Leo nayatoa ya moyoni

Wanaume wa Dar mtatuzeesha kaka zenu wa mikoani jamani!? Hata hili nalo unataka tukushauri!
 
mi nasubiri vitu viwili muhimu...jina la huyo X fisadi na jina la current baaasi!
Hahaha daah, haya subiri story iishe though I wish majina ya wahusika yasitajwe,, inayemuhusu ujumbe utakuwa umeshafika. Kama walishamalizana ni vizuri kila mtu afanye yake ..ndo kuachana kiutu uzima huko
 
Hahaha daah, haya subiri story iishe though I wish majina ya wahusika yasitajwe,, inayemuhusu ujumbe utakuwa umeshafika. Kama walishamalizana ni vizuri kila mtu afanye yake ..ndo kuachana kiutu uzima huko
sasa kama walishamalizana si angeyasimulia huko aliko kwa mdomo badala ya kuyaleta huku halafu asiyamalize
 
Wanawake wa JF!!! kaka una moyo na bado tena umerudi kutafuta humu humu nahisi unataka kujitoa muhanga.
 
sasa kama walishamalizana si angeyasimulia huko aliko kwa mdomo badala ya kuyaleta huku halafu asiyamalize
Mmh umbea utaniua sasa khaaa. Me nilivyomuelewa ni kwamba anataka kuweka mambo clear, especially kwa baby wake mpya. Coz ni kama figisu figisu za huyo ex zinaweka huu uhusiano wake mpya matatani + baby wake mpya kuchafuliwa humu ndani( khaa bye mpendwa, ntakuja kusutwa mama mtu mzima hivi haipendezi, utadhani Nilikuwepo sasa mmh)
 
Ok....
Baada ya X kufanya yake wakati mimi sijui, ghafla nilianza kupata PM kadhaa kutoka kwa wadau humu jf wakiniuliza kulikoni.
Wakati huo pia nilipata msukosuko mkubwa na huyu mdada mpya huku akinitumia shutuma nyingi sana.
Hapo nilibaki kati na nikaamua kunyamaza na kukata mawasiliano kwa new girl na X.
Kwambaali nikaanza kushuhudia minyukano ya wawili hawa humu jf, new girl akiwa mzuri kwa hoja na X akiwa mtu wa kupopoa maneno ya hovyo.
Hapo nilijiweka pembeni zaidi ya sana huku nikiwa tazama kwambaaaali... na nikiendelea kuwapuuza kwasababu wote walikua wakishutumiana kupitia kwangu.
New girl aliamua kukata mawasiliano na mimi kabisa, huku X akizidi kupigana kufa na kupona kwamba mahusiano yake yamevunjwa na NG, hata nilipokua nikimueleza wazi kwamba simpendi tena jibulake lilikua ni kwamba kwakua nipo na NG.
Mwisho nae niliamua kupuuza.
Baada ya muda flani kupita huku nikishudia X akim quote NG humu jf kwa crushed comments... Ghafla nilipata msg kutoka kwa NG... huku akinishutumu kwa mambo mengi mabaya ambayo kwa hakika siku yafanya na sikuhusika.
Kumbe X alitengeneza picha chafu za NG kwa kushirikiana na X boy wa huyu NG. Na sijui waliweza pata mawasiliano wapi hata wakaanza kuwasiliana, kwakweli yule jamaa x boy wa NG wangu alimueleza X wangu mambo mengi sana ambayo ni past za NG.
Amahakika kweli kua uyaone.
Lengo lilikua ni kumchafua na hapo X Boy wa NG wangu pia akapata kushawishika kwamba mimi ndie nilie sababisha waka achana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…