Niwe wazi kabisa. Soka la bongo niliacha kulifuatilia siku nyingi zilizopita. Na sababu haswa ya kuachana nalo ni aina ya mpira tunaocheza. Vilabu vilivyopo ni vitatu tu. Simba, Yanga na Azam. Hao wengine sijui Ihefu, Mbeya kwanza, Mbeya City na nyingine za aina hiyo ni upuuzi mtupu.
Mpira unaochezwa uwanjani ni wa hovyo, hauna kitu choxhote cha ufundi, ni butuabutua tu.
Waamuzi nao ni eneo lingine ambalo linaangusha soka la bongo ambalo tayari ni bovu. Haswa linesman. Hawa hawajui wakati gani mchezaji anakuwa off side. Akiona beki kazidiwa mbio na mshabuliaji kawa mbele kwao wao ni off side hata kama alianza kukimbia akiwa on side.
Kwa kifupi sina muda wa kufatilia soka la bongo.