Hii picha ilikuwa ngumu pia ilinipotezea muda wangu sana katika kuuchimba ukweli wa pande zote mbili... nilitumiwa mpaka cheti cha ndoa cha mlalamikaji akiwa ameolewa na mwanaume mwingine. sikutaka kumhukumu mtu kwa kuwa naijua maana ya haki ya msingi ya mtuhumiwa na kwa kuwa mtuhumiwa alikuwa Rafiki Yangu nikamuhoji katika kuupata ukweli ni upi.
ni mahojiano yalioambatana na hasira, malalamiko, lakini mwisho wa siku nilimuelewa na kumwambia kile ambacho anatakiwa kufanya. lakini cha ajabu hata mimi rafiki yake akanichukia na hata pale nilipokuwa nikimtania alikuwa tofauti na mimi. Upande wa mlalamikaji nae alinipa vitu kibao ambavyo vilinithibitishia kuwa kuwa mlalamikaji alikuwa na haki. nilitumiwa mpaka mambo ambayo hayafai lakini mwisho wa siku nikabaki nimetulia kuangalia game na mnyukano. Kila siku upande wa mlalamikaji ulikuwa ukija na Ushahidi mzito lakini kile nilichokiongea na@USHIMEN bado kilikuwa ndio msimamo wangu. Licha ya mlalamikiwa kunichukia lakini bado nilimuona ana haki ingawa si kwa asilimia mia moja na bado nilikuwa nikimpenda kama dada. Hatimaye Majuzi nadhani amelitambua na ameendelea kuwa Dada Rafiki. Mengine yataendelea kuwa siri katika maisha Yangu.
TUKUBALIANE NA UKWELI NA TUANZE MOJA KATIKA HILI. HONGERA USHMEN KWA KUONGEA UKWELI.
MAKAPUKU
for
life