Leo ni Kumbukizi ya Nguli wa Muziki Congo DR na Afrika Franco A.K.A Le Grand Mitre

Leo ni Kumbukizi ya Nguli wa Muziki Congo DR na Afrika Franco A.K.A Le Grand Mitre

Uzi wa popoma bila matusi ni makamasi
 
Franco Luambo Makiadi A.K.A Le Grand Mitre (Mwalimu Mkuu) atakumbukwa kwa mengi ila makubwa ni haya yafuatayo;

1. Utunzi makini.
2. Upangiliaji wa nyimbo.
3. Upigaji bora wa solo gitaa.
4. Uibuaji wa vipaji vya muziki.
5. Nidhamu kwa wanamuziki.
6. Sebene la muda mrefu.
7. Kuchomekea majina katika nyimbo.

Sifa yake nyingine binafsi alikuwa ni mtu wa kupenda sana kula ugali, kisamvu, samaki na pilipili nyingi.

Marehemu Franco ndiyo icon ya muziki wa Congo DR (zamani Zaire) na ndiyo maana mpaka leo 99% ya wanamuziki wakubwa na maarufu wa huko huenda kuhiji katika kaburi lake ili kupata baraka zaidi kimuziki kama Jean Bedele Tshituka Mpiana (JB Mpiana) A.K.A Bin Adam A.K.A Souverain Premiere A.K.A Moto Pamba A.K.A Mareshale Mukulu A.K.A Papa Cherie A.K.A Lonkia Milo Dan Kokoo A.K.A Sulutane A.K.A Mukulu ya Bamukulu na A.K.A De La Patria.

R.I.P Fundi Franco Luambo Makiadi.
Sijui ni kweli au dingi alinipanga eti "Huyu gwiji alikufa kwa ngoma alafu wakati anaugua UKIMWI alisingizia wachawi wamemroga...aliwahi watukana kwenye ngoma yake ya KIMPA KISA..."
 
Sijui ni kweli au dingi alinipanga eti "Huyu gwiji alikufa kwa ngoma alafu wakati anaugua UKIMWI alisingizia wachawi wamemroga...aliwahi watukana kwenye ngoma yake ya KIMPA KISA..."
100% Sure.
 
Back
Top Bottom