Leo ndiyo leo: Messi, Ronaldo vitani kupambania mataifa yao

Leo ndiyo leo: Messi, Ronaldo vitani kupambania mataifa yao

upload_2017-10-10_18-50-10.png
upload_2017-10-10_18-50-10.png
Mungu ibariki Albiceleste. Hope watafanya wonders kama watapita.



1 King Messi
2 mchawi Dybala
3 Kun Aguero
4 Higuain
5 De Maria
6 lcardi
7 Mascherano
8 Maidana
9 Nicolas Gaitan
10 Javier Pastore
11 Fernando Gago
12 Marcos Rojo.
13 emanuel Mammana
14 angel correa
15 ezequiel lavezi n.k
16 Jonathan Maidana

Wana majembe yakufa m2. Mungu ibariki Argentina wapite na wabebe ndoo.
 
Ni siku muhimu katika maisha yao ya kisoka. Siku ya kuzipambania timu zao za taifa ziweze kufuzu Kombe la Dunia la mwakani huko Urusi. Ni siku za wao kuudhihirishia ulimwengu wa soka kuwa wanaweza kuwa tegemeo katika klabu zao na timu zao za taifa.

Nchini Ecuador, Lionel Messi atawaongoza Argentina katika pambano la 'must win' kati yao na wenyeji Ecuador. Messi ataiongoza Argentina kusaka ushindi wa kufa au kupona ili waweze kufuzu fainali za kombe la dunia. Ushindi dhidi ya Ecuador utawafikisha Argentina kwenye alama 28 na kuweza kuwapiku wengine.

Huko Amerika ya Kusini, washindi wanne wa mwanzo hufuzu moja kwa moja. Wa tano hucheza na mshindi wa Oceania ambaye ni New Zealand ili mmojawapo afuzu. Kwasasa, Argentina inakamata nafasi ya sita. Tayari vinara Brazil wameshafuzu na leo watashuka uwanjani kupambana na Chile inayosaka kufuzu. Macho na masikio ya kocha Jorge Sampaoli na Waargentina wote ni kwa Messi.

Nchini Ureno, Christiano Ronaldo ataiongoza Ureno, mabingwa wa Ulaya, katika mechi ya kufa au kupona dhidi ya Uswisi. Hadi sasa, Uswisi inaongoza kundi la Ureno ikiwa na alama 27 na Ureno iko nafasi ya pili ikiwa na alama 24. Kwakuwa ina faida ya magoli ya kufunga, Ureno inahitaji ushindi wowote ili ifuzu. Uswisi inahitaji ushindi au sare ili ifuzu.

Hapa Ronaldo, pale Messi. Wote ni Manahodha na wachezaji bora wa soka kwasasa duniani. Wote wapo hatarini kufuzu kombe la dunia. Wote wanacheza mechi za leo wakiwa wanategemewa kuonyesha umahiri na ubora wao. Ureno watateremka dimbani saa 3:45 usiku huku Argentina wakicheza saa 8:30 usiku.

Katika ubora wako mzee PETRO. big up kiongozi

Vivaa Argentina
Vivaa King
 
Hapo ndipo utagundus America hawana utani linapokuja suala la soka.

Inauma kuikosa Argentina kwenye michuano kama hiyo,Upande wa Ureno namiss vipaji vyao miaka 12 kurudi nyuma
 
King Leo Messi lazima afanye kweli leo...

Kila la kheri uswisi Granit Xhaka we can do this...
 
  • Thanks
Reactions: PNC
View attachment 606299 View attachment 606300 Mungu ibariki Albiceleste. Hope watafanya wonders kama watapita.



1 King Messi
2 mchawi Dybala
3 Kun Aguero
4 Higuain
5 De Maria
6 lcardi
7 Mascherano
8 Maidana
9 Nicolas Gaitan
10 Javier Pastore
11 Fernando Gago
12 Marcos Rojo.
13 emanuel Mammana
14 angel correa
15 ezequiel lavezi n.k
16 Jonathan Maidana

Wana majembe yakufa m2. Mungu ibariki Argentina wapite na wabebe ndoo.

Maajabu hayaishi duniani timu ina King na inampaka mchawi lakini wanakaribia kukata roho
 
Back
Top Bottom