Leo ngoja nivisanue hivi vitoto va Gen Z

Vina wakati mgumu Sana, baba na mama zao ni machawa pro max kutwa wanaimba na kuabudu wenzao mitandao I. Unategemea vitoto vitakuaje
Viliachiwa vijilee vyenyewe masikini.
 
Wewe unataka kushindana na wazazi wako, unahisi utaweza kushinda?
 
😄😄Mnajificha kwenye kivuli Cha mtu mzima hakosei mkuu, alafu sio wote Sasa hata kwa Gen z inatakiwa useme baadhi Yao sio wote
Nisamehe Kama nakosea kujibizana nawew bamkubwa😄
 
Mkubwa ni mkubwa tu kuna hoja atakubana unashindwa kupumua utaomba poo mwenyewe.
Sawa mkuu mimi sikupingi, wewe unashauri Nini sasa ili Hawa Gen z warudi kwenye njia ya watangulizi wao akina ninyi hapo
 
Sawa mkuu mimi sikupingi, wewe unashauri Nini sasa ili Hawa Gen z warudi kwenye njia ya watangulizi wao akina ninyi hapo
Hapa nimevisema ili vijitambue tu kuwa vina changamoto za kimalezi ila mjadala unatuhusu hata sisi tuliowatangulia kwasababu tuna mchango mkubwa sana kwenye mabadiliko ya kitabia kutokana na malezi ya hovyo ambayo hawa madogo wamepitia.

Kwa mfano hali ya sasa,ni kama 90% ya watoto waliozaliwa baada ya 2015 hawatabahatika kupata malezi ya Baba na mama kwapamoja,ni aidha mama pakee yake, bibi, baba, au nyumba za yatima, na mbaya zaidi wataona kama mtu aliyetoka familia ya baba na mama ni tatizo au dosari. Hii inanitisha sana kwasababu ndio msingi wa kujenga jamii ya hovyo zaidi siku za baadae ambapo watoto wachanga hawatakuwa salama, wanawake hawatakuwa na mtetezi, wazee hawatapata mtetezi, na jamii itaongozwa na wahuni na makundi yao.

Tupambane saa hii mapema,kujenga na kuisimamia jamii sio jambo la mtu m'moja.
 
Case closed
 
wanaonekana ni don’t care na wanajua how to mind their own business, kama wazungu tuu
Ni tatizo kubwa sana kitabia. Wazungu wenyewe wakija Africa huwa wanashangaa sana kuona asili ya binadamu kuishi hivi maana hawajawahi kuona vijana wanalea wazee wao kwa upendo hakuna clinic za wazee, familia kuwa pamoja, kutembeleana, watoto kutii wakubwa wakifuata maamuzi na malekezo yao, wanawake watii kwa wanaume zao na kuwa na watoto wengi, hivi vitu huwastaajabisha sana wazungu na kuona kumbe wao wamekuzwa na utamaduni wa tofauti sana.
 
Umezaliwa mwaka gani kwanza wewe dogo,ntakutandika hapa sasa hivi.
Mwaka ule wakubwa zetu mliaminishwa ni mwisho wa dunia na mkakubali kisa Computer zimesoma 2YK, kaka mkubwaa wa Gen Zers wote hapa.
Hahahaha!
 
Mkuu, hili jambo la kulalamika kukiona kizazi cha tofauti na chako kuwa hakiko sawa, halijaanza leo, na wala halitawahi kuisha.

Kumbuka na kizazi cha mbele pia huwa kinashangaa sana mambo ya kizazi cha nyuma.

Mfano, ulishawahi kujiuliza kwa nini wengi kati ya kina baba zetu walikuwa wakikasirika sana pindi walipoombwa kutoa pesa ya kununulia mboga? Kina mama zetu wamelalamikia sana hilo jambo.

Sasa hivi hao kina baba wanashangaa kuona sisi tunafanya shopping ya mwezi mzima kujaza mboga kwenye jokofu wakati soko liko jirani tu unaweza kununua vitu fresh kila siku.

So inawezekana kabisa tabia za kikazi kimoja zina athari kwenye tabia za kizazi kingine.

Sisi tumekuwa tukiitwa "Watoto wa siku hizi". Nakumbuka kuna mwalimu wangu mmoja aliuliza, "Hivi huyo Siku Hizi ni nani jamani? Mbona kila mtoto ni wake?".

Sasa tumekua, hiyo siku hizi hatuitumii tena, tumehamia Gen Z. Wao pia wanatushangaa tabia zetu, na watashangaa tabia za watoto wao.
 
Daah mzee 1-12 kuhusu gen z ni kweli kuna mmoja ivi nilikuwa nadate nae asa ghafla akabreak up na mm na kudate na jamaa mmoja ivi aliyeonekana ana pesa kuliko mm...😂😂kumbe yule jamaa mm ndio nampa pesa.Hivi vigen z daah viko complicated n foolish sana
 
hahahaha ndugu mwandishi, haya uliyoandikla ni ya kweli kabisa.

vijana wa rika langu wengi wanaingia hapa kasoro mimi.

huwa nawaambia vijana wenzangu kuwa mimi niliishi ugiriki ya kale, so siwezi ishi kama wao.

kwani ! ngoja niulize, hadi sisi wa aftisa mia mwishoni nasi ni gen z?
 
Eti foolish 😂 kumbe kalikupiga chini
 
Waacheni, kila generation na mambo yake, nyie old school mna nini zaidi ya kuongeza umaskini generation nzima na kuibiana kura, nyie hamtakiwi kusikilizwa mmeharibu nchi , na mimi sio Gen Z
 
Kaunzia 1995 ila officially ni kuanzia 1997
 
Waacheni, kila generation na mambo yake, nyie old school mna nini zaidi ya kuongeza umaskini generation nzima na kuibiana kura, nyie hamtakiwi kusikilizwa mmeharibu nchi , na mimi sio Gen Z
Hebu kelele hapo, wewe usiwe generation Z kwasababu zipi sasa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…