Leo ni Kumbukumbu ya kifo cha Tx Moshi William

Leo ni Kumbukumbu ya kifo cha Tx Moshi William

Tangu jana nipo hewani na Rajabu Zomboko radio One tukimuenzi TX Moshi William, na leo tunaendelea tena usiku kumkumbuka kupitia radio one.

Baadhi ya nyimbo zake nipamoja na:

1. Amida
2. Kilio cha mtu mzima.
3. Cheusi Magala.
4. Queen Cathe.
5.
6.
7.
Asha Mwana Seif
 
Kwasababu Tanzania hatuna mfumo wa kuwakumbuka wasanii kwa michango yao!Hivyo tunapoteza kumbukumbu kwa vizazi.

Lakini ni mmoja ya wasanii wenye mchango mikubwa sana katika muziki wa dansi kutokana na tungo zilizosheheni ujumbe maridhawa na sauti yake yenye mpangilio mahsus tangu akiwa Polisi Jazz.

Niishie kwa kusema kila nafsi itaonja mauti,Pumzika kwa amani gwiji wa muziki wa dansi...
"Huku bado kwetu ukizaliwa mwanaume kila kitu kwako kitakuwa ni tabu"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
R. I. P TX moshi William
Nafikiri alilipata jina hili kutokana na umahiri wake ktk kuimba na kutunga nyimbo.Pia miaka Ile ya 80's to 90's hili neno Tx lilivuma sana likimaanisha watu ma ex part{wataalam kutoka nje ya Tanzania}Na magari waliyotumia plate no zilianza na maandishi ya Tx na magari yaliyotolewa misaada na mashirika ya nje na ya miradi ya msaada kama vile Danida na mengineyo ya nje
 
View attachment 488271
Leo ni Kumbukumbu ya kifo cha Tx Moshi William wa msondo ngoma Machi 29, 2017.

Marehamu Moshi William alifariki tarehe 29 Machi mwaka 2006 siku ya jumatano majira ya saa 3 asubuhi na kuzikwa siku hiyo hiyo katika makaburi ya Keko Machungwa.

Tarehe na siku ya kifo chake vimejirudia mwaka huu. Alitunga nyimbo nyingi lakini baadhi ya nyimbo zilizotia fora sana ni kilio cha mtu mzima, ndoa ndoana, kaza moyo na ajali.

Tx Moshi William ameacha pengo na kumbukumbu isiyosahaulika kwa wapenzi wa msondo na muziki wa dansi kwa ujumla hapa Tanzania na Duniani kwa ujumla.
Hawa walikuwa !st eleven ya Msondo, na wote wameshatangulia mbele za haki, hapa Tx,hapa Mbwebwe mzee masharubu,pembeni Momba, kwa mbali mzee wa kuchechemea,huku Maina akichagizwa na gwiji Gurumo. Mungu awape pumziko la milele sote tupo kwenye foleni ya umauti
 
Ivi huyu Momba nae alikufaga,,,nawependaga sana msondo
Ndio miaka mingi hawa waliongozana kwa mpigo,Momba,TX, Mbwebwe ila Mzee Gurumo alikaa kidogo nae ndio ikawa kwa heri nadhani yeye ndie alikamilisha listi baada ya Maina nae kufariki akiwa ndani ya daladala.
 
Ni wakati sasa, kuanzisha Kumbukumbu za wasanii wetu kwa jumla (Hall Of Fame)!......kwani vizazi vya sasa hawana habari wala historia kabisa juu ya Magwiji waliotangulia mbele za haki na walioleta Sifa na fahari nchini.

Mfano, ni wangapi wanajua Historia ya Mwamba; Mzee Morris na Ngoma zake Kumi????( Aliwakilisha Africa huko Osaka, kwenye Tamasha la Utamaduni wa Dunia). Kumbuka Mzee Morris alikua kipofu na mpiga misondo 10 kwa tune ambayo wazungu hawakuamini alikua kipofu!!!!
 
R.I.P all regends MSONDO NGOMA MUSIC BAND(BABA YA MUZIKI DESPLINE FAIR PLAY) MOSHI WILLIAM(Tx),JOSEPH MAINA,BWEBWE(Masharubu),MOMBA(Baba Natasha),NGURUMO(Kamanda) na legendary solo guitar MABELA(Captain)
 
Back
Top Bottom