Dr. Chapa Kiuno
JF-Expert Member
- Sep 11, 2009
- 443
- 18
Friday, October 09, 2009
Leo ndio ile siku iliyokuwa ikisubiriwa ambapo Marekani inatuma makombora yake angani kulipua sehemu ya mwezi katika utafiti wao wa kutafuta maji kwenye mwezi.
Leo oktoba 9 ndio siku ambayo Marekani inatuma makombora yake mawili angani kulipua sehemu ya mwezi katika utafiti wao wa kutafuta maji kwenye mwezi.
Kama tulivyowataarifu awali kwamba shirika la utafiti wa anga la Marekani (NASA) lilikuwa likijiandaa kuzindua mpango wake unaoitwa LCROSS (Lunar CRater Observing and Sensing Satellite) ambapo mwezi utapigwa mabomu kwa kutumia kombora linaloitwa Centaur ambalo linaenda spidi mara mbili ya spidi ya risasi.
Tukio hilo litafanyika leo, wenye darubini katika baadhi ya nchi ambazo zitakuwa usiku wakati huo wataweza kushuhudia kwa macho yao na wengine kama Tanzania ambako itakuwa mchana tutaweza kushuhudia Live kwenye luninga za tukio hilo.
Inatarajiwa kuwa saa nane na nusu mchana kwa saa za Bongo, kombora hilo litatua kwenye uso wa mwezi likiwa katika spidi ya maili 5,600 kwa saa na litasababisha kufukuliwa kwa kifusi chenye uzito wa tani 350 na kutengeneza shimo kubwa sana kwenye mwezi.
Mabomu hayo yatalipuliwa kwenye mhimili wa kusini wa mwezi ambako wanasayansi wanaamini mabilioni ya barafu zilizoganda yanapatikana mita kadhaa chini ya ardhi ya mwezi.
Chini ni Video jinsi mwezi utakavyopigwa na mabomu leo na jinsi itakavyokuwa kama ambavyo wanasayansi wa Marekani wanatarajia.
NASA watarusha Live tukio hilo kupitia tovuti yao. Tembelea Link hii mida ya mchana kushuhudia tukio hilo.
http://www.nasa.gov/multimedia/nasatv/index.html