Leo ndio nimejua kwanini TANESCO wamegoma kushusha bei ya umeme hata baada ya Bwawa kuanza kazi mwakani

Leo ndio nimejua kwanini TANESCO wamegoma kushusha bei ya umeme hata baada ya Bwawa kuanza kazi mwakani

Exactly, na hiki ndicho ninachokisemamsiku zote! Malengo ya mradi yanakwepeshwa kwa makusudi! Kuna faida gani sisi tuumie hivi kujenga Mradi kwa mika kibao halafu faida ziende Uganda, Rwanda na Malawi?! Sisi tunafaida gani na huo mradi kama bei haishuki, viwanda havikui na ajira haziongezeki?!!!!!
Viwanda vinahitaji mtaji,Bei ya umeme ni factor ndogo,mtu hawezi anzisha kiwanda kisa tu Bei ya umeme ndogo
 
Bt kwa akili ya kawaida tu how comes 2600Megawatts ziongezeke then bei isishuke jmn,I wish angekuwepo chuma...yan watu huku umeme ushakuwa wa kuwashia taa tu hata kutumia pasi inaonekana ni anasa kwa sababu ya gharama kubwa ya umeme.
Kabisa, lengo la mradixlilikuwa kushusha bei ya umeme na kichagiza ukuaji wa viwanda ili vijana wapate ajira na kukuza uchumi. Leo hii hata kutumia heater kuchemshia maji ni anasa, umeme watu wanawashia taa tu, tena ya nje inawashwa moja tu.., vieanda viko hoi, umeme bei juu!! Sasa zinaingiaje Megawatt 2,100 mpya kabisa na bei isishuke?! How!???
 
Huo mradi wa kuongeza megawatt umejengwa bure?
Hizo gharama za ujenzi nani analipa? Si mwananchi? Sasa anepaswa kufaidika na uwekezaji wake ni nani kama si mwananchi?
Na kama gharama za kuzalisha umeme zinashuka, na umeme ni mwingi kuliko demand ya ndani ni kwanini bei isishuke?
 
Unalipaje wakati hata kodi hulipi
 
Viwanda vinahitaji mtaji,Bei ya umeme ni factor ndogo,mtu hawezi anzisha kiwanda kisa tu Bei ya umeme ndogo
Acha kujitoa akili, umeme (nishati) ni critical factor katika uzalishaji wa kisasa, ni kama yalivyo mafuta, bei ya hivi viwili vikishuka, impact yake kwenye sekta zote ni kubwa mno!
 
Hutaki kivipi?! Lengo la mradi wa Rifiji ulikuwa ni kuzalisha umeme mwingi wa bei nafuu ili kuwapa wananchi unafuu wa maisha na kuchagiza ukuaji wa viwanda na unazalisha kwa ajili ya kutoa ajira kwa vijana na kukuza uchumi. Sasa ni kwanini leo hii wantuhujumu kwa makusudi, Megawatt 3700 zinaingizwaje kwenye gridi na bado umeme usishuke , how? Hapo ni kwamba utauzwa na pesa kuingia mfukoni huku tukikamulowa tozo za miamala na kodi za majengo kuulipa mkopo wa trillion 10 tuliokopa kujenga bwawa.., inaumiza sana.
Nakupata vizuri..yaani Kuna plan inapigwa ya kupiga.
 
Acha kujitoa akili, umeme (nishati) ni critical factor katika uzalishaji wa kisasa, ni kama yalivyo mafuta, bei ya hivi viwili vikishuka, impact yake kwenye sekta zote ni kubwa mno!
Mtu mwenye mtaji ambaye hakuwa na nia ya kuanzisha kiwanda, hawezi anzisha kiwanda kisa umeme umeshuka bei
 
"can’t imagine huyo mama abaki hapo hadi 2030, kweli?!! Tanganyika Tutakuwa na hali gani sisi, si tutakuwa tunatembea tunaongea wenyewe kama wehu?!"

UNAONGELEA ABAKI HADI 2030 WAKATI WAKULUNGWA WANATAKA KUMCHOMOA KABLA MWAKA HUU HAUJAISHA😂😂😂😂🤣🤣
INSHORT WATANZANIA TUMEPIGWA.
 
Tangu Maharage pale TANESCO alipotoa tamko lisilo na mantiki na linalo-defy all logical reasoning, kwamba eti hata baada ya Megawatt 2100 kuanza kuzalishwa kwenye bwawa la Nyerere na kuingizwa kwenye Gridi bado eti umeme hautashuka bei, nimekuwa nikiwaza sana nisielewe hii itawezekana vipi?!

Ni kwamba Law ya demand vs Supply inagoma kabisa!! Kwamba matumizi yetu hivi sasa ni Megawatt 1,600, na ndizo zinazalishwa kwa sasa, halafu ghafla uingize Megawatt 3,700 kwenye gridi, huo umeme wote atautumia nani kwa ghafla hivyo hadi uishe?

Tulitegemea kwa kuwa umeme hauwezi kutunzwa kwenye betri, kwamba Tanesco washishe bei ili hadi vijijini wapikie majiko ya umeme, kiasi umeme huo sasa utumike wote bila kupotea, vinginevyo itabidi tufungulie maji bwawani yamwagike bire bila kuzalisha umeme.

Sasa leo ndio nimejua mchezo wanaotaka kufanya, ni mwamba hizo Megawatt 2,100 za Bwawa la Nyerere tutazisikia kwenye bomba tu, maana zitaingizwa kwenye gridi ya taifa na kuwa offloaded kwenda Zambia, Malawi, Uganda, Kenya ,Zanzibar, Burundi, Rwanda, Msumbiji, na hata sentano mbuni hatutaiona ya mauzo ya umeme. How? Kwanini nasema hivi?

1.) Umeme huo hautaonekana kwamba umetoka Tanesco, bali kuna dogo mmoja inadaiwa ni mtoto wa mama yetu, yeye kaongozana eti na maafisa wa Wizara ya Nishati ili azalishe umeme wa Solar na kuiuzia Uganda , [emoji23][emoji23][emoji23], kwamba umeme utoke Rufiji, mseme ni umeme jua wa huyo dogo? Halafu malipo yote alipwe yeye?!! [emoji23][emoji23][emoji23] , ujamja wa kizani sana huu...

2.) Inadaiwa January Makamba anakazana sana kuunganisha gridi ya Tanzania na Gridi za Rwanda kupitia Rusumo, na anafanya mikutano na nchi nyingi zinazotuzunguza hasa malawi, Zambia na wengine eti tuunganishe gridi yetu kwa pamoja ili tuuziane umeme panapokuwa na upungufu. Shida hapa ni kwamba umeme utatoka Rufiji halafu watasema ni umeme wa gesi, hivyo malipo yataenda kwa wenye gesi yao.., sisi tutabaki kulipa mkopo wa Trillion 10 zilizotumika kujenga hiko bwawa, kwa tozo za miamala na kodi za majengo za kwenye umeme zilizopoandishwa.

Hivi mtu mwenye akili timamu unakubali vipi kuambiwa kwamba Megawatt 2,100 ziingizwe kwenye gridi na bado zote zitumike ziishe bila kushusha bei?!!!

We are finished!! Tumekwisha...

View attachment 2715874

I can’t imagine huyo mama abaki hapo hadi 2030, kweli?!! Tanganyika Tutakuwa na hali gani sisi, si tutakuwa tunatembea tunaongea wenyewe kama wehu?!
Hata haiwezi kuwa hivo!

BWN MAHARAGE CHANDE anazo hoja lakini aliongea as if sisi wote tunafanya kazi TANESCO na tunajua hali ilivyo!

Ukweli ni kwamba Mradi ukikamilika kutaisaidia TANESCO kuwa na Stable supply ya Ndani ns Ziada Nje lakini watakuwa na Ombwe la Uwekezaji kwenye Miundombinu ya usambazaji umeme kwa wateja ambao imechakaa sana!

Pili ni Kwamba Deni lililojenga Bwawa ni kubwa na hivo ni Afya kwa Serikali kulilipa mapema ili tuweze kupata umafuu wa Finance kwenye maeneo mengine...

Tatu ni kwamba TANESCO inaendeshwa kwa Ruzuku...baada ya Mradi itabidi Shirika lijipange kujiendesha na kuipstia Serikali Gawio Nono!

Ili hayo yawezekane inabidi Tarrifs zibaki hizi hizi kwa miaka si chini ya Mitatu/Mitano kisha ishuke taratibu mpk kuwa competitive and attractive!

Halafu
TANESCO wamerekebisha Sheria na kuruhusu Uwekezaji na uzalishaji wa Umeme na kuuzia TANESCO licha ya Ongezeko linalotegemewa...

Anzaia hapo...
Tafuta fursa wewe binafsi kuanzia hapo...hayo mengine ni Majungu tu!
 
Mtu mwenye mtaji ambaye hakuwa na nia ya kuanzisha kiwanda, hawezi anzisha kiwanda kisa umeme umeshuka bei
Nishati ya umeme ni critical driving factor ya viwanda, hilo ni dhahiri, au mashine viwandani zinaendeshwa kwa mkaa?!
 
Hutaki kivipi?! Lengo la mradi wa Rifiji ulikuwa ni kuzalisha umeme mwingi wa bei nafuu ili kuwapa wananchi unafuu wa maisha na kuchagiza ukuaji wa viwanda na unazalisha kwa ajili ya kutoa ajira kwa vijana na kukuza uchumi. Sasa ni kwanini leo hii wantuhujumu kwa makusudi, Megawatt 3700 zinaingizwaje kwenye gridi na bado umeme usishuke , how? Hapo ni kwamba utauzwa na pesa kuingia mfukoni huku tukikamulowa tozo za miamala na kodi za majengo kuulipa mkopo wa trillion 10 tuliokopa kujenga bwawa.., inaumiza sana.
Hataree
 
Hata haiwezi kuwa hivo!

BWN MAHARAGE CHANDE anazo hoja lakini aliongea as if sisi wote tunafanya kazi TANESCO na tunajua hali ilivyo!

Ukweli ni kwamba Mradi ukikamilika kutaisaidia TANESCO kuwa na Stable supply ya Ndani ns Ziada Nje lakini watakuwa na Ombwe la Uwekezaji kwenye Miundombinu ya usambazaji umeme kwa wateja ambao imechakaa sana!

Pili ni Kwamba Deni lililojenga Bwawa ni kubwa na hivo ni Afya kwa Serikali kulilipa mapema ili tuweze kupata umafuu wa Finance kwenye maeneo mengine...

Tatu ni kwamba TANESCO inaendeshwa kwa Ruzuku...baada ya Mradi itabidi Shirika lijipange kujiendesha na kuipstia Serikali Gawio Nono!

Ili hayo yawezekane inabidi Tarrifs zibaki hizi hizi kwa miaka si chini ya Mitatu/Mitano kisha ishuke taratibu mpk kuwa competitive and attractive!

Halafu
TANESCO wamerekebisha Sheria na kuruhusu Uwekezaji na uzalishaji wa Umeme na kuuzia TANESCO licha ya Ongezeko linalotegemewa...

Anzaia hapo...
Tafuta fursa wewe binafsi kuanzia hapo...hayo mengine ni Majungu tu!
Ombwe la uwekezaji kwenye miundombinu kwa mantiki ipi? Hapa tunazungumzia kwa wateja ambao tayari wameshaunganishwa na gridi, kama umeme umezalishwa mwingi, utaoelekwa wapi wote kama hakuna incentive ya kuwafanya utumike wote na kuisha, maana huwezi kuhifadhi umeme kwenye battery, lazima utumike wote nauishe, na ziada inayobaki iuzwe nje ili kuinua shirika loweza kusimama imara.

Hilo deni unalozungumiza hata sasa linalipwa kwa kodi lukuki zilizopo, inaleta mantiki zaidi kwa umeme ukiozalisjwa kwa gharama nafuu na uliomwingi kuliko mahitaji ya ndani, Ile excess ikauzwa kwa faida nje ya nchi, ila ule unaozwa ndani ukashuka bei accordingly ambapo kupitia ukuaji wa viwanda na kuongezeka kwa ajira serikali ikakusanya kodi kubwa zaidi na kusaidia kulipa mikopo yetu kwa ujumla, na hata ruzuku isihitajike tena, kwa i tayari kuna mapato yatokanayo na uuzaji umeme nje ya nchi.

Kuuza ziada nje ya nchi hakuzuii kushusha umeme ndani ya nchi!

Kibaya zaidi, umeme utakaouzwa nje ya nchi kuna watotocwa vigogo wanaunda vikampuni ili wapokee hizo fedha za mauzo.., mfano huyo wa solar, umeme utoke Rufiji mseme ni wa Solar zake
 
Haijalishi, msisahau na Ahadi alizowapea Waarabu kule Dubai, wa kuwagawia Tanesco baada ya kudumbukiza matrillioni ya Fedha za watoa Jasho Tanzania .

Hatahivyo msiwatafutie pahali pa kutokea, hakuna cha Law of Supply and Demand wala nini...ni Ufisadi tu.

Wanachokifanya ni kujisapply wenyewe.
 
Hili bando nimetoa wapi? Si nimenunua, na kodi si wamekata? Au kodi unazungumzia?
Kwa hiyo iyo hela yako ndo inaenda kuzalisha umeme? Barabara zinajengewa hela ipi? Dawa hospitalini zinanunuliwa kwa hela ipi? Mishahara ya watumishi wa Umma inalipiwa hela ipi?

Icho ki 150 za vocha ndo kifanye upunguziwe umeme? Chizi kabisa wewe
 
Back
Top Bottom