Leo ni kumbukumbu ya miaka 25 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius K Nyerere, unakumbuka nini kuhusu huyu mzee?

Nakumbuka marehemu mzee Mkapa wkt anatangaza Kwa hisia Kali.nilikua mdogo but I remember mpk leo ilikua moja ya siku mbaya sana Kwa nchi,m.mungu awarehemu
Mto...
Utampata historia ya Mkapa na ya Mwalimu kama ilivyokuwa mwak wa 1968:


View: https://youtu.be/GR0DQyhAdHs?si=A09tkEY3pLBnwSL9
 
Aloooh! Mumbe hawa wanawake wanaishi long time...so toka husband aende six feet mke anadunda miaka 25 and still kicking
 
Mkuu Wahuni wa Hamas wanahusika vipi kwenye huu Uzi?wale ni wahuni tu ndo mana wanashughulikiwa KIHUNI huko Gaza.
 
Kaacha katiba mbovu.

Katiba ndio msingi wa utawala bora.

Kwangu mimi siku hii naiadhimisha kama hasara kubwa nchi ilipata kwa Oscar Kambona kutokuwa rais.
 
Leo ni miaka 25 ya kumbukizi ya kifo cha Mtumishi wa Mungu Julius Kambarage Nyerere, huku Kanisa Katoliki likiendelea na mchakato wa mkumtangaza kuwa Mwenye Heri na hatimae Utakatifu. TUMUOMBEEEE!!
Baadhi ya mabaya au ubovu wa Mwl. Nyerere:-
1. Kuiga, Kuanzisha na kuendeleza Sera na Itikadi Mbaya kabisa ya Siasa za Ukomunisti/Ujamaa hapa Tanzania.

Huu ndio ulikuwa mwanzo wa Kujenga Msingi mbovu wa Taifa la hovyo kabisa lililopo hivi sasa.
Itikadi na Sera ya Ukomunisti/Ujamaa ikaja kushindwa vibaya Sana huku yeye mwenyewe akishuhudia kwa macho yake kushindwa kwa itikadi yake aliyoileta hapa Tanzania kutoka kwa marafiki zake wa China, Urusi na Cuba.

2. Kutengeneza Taifa la Watu waoga, Wanyonge, dhaifu wa fikra wasiojitambua na Wala wasioweza kuhoji. Taifa la watu 'misukule'.

3. Kutengeneza au kuunda nchi isiyokuwa na Mipango-miji, hususani kupitia kwenye Sera yake mbaya kabisa ya ujamaa/Ukomunisti. Sera au Itikadi hiyo ya Ujamaa/Ukomunisti ndio ilikuwa chanzo Cha Kuanzishwa kwa Azimio la Arusha na Operesheni Vijiji, the Worse Operation that completely destroyed the Country and Town Planning process within the Country.
Arusha Declaration and Operation Vijiji also led to the Death of Real Estate Industry and its development.

Kupitia Itikadi hiyo ya Ujamaa/Ukomunisti, Azimio la Arusha na Operesheni Vijiji, Watu wengi sana walinyang'anywa Ardhi zao pamoja na majumba yao waliyokuwa wakimiliki. Nyumba nyingi sana za Watu zilitaifishwa, Leo hii nyumba hizo zinamilikiwa na Shirika la Nyumba (NHC).

4. Kutuletea Katiba ya nchi ambayo ni mbaya kabisa, isiyofaa na ambayo imesababisha na inaendelea kusababisha madhara makubwa sana kwa Raia. Katiba mbaya ambayo imewatengeneza Watawala wa nchi hii kuwa 'Miungu Watu.'
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…