Leo ndio nimejua kwanini wanawake wanajiingiza katika tabia za udangaji

Leo ndio nimejua kwanini wanawake wanajiingiza katika tabia za udangaji

Course mpya na wewe ulisema umemaliza chuo una miaka miwili nyumbani na ulimalizia Mzumbe..hahaha

Jamaa acha ujuaji basi usitake kujua kila kitu Kama wewe unanifahamu weka hapa taarifa zangu… mtu hunijui nimeleta mwenyewe uzi wangu unakuja kunibeza sijui chai

Haya wewe andika story yako hapa maana tunafahamiana
 
Hapa nilipo nina majonzi, roho imeniuma sana kwa kuzaliwa kwenye familia maskini

Ipo hivi mimi kwetu ndio wa mwisho msichana peke yangu kati ya watoto 6.. Mzee wangu alitangulia mbele za haki hivyo tumebaki na mama tu.. hao ndugu zangu wote hawana maisha ya kueleweka isipokuwa mmoja tu angalau yeye ameajiliwa serikalini ndio kidogo anaibeba familia, yeye ameshaoa ana familia yake

Mimi nimeshahitimu chuo nina kama Miaka miwili nyumbani.. nimepata sehemu ya kujishikiza wananilipa 250000.. Kwetu ni bunju nafanyia kazi magomeni kila siku natumia 5000 yaani 3000 nauli 2000 nakula mchana hapo Ndio najibana mno..

Sasa kwasasa Hivi nyumbani Hakuna mtu nipo peke yangu mama ameenda kijijini kwao bibi anaumwa, mama yangu hana kazi ile ya kumtegemea anauza chupa za maji hivyo siwezi kumsumbua kwa chochote, amesafiri hajaniachia hata shilingi 100.. Hakuna chakula ndani Hakuna chochote, nachofanya nikitoka kazini nashukia kwa brother nakuta wamepika nakula naondoka

Leo nimeumia sana sijaenda kazini Nina siku 2 sina nauli hela niliokuwa nayo akiba imeisha nimemuomba bro kasema yeye hana hela hawezi kuwa anatoa hela mara mbili mbili kwa familia yake na kwangu, Kama niliweza kutafuta kazi basi nijitegemee nauli nikitaka kula nije nyumbani,, nikamuuliza sasa nitatoa wapi na Ndio naanza kazi akanijibu nitajua mwenyewe

Hiyo kauli imeniuma yaani anamaana gani kusema nipambane nitafute nauli yaani naitafutia wapi ..

Leo nimeacha kuwa judge Watu na maisha wanayoishi Kama ndugu yangu wa damu ananiambia maneno haya hao wa nnje watanijibu vipi

Ni hayo tu wakuu
Pole sana,ila kaka yako alitaka uzinduke usingizini,hiyo ajira ya 250k
kwa mwezi ni kizuizi cha mafanikio yako. Pia naye usikute anayapitia hayo hayo unayoyapitia ila anapambana kiume naye apate nauli hadi mwisho wa mwezi.

Una uwezo wa kulima chinese spinachi
kwenye mifuko ya simenti au mchicha hapo hapo nyumbani au kulima maua ya kwenye makopo
na ukaipata hiyo 250k bila kulipa nauli ya kwenda kazini na maisha yakasonga.

Kudanga na ukalipwa ni kipaji,Unaweza kudanga na ukadhurumiwa na hakuna pa kushtaki,ungewapata wadangaji
wakakueleza wanayoyapitia,utajua hakuna njia ya kutoka kimaisha kirahisi.
Kila aliyefanikiwa kimaisha,ana historia yake.Wewe shukuru Mungu angalau umesoma
siku moja Mungu atakujalia upate kipato kizuri,si lazima kuajiriwa .
 
Back
Top Bottom