Leo ni 9/11: Tujikumbushe mwanzo wa harakati ulioanzia na shambulio la ubalozi wa US Tanzania na Kenya

Leo ni 9/11: Tujikumbushe mwanzo wa harakati ulioanzia na shambulio la ubalozi wa US Tanzania na Kenya

gammaparticles

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2024
Posts
1,407
Reaction score
3,855
Shambulio la Bomu Dhidi ya Balozi za Marekani (Kenya na Tanzania)
Soma pia:FBI walivyomdaka Thomas Lyimo 1998
Imepita miaka 25 tangu shambulio la bomu la ubalozi wa Marekani jijini Nairobi na Dar es Salaam kusababisha maafa na kuacha majeruhi.

Waathiriwa hao bado wanasaka fidia kutoka kwa serikali ya Marekani.

Soma zaidi: Miaka 20 baada ya mashambulizi ya pamoja Kenya na Tanzania, Ugaidi bado ni kitisho

Douglas Sidialo ni mmoja ya waliojeruhiwa kwenye shambulio hilo la kigaidi la mwaka 1998, naye anasema maisha yake yalibadilika na alipoteza uwezo wake wa kuona.

"Kwa sasa nahitaji usaidizi kufanya shughuli za kila siku." Anasema manusura huyo.

Ili kuiongeza kasi ya kudai fidia kutoka kwa serikali ya Marekani, Kamati ya Muda ya Seneti ilianzisha mchakato mpya. Kwa mujibu wa mwenyekiti wa kamati hiyo, Agnes Kavindu, anasema "upo mpango wa kukutana na baraza la Seneti la Marekani ili kufuatilia suala la fidia."

Tuzo kwa Mahakama inaahidi kutoa tuzo ya hadi dola milioni tano kwa taarifa kuhusu mashambulio ya mabomu ya mwaka 1998 dhidi ya Balozi za Marekani nchini Kenya na Tanzania. Mnamo tarehe 7 mwezi Agosti, mwaka 1998, wanachama wa kundi la kigaidi la al-Qa’ida (AQ) sawia walishambulia kwa mabomu Balozi za Marekani Nairobi na Dar es Salaam. Mashambulio hayo yaliwaua watu 224, yakawajeruhi wengine zaidi ya 4,500, na yakasababisha hasara kubwa kwenye majengo ya balozi hizo na uharibifu wa miundo iliyokuwa karibu.

Jijini Nairobi, magaidi walilipua lori lililobebeshwa vilipukaji karibu na maegesho ya ubalozi huo na kuwaua watu 213 — wakiwamo wafanyakazi 44 wa ubalozi (Wamarekani 12 na raia 32 wa mataifa ya kigeni) — na kuwajeruhi watu wengine 4,500, akiwamo Balozi wa Marekani Prudence Bushnell.
Jijini Dar es Salaam, magaidi walioendesha loriu lililobebeshwa vilipukaji walijaribu kuligonga lango la ubalozi, wakapiga risasi masijala ya ubalozi, na halafu wakalipua vilupukaji vyao. Mlipuko huo uliwaua watu 11 na kuwajeruhi 85.

Watu wafuatao walishtakiwa na kupatikana na hatia kwenye mahakama ya serikali kuu ya Marekani kuhusiana na mashambulio hayo:
  • Mamdouh Mahmud Salim, mwanachama mwanzilishi wa AQ, alikamatwa mnamo mwezi Septemba, mwaka 1998 nchini Ujerumani na kurejeshwa Marekani. Anatumika kifungo cha maisha gerezani kwa kuhusiana kwake na mashambulio hayo ya mabomu.
  • Mnamo mwezi Oktoba, mwaka 2001, majasusi wa AQ Wadih El-Hage, Khalfan Khamis Mohamed, Mohamed Rashed Daoud Al-Owhali, na Mohamed Sadeek Odeh walipatikana na hatia kwa mashtaka ya kupanga na kutekeleza mashambulio hayo ya mabomu na wakahukumiwa kufungwa maisha gerezani.
  • Mnamo mwezi Januari, mwaka 2011, jasusi wa AQ Ahmed Khalfan Ghailani alipatikana na hatia na akahukumiwa kifungo cha maisha kwa jukumu lake katika mashambulio hayo ya mabomu.
  • Mnamo mwezi Septemba, mwaka 2014, Adel Abdel Bari, mshirika wa karibu wa kiongozi wa AQ Ayman al-Zawahiri, alikiri shtaka la kula njama ya kuwaua raia wa Marekani na kupokea kifungo cha miaka 25 gerezani. Aliachiliwa huru kutoka gerezani mnamo mwaka 2020.
  • Mnamo mwezi Mei, mwaka 2015, Khaled al-Fawwaz, naibu wa kiongozi wa AQ ambaye sasa ni marehemu Usama bin Laden, alihukumiwa kifungo cha maisha gerezani kwa kuhusiana kwake na mashambulio hayo.
Jopo la kusikiliza kesi la mahakama ya serikali kuu liliwafungulia rasmi mashtaka Abdullah Ahmed Abdullah, Anas al-Libi, Mohammed Atef, na Usama bin Ladin kwa majukumu yao katika mashambulio hayo. Wote wakiwa viongozi muhimu wa zamani wa AQ, sasa ni marehemu.
Tuzo kwa Mahakama pia tuzo zawadi kwa taarifa kuhusu kiongozi wa AQ Sayf al-Adl, ambaye alishtakiwa kwa jukumu lake katika milipuko ya Ubalozi.

Kesi ya mfungwa aliyekuwa akishikiliwa katika gereza la Guantanamo imeanza kusikilizwa katika mahakama ya mjini New York, Marekani, hii ikiwa ni mara ya kwanza kufanyika kesi ya aina hiyo.
Mtanzania Ahmed Khalfan Ghailani, anayetuhumiwa kusaidia mashambulio ya kigaidi katika ubalozi wa Marekani, Kenya na tanzania mwaka 1998

Mtanzania, Ahmed Khalfan Ghailani ambaye anatuhumiwa kuhusika na mauaji ya watu 224 katika shambulio la mabomu lililotokea mwaka 1998 dhidi ya ubalozi wa Marekani nchini Tanzania na Kenya, alionekana akitabasamu na kutaniana na mawakili wake wakati zoezi la kuwachagua wajumbe wa baraza la mahakama lilipokuwa likiendelea katika chumba cha mahakama mjini New York.
ngawa ulinzi ulikuwa mkali ndani ya mahakama hiyo ambayo iko jirani na eneo lilipokuwa kituo cha biashara cha kimataifa kilichoteketezwa wakati wa shambulio la kigaidi la Septemba 11, maeneo kuzunguuka eneo hilo ilikuwa katika hali ya kawaida, huku watalii, wafanyakazi na wakaazi wa eneo hilo wakiendelea na shughuli zao.

Jana Jaji Lewis Kaplan alichuja jopo la wajumbe hao, ambao hawatajulikana muda wote wa uendeshaji kesi hiyo.

Amefafanua kuwa yeye na wanasheria wa pande zote mbili walikubaliana kupunguza jopo hilo, kutoka mamia ya watu hadi kufikia watu 12, ikiwemo wale wa akiba, ifikapo Jumatatu.

Na katika kuonesha kuwa kesi hiyo ni nyeti, Jaji Kaplan alisisitizia kuhakikishia majaji wa baraza la mahakama kwamba majina yao, sehemu wanazofanyia kazi na makaazi yao hayatawekwa hadharani.

Mwaka jana, Ghailan alikanusha kusaidia mipango ya shambulio hilo la mabomu katika ubalozi wa Marekani Dar es Salaam, Tanzania, huku bomu jingine likilipuka katika muda huohuo kwenye ubalozi wa Nairobi Kenya.

Anadaiwa pia kuwa msaidizi wa karibu wa Osama bin Laden.

Wanasheria wake walijaribu kuizuia kesi hiyo, wakihoji kuwa haki za kisheria za mteja wao zimekuwa zikikandamizwa kutokana na kuteswa katika gereza la siri la shirika la Ujasusi la marekani CIA, na pia kuwekwa kizuizini kwa miaka mitano, ikiwemo katika gereza la Guantanamo, kabla ya kesi yake kusikilizwa mahakamani.

Anakabiliwa na kifungo cha maisha, iwapo atatiwa hatiani.

Kesi hiyo ni mtihani kwa Rais wa nchi hiyo Barack Obama kwa ahadi yake ya kumaliza mateso na ukiukaji wa haki katika vita dhidi ya ugaidi. Kwa mara ya kwanza kesi hiyo ilisikilizwa jana Jumatano.

Itakumbukwa kuwa lori lililosheheni mabomu liliripuka nje ya ubalozi wa Marekani uliokuwa katikati ya jiji la Nairobi na shambulio jengine lilitokea Dar es Salaam katika nchi jirani ya Tanzania kwa wakati mmoja.

Marekani ilimtuhumu kiongozi wa kundi la kigaidi la Al Qaeda, Osama Bin Laden aliyeuawa mwaka 2011, kwa kuamuru na kupanga mashambulizi hayo.
1726087460733.png
1726087428734.png

1726087399426.png

1726093182821.png

1726093228514.png

1726093261041.png

1726093505636.png

1726093555502.png

1726093584912.png

1726093627730.png

1726093676229.png
 
Ukitaka kucheka na ndipo ujue askari wa hapa bongo ni viazi, baada ya tukio wakaanza uchunguzi, namnukuu askari waliokuwa kwenye zoezi kutafuta magaidi .

“Baada ya Ubalozi kulipuliwa sisi polisi tulifanya kazi moja tu. Hatukufanya uchunguzi, ila hatua ya kwanza ilikuwa ni kukamata kila aliyekuwa jirani na Ubalozi, aliyepita au tuliyemwona anapepesa macho. Baada ya siku tatu mahabusu za Central Polisi, Oysterbay na Salender zote zilijaa watuhumiwa. Ilikuwa hawana hata mahala pa kukanyaga, maana tulikuwa tunakamata kila tuliyemshuku.

“Baadaye walikuja askari wa FBI kutoka Marekani. Wakasema mbona mmekamata watu wengi hivi? Tukawaambia tunawashuku. Wakasema hapana. Haki za binadamu haziendi hivyo. Hapaswi kukamatwa mtu kwa kumshuku, bali mtu anakamatwa baada ya kufanya uchunguzi na kupata ushahidi usiotiliwa shaka. Tukawauliza sasa tufanyeje?

“Wale FBI walisema leteni meza hapa nje. Tukapeleka meza. Wakasema waiteni wote wanaotuhumiwa mliowakamata kisha apite mmoja mmoja tutawaambia nani ni gaidi au ameshiriki kulipua ubalozi. Tukaweka meza, tukawaita watuhumiwa wakapita mmoja baada ya mwingine. Walikuwa wengi kweli. FBI baada ya zoezi lile wakasema waachieni wote hawa hakuna mtuhumiwa hata mmoja. Tukawauliza, tukiwaachia tutaanzia wapi upelelezi? Wakatwambia waachieni tu, tutazungumza. Tukawaachia.

“Tulipoingia kwenye kikao, wakasema wale wote mliowakamata hawajui lolote katika tukio la kulipua Ubalozi. Wakatuuliza tunaweza kupata askari anayelifahamu vizuri Jiji la Dar es Salaam? Tukawaambia ndiyo. Wakasema mleteni. Akaletwa (jina linahifadhiwa) kutoka makao makuu. Wakamuuliza unafahamu eneo linaloitwa Kimara? Akasema ndiyo. Wakasema tupeleke.....

********************************

Hapo chini polisi(koplo) anaulizwa mahakamani kwenye kesi ya Mbowe, Terrorism ni nini? Anajibu ni mambo ya utalii 🤣😂
Kwa style hii Mbowe yupo sawa kuita hao Scotland Yard, hapa bongo kuna mabumunda 😂🤣
1635506968531-png.1990831
 
Ulipolipuliwa ubalozi nlikuwa na mchakato wa kuhudhuria interview ya ku apply visa hapo
Chupuchupu yangu nlipata safari
Ya kwenda moro,siku ubalozi unalipuliwa nlikuwa morogoro
Hiyo ndiyo ilikuwa pona yangu
Hapo jirani laibon kulikuwa na familia moja wakuna luhanga
Nlikuwa naendaga sana kwao
Wao pia waliathirika na bomu
Nliporudi dar nkaenda kuwajulia hali na pale nliona madhara,mke wa luhanga mama pale alipata madhara

Ova
 
Ukitaka kucheka na ndipo ujue askari wa hapa bongo ni viazi, baada ya tukio wakaanza uchunguzi, namnukuu askari waliokuwa kwenye zoezi kutafuta magaidi .

“Baada ya Ubalozi kulipuliwa sisi polisi tulifanya kazi moja tu. Hatukufanya uchunguzi, ila hatua ya kwanza ilikuwa ni kukamata kila aliyekuwa jirani na Ubalozi, aliyepita au tuliyemwona anapepesa macho. Baada ya siku tatu mahabusu za Central Polisi, Oysterbay na Salender zote zilijaa watuhumiwa. Ilikuwa hawana hata mahala pa kukanyaga, maana tulikuwa tunakamata kila tuliyemshuku.

“Baadaye walikuja askari wa FBI kutoka Marekani. Wakasema mbona mmekamata watu wengi hivi? Tukawaambia tunawashuku. Wakasema hapana. Haki za binadamu haziendi hivyo. Hapaswi kukamatwa mtu kwa kumshuku, bali mtu anakamatwa baada ya kufanya uchunguzi na kupata ushahidi usiotiliwa shaka. Tukawauliza sasa tufanyeje?

“Wale FBI walisema leteni meza hapa nje. Tukapeleka meza. Wakasema waiteni wote wanaotuhumiwa mliowakamata kisha apite mmoja mmoja tutawaambia nani ni gaidi au ameshiriki kulipua ubalozi. Tukaweka meza, tukawaita watuhumiwa wakapita mmoja baada ya mwingine. Walikuwa wengi kweli. FBI baada ya zoezi lile wakasema waachieni wote hawa hakuna mtuhumiwa hata mmoja. Tukawauliza, tukiwaachia tutaanzia wapi upelelezi? Wakatwambia waachieni tu, tutazungumza. Tukawaachia.

“Tulipoingia kwenye kikao, wakasema wale wote mliowakamata hawajui lolote katika tukio la kulipua Ubalozi. Wakatuuliza tunaweza kupata askari anayelifahamu vizuri Jiji la Dar es Salaam? Tukawaambia ndiyo. Wakasema mleteni. Akaletwa (jina linahifadhiwa) kutoka makao makuu. Wakamuuliza unafahamu eneo linaloitwa Kimara? Akasema ndiyo. Wakasema tupeleke.....

********************************

Hapo chini polisi(koplo) anaulizwa mahakamani kwenye kesi ya Mbowe, Terrorism ni nini? Anajibu ni mambo ya utalii 🤣😂
Kwa style hii Mbowe yupo sawa kuita hao Scotland Yard, hapa bongo kuna mabumunda 😂🤣
1635506968531-png.1990831
😂😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom