Leo ni Kumbukumbu ya kifo cha Tx Moshi William

Leo ni Kumbukumbu ya kifo cha Tx Moshi William

View attachment 488271
Leo ni Kumbukumbu ya kifo cha Tx Moshi William wa msondo ngoma Machi 29, 2017.

Marehamu Moshi William alifariki tarehe 29 Machi mwaka 2006 siku ya jumatano majira ya saa 3 asubuhi na kuzikwa siku hiyo hiyo katika makaburi ya Keko Machungwa.

Tarehe na siku ya kifo chake vimejirudia mwaka huu. Alitunga nyimbo nyingi lakini baadhi ya nyimbo zilizotia fora sana ni kilio cha mtu mzima, ndoa ndoana, kaza moyo na ajali.

Tx Moshi William ameacha pengo na kumbukumbu isiyosahaulika kwa wapenzi wa msondo na muziki wa dansi kwa ujumla hapa Tanzania na Duniani kwa ujumla.

Huyu jamaa alikuwa jembe lisilo na mpini na kompyuta isiyo na CHIP...yaani alikuwa hana mfano. Mungu ampumzishe salama huko peponi na amsamehe dhambi zake yeye pamoja na mkewe 'Asha Mwana Seif."
 
Huyo Mzee (RIP) na Diamond nani mkali?

Diamond ni msanii, si mwanamuziki. Ukibisha muulize hata Diamond mwenyewe atakuambia nani mkali kati yao. Usiwavunjie watu heshima katika kazi zao, kuna wanamuziki na wasanii. Tofautisha hii upate kuelimika.
 
RIP japo tangu utotoni nilikuwa sizipendi nyimbo zake, yani mdingi akiweka CD ya nyimbo zake nilikuwa nalaani kimoyomoyo
Post zako nyingi zimejaa kejeli hasa kwa watu waliotangulia mbele za haki.jamii ya watu kama wewe hukata kauli miezi sita hadi kumi na mbili kabla ya kukumbwa na umauti.jaribu kupunguza kejeli
 
Aiseee kweli nakumbuka miaka ya zamani 80's kuna magari ya wazungu walikuwa Ma Expert kwenye kiwanda cha kuchakata Sukari Morogoro walikuwa na gari Plate Number zimeandikwa TX.

Ni kweli TX ilisimama ikimaanisha Tanzanian eXpatriate na huyu Moshi William alikuja Juwata Jazz Band (Msondo) kama expatriate kutoka Polisi Jazz Band. Kulikuwa na TX wa mpira pia marehemu Lillah Shomari wa Simba SC akitokea CDA nadhani....
 
Kwa kuongezea Moshi alikuwa chakaramu na mbunifu wa kutunga vionjo ikiwemo mtindo uliojulikana kama "mambo hadharani" na alipenda kuchombeza vionjo vyenye kutoa raha na kunogesha wimbo kama "we nani" "kitu kidogo tu" "Kwanini lakini" "wanachezea umeme" "discipline" "fair play" n.k
Marehemu Moshi William alibatizwa jina la "TX" na mwandishi na mtangazaji wa siku nyingi wa Radio Tanzania baadae alihamia vituo vya habari vya IPP Media Marehamu Julius Nyaisanga alimbatiza jina ilo kutokana na tunzi zake za uhakika.
Jina lake halisi TX Moshi William ni SHAABAN MHOJA KISHIWA.
 
Ni kweli TX ilisimama ikimaanisha Tanzanian eXpatriate na huyu Moshi William alikuja Juwata Jazz Band (Msondo) kama expatriate kutoka Polisi Jazz Band. Kulikuwa na TX wa mpira pia marehemu Lillah Somari wa Simba SC akitokea CDA nadhani....

Ndiyo, huyo alikuwa mkoba wa Simba Lillah Shomari.

Ilikuwa Yanga wana Athuman Juma Chama "Jogoo"

Simba walikuwa na Lillah Shomari "TX"

Hawa walikuwa mabeki mshahara kwelikweli.
 
Post zako nyingi zimejaa kejeli hasa kwa watu waliotangulia mbele za haki.jamii ya watu kama wewe hukata kauli miezi sita hadi kumi na mbili kabla ya kukumbwa na umauti.jaribu kupunguza kejeli
Kejeli ipo wapi hapo??? Kwahiyo kama nilikuwa sizipendi nyimbo zake ulitaka nidanganye kwamba nazipenda??? Kiazi kweli
 
View attachment 488271
Leo ni Kumbukumbu ya kifo cha Tx Moshi William wa msondo ngoma Machi 29, 2017.

Marehamu Moshi William alifariki tarehe 29 Machi mwaka 2006 siku ya jumatano majira ya saa 3 asubuhi na kuzikwa siku hiyo hiyo katika makaburi ya Keko Machungwa.

Tarehe na siku ya kifo chake vimejirudia mwaka huu. Alitunga nyimbo nyingi lakini baadhi ya nyimbo zilizotia fora sana ni kilio cha mtu mzima, ndoa ndoana, kaza moyo na ajali.

Tx Moshi William ameacha pengo na kumbukumbu isiyosahaulika kwa wapenzi wa msondo na muziki wa dansi kwa ujumla hapa Tanzania na Duniani kwa ujumla.
RIP MOSHI, MOSHI ALIKUA NA SWAGGA ZA VIJANA, ALIKUA AKIJIPENDA SANA, ALIKUA AKIPENDA KUVAAA MA-BUKTA YA VIJANA NA CHENI, NA MA-JEANS.. NYIMBO ZA MSONDO KWENYE ALBUM ZAO ASILIMIA 80 YEYE NDIO ALIKUA MTUNZI KIFUPI ALIKUA KICHWA...
 
Kiu kweli TX alikuwa mhimili mhimu kwa msondo,moja ya nyimbo ZAKE ni AJUZA .MWENYEZI MUNGU AMPUZISHE KWA AMANI
 
Back
Top Bottom