Leo ni miaka 20 tangu kufariki kwa Rais Mobutu Seseseko Kukungedu Wanzabanga wa Zaire ya Zamani(Congo DRC)

Leo ni miaka 20 tangu kufariki kwa Rais Mobutu Seseseko Kukungedu Wanzabanga wa Zaire ya Zamani(Congo DRC)

Freed Freed

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2017
Posts
6,547
Reaction score
7,167
Habari zenu familia ya JF.
Wadau mtakumbuka bara hili liliwahi kutawaliwa na viongozi wadhalimu na Madikteta wa hatari. Zaire ama Congo DRC iliwahi kutawaliwa na Mobutu Sseseseko 1965 hadi 17/05/1997. Alipinduliwa na Laurence Kabila kwa msaada wa Banyamulenge wa Rwanda nyuma ya Kagame.

Huyu bwana alikuwa anajiita pia Kukungedu wa Zabanga, maana yake jogoo katikati ya majogoo. Alipora madini ya Zaire(Congo) kwa kuweka fedha za nchi kwenye akaunti yake binafisi. Alikuwa hanywi wala kuoga maji ya Congo DRC. Kulikuwa na ndege ya kuleta maji yake kila wiki kutoka Paris ufaransa.

Alipinduliwa akiwa mgonjwa wa kansa na wakati vuguvugu la mapinduzi likianza alikuwa yupo ufaransa matibabuni. Alijaribu kurejea nyumani kuzima uasi lakini jeshi lake lilikuwa dhaifu sana Mbele ya Banyamulenge wa Rwanda. Baada ya muda wa takribani miezi minane ya uasi kuanzia mash mwa nchi majeshi yalifika Kinshasa huko Magharibi na kutwaa dola.

Alikufa akiwa tajiri mkubwa sana. Alikufa tarehe 07/09/1997 huko Morocco na alizikwa Rabat mji mkuu wa Morocco na watu 15 tu wa familia yake baada ya serkali ya kabila kukutaa mwili wake kurejeshwa Congo kutokana na kuchukiwa sana na Wazaire/Wakongomani.
 
Huyu mtemi alioa identicle twins

images
 
Mke wake wa kwanza Antonella alikufa baada ya kupigwa mpaka kupoteza fahamu akiwa njamzito. Ingawaje aliwahishwa hospital Belgium lakini mauti yalimfika
Sky Eclat thanks kwa Maelezo yako kuhusu huyu mshenzi..Mobutu..Kiukweli huwa nikiangalie ile ya clip ya pale Patrice Lumumba alivyokamatwa na wale askari wa Mobutu na kufungwa kamba mikono nyuma huko analazimishwa kula karatasi ya speech au hotuba yake ya mwisho huku Mobutu akiaangalia kwa dharau kabla hajasafirishwa kwenda jimbo la kati la Kasai kisha kuuwawa inasikitisha sana.
 
Kuna wakati nilidhani wa Zaire walikuwa ama wajinga ama wazembe kuwa na kiongozi ka Mobutu !! Mhh nilidanganyika!!

Tanzania tuombe Mungu atunusuru na viashiria, najifunza kuwa hata ujerumani walifanya uchaguzi tena wa kidemocrasy kumpata Adolf Hitler aliyekuja kuwafanya mbaya

Cairo's
 
Back
Top Bottom