha kocha
Ndio mkuu zinaweza kuwa sababu lakini mimi nakuhakikishia kuwa mfano last season kwa Kaizer tulitolewa kwasababu ya yule roporopo alieko Utopolo kwasasa na sio kocha. Yule alifanya mpaka wachezaji wakajua walishafika fainali wakati hawajacheza mechi.

Kwahiyo kimsingi mimi nalaumu aina ya uendeshaji wa hizi team zetu. Zina mifumo ya hovyo sana.
 
Gomez ameonewa na hamtapata coach bora kama gomez nakuambieni pale simba mmeweka siasa ila uyu jamaa anajua shida anapangiwa na wazee wanaojifanya kuijua simba ila mtahjuta
 
Kocha anayekisia wacha afurushwe tu, kocha hataki kubadilika yaani kwasababu plan A ilimpa matokeo basi yeye anastick hapo hapo kwenye plan A ikiwa plan B inaonekana inafaida

Mfano pale Liver, Matip kaanza karibu kila game lakini angalia Klopp akambench na Man Utd, kamuanzisha Konate ambaye hata game tatu hajacheza tangu mwezi may!

Simba ni timu bora sana tukimpata kocha anayejuwa kutumia resources zilizopo, nakuhakikishia tu kuanzia kesho ushindi wa goli tatu unarejea.
Mkuu Da Rosa ni kocha mzuri. Ni mambo madogo madogo tu yakurekebisha.

Unataka kuniambia kwa uliyoandika hapo Da Rosa ni kama Ole Gunnar?
 
Gomez ameonewa na hamtapata coach bora kama gomez nakuambieni pale simba mmeweka siasa ila uyu jamaa anajua shida anapangiwa na wazee wanaojifanya kuijua simba ila mtahjuta
Mbona kwa uchebe mliandika haya haya tu bdae akaja Sven Mlikaaa kimya

Kila zama na kitabu chake
 
Back
Top Bottom