Leo ndio nimegundua kuwa kulia ni tiba kubwa sana

Leo ndio nimegundua kuwa kulia ni tiba kubwa sana

Miss_Mariaah

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2022
Posts
2,176
Reaction score
4,979
Hatimaye Leo nimegundua kulia Ni therapy nzuri Sana nlipatwa Na kipindi kigumu kilichoniumiza Sana nkawa najitahidi kukabiliana nashindwa.

Nikaingia room nikaangua kilio🤣🤣Kile kama cha mtoto nikalia Sana then nikanyamaza baada ya dakika chache nikakaa Sawa nikajisikia vizuri.

Mnapopatwa na magum ukiona limekulemea lia tu msiache kulia ndugu zangu lieni tu ni tiba pia.

====

MAONI YA MWANASAIKOLOJIA NA MSHAURI WA MASUALA YA AFYA JAMII, JIWA HASSAN
Kimsingi kulia ni jambo linalofungamanishwa na HISIA. Na mara zote si LAZIMA iwe ni huzuni tu hata katika Furaha ya dhati huwa tunatokwa na machozi. Na hii utaiona Kwa wanyama wote kwani wao pia wana HISIA na matamanio ndiyo maana unaweza kumuona Tembo anatokwa machozi na anamuokoa MTOTO wake shimoni.

Kulia ni NAMNA Bora ya kupunguza shinikizo la HISIA hasi NDANI yetu pia kwani ni moja ya njia za kutokusanya majeraha ya HISIA. Hii husaidia kemikali za msongo kupunguzwa (stress chemicals) na zikaletwa zile za Furaha (endorphins). Hapa sasa mapigo ya moyo yatakuwa sawa na Ari ya kutenda inarejea.

Kutokwa machozi huleta u-sumaku wa HISIA endapo wapendanao wakikumbatiana Kwa Furaha ya dhati nadhani unaweza kuiona Kwa mama na MWANAYE.

Hivyo Kwa ujumla wacheni tuyaruhusu machozi kutoka. Usiikusanye HISIA NDANI YAKO. Kama ni huzuni achilia nishati hasi hii itoke na kama ni Furaha iruhusu nishati hii chanya itawale Lakini usikithirishe kwani lolote likizidi ni ishara ya changamoto za afya ya AKILI

Jina langu: Jiwa, Othman Hassan. (Mkurugenzi: THE BETTER YOU LTD) Mshauri Afya ya Jamii na Kujimudu
 
Hatimaye Leo nimegundua kulia Ni therapy nzuri Sana nlipatwa Na kipindi kigumu kilichoniumiza Sana nkawa najitahidi kukabiliana nashindwa ....nikaingia room nikaangua kilio🤣🤣Kile kama cha mtoto nikalia Sana then nikanyamaza baada ya dakika chache nikakaa Sawa nikajisikia vizurii....mnapopatwa Na magum ukiona limekulemea lia tu msiache kulia ndugu zangu lieni tuu Ni tiba pia
😂😂😂 Ukimaliza, jiqngalie kwa kioo na ujiulize kwanini unalia
 
Siku moja niko bar ,vikombe vingi sana.Naingia toi nakuta jamaa mmoja analia na mimi wacha niporomoshe kilio.Tukaanza kufarijiana yataisha tu,yote maisha .Tukafuta machozi vikombe vikaendelea.Mimi mpaka leo sijui alikuwa analilia nini na mimi sijui kilichokuwa kinaniliza ni nini?
Oiiii.
 
Hatimaye Leo nimegundua kulia Ni therapy nzuri Sana nlipatwa Na kipindi kigumu kilichoniumiza Sana nkawa najitahidi kukabiliana nashindwa ....nikaingia room nikaangua kilio🤣🤣Kile kama cha mtoto nikalia Sana then nikanyamaza baada ya dakika chache nikakaa Sawa nikajisikia vizurii....mnapopatwa Na magum ukiona limekulemea lia tu msiache kulia ndugu zangu lieni tuu Ni tiba pia
Ulilia kwa dakika ngapi ukapata nafuu?
 
Siku moja niko bar ,vikombe vingi sana.Naingia toi nakuta jamaa mmoja analia na mimi wacha niporomoshe kilio.Tukaanza kufarijiana yataisha tu,yote maisha .Tukafuta machozi vikombe vikaendelea.Mimi mpaka leo sijui alikuwa analilia nini na mimi sijui kilichokuwa kinaniliza ni nini?
Oiiii.
Mligeuka kua bendi ya Washirika watu njatanjata!
 
Back
Top Bottom