KimbakaeKO
Member
- Jun 23, 2024
- 39
- 45
Hu
Huyu ndio Mimi, ila huyu hajajielewa. Mimi najielewa na ninajifahamu, sihitaji ushauri hivi nilivyonajipenda, na niendelee milele.Mara nyingi nimekuwa nalaumiwa sana na mabinti ninaokuwa nao kwenye mahusiano kuwa sipendeki,kwa madai kadhaa ikiwemo kuwa sijali na au sionyeshi kama napenda kweli ile upendo wa kuonekana, japokuwa mara zote huwa najitetea kwamba mimi mahaba ya kinjiwa njiwa sijabarikiwa ndo maana hata njia yangu ya kuwapata sio ile ya tongoza tongoza nyingi, shawishi shawishi kadhaa etc.
Ni nakupenda nafatilia fatilia kidogo na tuvishawishi tudogo sana tu basi na huwa situmii rasimali pesa au muda na siku nyingi huku nikiambiwa hapana zaidi ya mara tatu naamini ni hapana kweli naachana nae, sasa kumbe wao ni tofauti wakiona nimepoa wanakuja wenyewe kwa gia zao na automatical mahusiano yanaanzia hapo.
Sasa kwenye mahusano yenyewe tudumu tusidumu sio jukumu langu tena, apate mimba asiwepate ni sawa tu tukianza mahusiano nitafanya hivi na vile kama wapenzi kweli kweli ila siku nikiambiwa ishu za penzi kuisha huwa hata siumii na tunaishia hapo kweli kweli japo sijawahi kuwa na binti wa watu kwa muda mfupi ni miaka kama miwili mitatu ndo penzi linrudi lilipotoka na linaisha bila ugomvi, mara zote naambiwa mimi ndo sieleweki, sina malengo yoyote kwenye mahusiano.
Nilifunga ndoa kabisa na binti wa watu japokuwa ndoa ilikuwa na taabu kadhaa ikiwemo feminist ila siku ananiambia kuwa anaondoka nilimpa jibu moja tu sawa nenda na akaenda kweli hadi leo ni mwaka.
Sasa wadau siwezi kuwa na tatizo la saikorojia kweli? Au sijapata mwanamke ninayempenda kwa dhati, maana nahisi kufanya ukatiri sana kwenye haya mambo. Nina watoto 5 wote mama tofauti.