Habari zenu familia ya JF. Wadau mtakumbuka bara hili liliwahi kutawaliwa na viongozi wadhalimu na Madikteta wa hatari. Zaire ama Congo DRC iliwahi kutawaliwa na Mobutu seseseko 1965 hadi 17/05/1997. Alipinduliwa na Laurence kabila kwa msaada wa Banyamulenge wa Rwanda nyuma ya Kagame. Huyu bwana alikuwa anajiita pia kukungedu wa Zabanga, maana yake jogoo katikati ya majogoo. Alipora madini ya Zaire(Congo) kwa kuweka fedha za nchi kwenye akaunti yake binafisi. Alikuwa hanywi wala kuoga maji ya Congo DRC. Kulikuwa na ndege ya kuleta maji yake kila wiki kutoka Paris ufaransa. Alipinduliwa akiwa mgonjwa wa kansa na wakati vuguvugu la mapinduzi likianza alikuwa yupo ufaransa matibabuni. Alijaribu kurejea nyumani kuzima uasi lakini jeshi lake lilikuwa dhaifu sana Mbele ya Banyamulenge wa Rwanda. Baada ya muda wa takribani miezi minane ya uasi kuanzia mash mwa nchi majeshi yalifika Kinshasa huko Magharibi na kutwaa dola. Alikufa akiwa tajiri mkubwa sana. Alikufa tarehe 07/09/1997 huko Morocco na alizikwa Rabat mji mkuu wa Morocco na watu 15 tu wa familia yake baada ya serkali ya kabila kukutaa mwili wake kurejeshwa Congo kutokana na kuchukiwa sana na Wazaire/Wakongomani.