kiatu kipya
JF-Expert Member
- Dec 4, 2016
- 3,269
- 1,977
Kwani Argentina ni nani kwenye world cupWorld Cup without ARGENTINA ni sawa sawa na ndondo cup kama hujui.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwani Argentina ni nani kwenye world cupWorld Cup without ARGENTINA ni sawa sawa na ndondo cup kama hujui.
Ni siku muhimu katika maisha yao ya kisoka. Siku ya kuzipambania timu zao za taifa ziweze kufuzu Kombe la Dunia la mwakani huko Urusi. Ni siku za wao kuudhihirishia ulimwengu wa soka kuwa wanaweza kuwa tegemeo katika klabu zao na timu zao za taifa.
Nchini Ecuador, Lionel Messi atawaongoza Argentina katika pambano la 'must win' kati yao na wenyeji Ecuador. Messi ataiongoza Argentina kusaka ushindi wa kufa au kupona ili waweze kufuzu fainali za kombe la dunia. Ushindi dhidi ya Ecuador utawafikisha Argentina kwenye alama 28 na kuweza kuwapiku wengine.
Huko Amerika ya Kusini, washindi wanne wa mwanzo hufuzu moja kwa moja. Wa tano hucheza na mshindi wa Oceania ambaye ni New Zealand ili mmojawapo afuzu. Kwasasa, Argentina inakamata nafasi ya sita. Tayari vinara Brazil wameshafuzu na leo watashuka uwanjani kupambana na Chile inayosaka kufuzu. Macho na masikio ya kocha Jorge Sampaoli na Waargentina wote ni kwa Messi.
Nchini Ureno, Christiano Ronaldo ataiongoza Ureno, mabingwa wa Ulaya, katika mechi ya kufa au kupona dhidi ya Uswisi. Hadi sasa, Uswisi inaongoza kundi la Ureno ikiwa na alama 27 na Ureno iko nafasi ya pili ikiwa na alama 24. Kwakuwa ina faida ya magoli ya kufunga, Ureno inahitaji ushindi wowote ili ifuzu. Uswisi inahitaji ushindi au sare ili ifuzu.
Hapa Ronaldo, pale Messi. Wote ni Manahodha na wachezaji bora wa soka kwasasa duniani. Wote wapo hatarini kufuzu kombe la dunia. Wote wanacheza mechi za leo wakiwa wanategemewa kuonyesha umahiri na ubora wao. Ureno watateremka dimbani saa 3:45 usiku huku Argentina wakicheza saa 8:30 usiku.
Uruguay tena?My prediction both teams (Ureno na Uruguay) will win tonight.
Ya timu ( mtu) kutakiwa ashinde mechi ( kesi) ndo mambo yakae sawa and not otherwiseHali ipi mkuu?
Kufa au kupona!Ya timu ( mtu) kutakiwa ashinde mechi ( kesi) ndo mambo yakae sawa and not otherwise
Kombe la Dunia bila Messi ni sawa na Msondo bila Ngurumo
Hapo ndipo utagundus America hawana utani linapokuja suala la soka.
Inauma kuikosa Argentina kwenye michuano kama hiyo,Upande wa Ureno namiss vipaji vyao miaka 12 kurudi nyuma
Mnaanzisha Uzi Ila Update Sifuri
View attachment 606299 View attachment 606300 Mungu ibariki Albiceleste. Hope watafanya wonders kama watapita.
1 King Messi
2 mchawi Dybala
3 Kun Aguero
4 Higuain
5 De Maria
6 lcardi
7 Mascherano
8 Maidana
9 Nicolas Gaitan
10 Javier Pastore
11 Fernando Gago
12 Marcos Rojo.
13 emanuel Mammana
14 angel correa
15 ezequiel lavezi n.k
16 Jonathan Maidana
Wana majembe yakufa m2. Mungu ibariki Argentina wapite na wabebe ndoo.
Hiyo ya akina ariel Ortega, Batistuta, Lopez...hatari hiyo.Kuna Argentina iliyokuwa bora kama ya mwaka 2002 South korea na Japan? Hawana maajabu yoyote
inauma sana mkuu ni sawa na sikukuu iangukie weekendInauma sawa kombe la dunia bila Messi na CR7