Leo ndio nimejua kwanini TANESCO wamegoma kushusha bei ya umeme hata baada ya Bwawa kuanza kazi mwakani

Hii mijizi ukiona vile mama alivyoirejesha jpm baada ya kuwatema ndio unashindwa hata kuamini kama kuondoka magufuli ni mapenzi ya mungu. Wanajipanga kuiteka nyara nchi.
 
Hoja hapa watu binagsi wanauza umeme gani nje. Kuna hila za watu binafsi kuuza umeme wa tanesco huku wakijifanya wamezalisha wao.
Jiulize kwa nini kuwe na watu binafsi kutafuta masoko kuuza umeme nje sasa na sio kabla ya kuwepo umeme wa bwawa la nyerere? Tunachotaka ni kushuka bei ya umeme utakopoanza kupatikana kwa gharama ya chini na sio kuuzwa nje na watu binafsi kujidai ni umeme wanazalisha wao.
Januari na maharage lazima kudhibitiwe na umma maana mama amewaweka pale kwa ajili ya upigaji tu. Umma wa wananchi tusikubali.
 
Bwawa kagharamia nani huo ujenzi wake? Maana unaongea as if hilo bwawa kuna mtu huko katoa zawadi pesa yake mfukoni kajenga, na sio wananchi
Uchumi hauendi hivyo, pesa tayari ni za serikali bila kujali ni mkopo au Kodi au Mapato yasiyo Kodi. Sasa kama serikali imeingia gharama kujenga say trillion 6 unadhani italipaje marejesho ya mkopo plus gharama za kuendesha ikishusha bei siku ya kwanza?

Ndio maana nikasema Tanesco ni monopoly so mjadala wake hauwezi husisha demand and supply kwenye kuamua bei.

CCM wanapenda maneno ya kutuhadaa tu ikija utekelezaji wanaturuka. Hata Hilo daraja la busisi likiisha usishangae watu wakatozwa 200 kuvuka hapo.
 
Kwa kushusha gharama za umeme na kuongeza uwekezaji na uzalishaji wa bidhaa Viwandani zenye ushindani Wa soko la ndani na nje, pamoja kuongeza ajira na kukuza uchumi, haitawezesha kulipa deni?
 
Weka evidence mezani ya kuwa umeme watu wanaiba sijui kwenye ndoo wanaenda kuuza nje otherwise ni hadaa.
Huwezi kupunguza bei tutaendelea kujenga taifa la wavivu kwa style hio kama kila kitu kigaiwe bure bure na tutakuwa tunajenga uchumi na huku tunaongeza matobo kwenye uchumi huo huo kwa wakati huo huo ,tukifanya hivyo itakuwa stori ya maendeleo na kukuza uchumi kwetu sawa na pakacha kulijaza maji yanayoingia yote yanatoka na umasikini unaendelea kutaradadi.
 
Umeme wa maji ni mwingi na ni nafuu, objectives za mradi ilkuwa ni kutumia rasilimali ya mto Rufiji kuzalisha umeme wa bei nafuu utakaoweza kuchagiza uzalishaji wenye tija viwandani nankuongeza viwanda vitakavyozalisha bidhaa zenye ushindani katika masoko ya ndani na ya nje, kuzalisha ajira na kukuza uchumi, hayo yataletq mapatocmengi serikalini na kugharamia mikopo yote, kwanini mnapindisha malengo kwa maslahi ya Akina Abduli na kiparangoto?
 

Hapa ndipo pesa inapopelekwa
 
Hivi vipuli vya mitambo ya bwawa la Mwalimu Nyerere vinapatikana wapi?
 
Moja ya sababu kubwa ya kujenga mradi huo ni umeme kushuka bei. Ndicho alichotuambia Hayati Magufuli.
Faida za kushusha bei viwanda/migodi vitapunguza gharama za uzalishaji na kuvutia uwekezaji. Impact yake tutaongeza mapato itakuwa rahisi kulipa madeni mnayoyasema, maana tutakuwa na fedha zaidi, aidha tutalinda mazingira, maana matumizi ya mkaa na kuni vitapungua. Tutapunguza gharama za maisha kutokana na kupunguza kwa gharama za uzalishaji viwandani.
Kushusha bei ya umeme ndicho walichotarajia watanzania wengi na ni kama ilisaidia kushawishi watu wengi kuunga mkono huo mradi.
 
Ndio kwa kuwa ni mwingi na ni nafuu kuzalisha na pia viwanda vitakuwa na uhakika wa umeme basi tutajihakikishia profit na ndio tunataka tutengeneze surplus ya kufanya mambo mengine ya kukuza uchumi bei haishushwi acha pesa na surplus itengenezwe tupunguze kodi maeneo mengine ili sekta mbalimbali mtambuka za kiuchumi zikue zaidi na kuchangia zaidi pato la taifa. Maana adha ya viwanda kuwa na njia nyingine mbadala sijui makaa ya mawe au magenereta itakuwa hayahitajiki tena kama njia mbadala kwa kuwa watapata nishati ya uhakika na watalipia na pia watajipunguzia gharama za ziada za kununua mafuta au makaa ya mawe kwa ajili ya uendeshaji wa viwanda kwa kuwa na uhakika wa umeme mwaka mzima.
 
Gharama za viwandani zitapungua kwa kuwa watakua na uhakika wa umeme bila kuhitaji installation ya mitambo ya ziada kuzalisha umeme bei watalipa hii hii tu. Lengo kuu la mradi ni kuhakikisha nchi inajitosheleza ktk nishati ya umeme kuepusha mgao wa umeme hili ndio kuu kabisa kukiwa na mgao uzalishaji mali unaathirika sana na pato la taifa linayumba kwa kipindi hicho.
 
Sasa unasema ivyo na unaguvu ,Sasa sababu Alie lianzisha Alisha kufa na mmekuja na ya maharege
 
Ulichoongea kwakweli kinakosa mtiririko wa kimantiki, sikatai kwamba umejibu, ila ni kama mbwa anabweka tu, hata sielewi hoja yako yabkuoinga kushuka umeme ni ipi, mara majenereta, mara makaa ya mawe, hata sielewi. Ngoja watakaolewa wanisaidie
 
Niliwaambia ccm tukingoja hadi 2025 bado tutavuna mabua, hawa dawa yao ni kuwaondoa kwa nguvu ya umma,wananchi wote tukiingia barabara watatoka tu hii nchi sio mali yao.
Duuu yaani watu waache kula Raha ikulu watoke kisa wewe umeingia barabarani kama ni hivyo wangekuwa washatoka maana Kila siku tuko barabarani na magari
 
Umeme utoke Rufiji halafu mseme ni wa Rostam?

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…