Leo ni miaka 20 tangu kufariki kwa Rais Mobutu Seseseko Kukungedu Wanzabanga wa Zaire ya Zamani(Congo DRC)

Rais Josef Desire Mobutu Sessesseko.
Ameacha watoto 21; Ameoa mara 2; Vimada 5.
Baadhi ya watoto wake ni wafanya biashara wakubwa sehemu mbalimbali ikiwemo hapa Tanzania. (mfano: Kampuni ya usafirishaji ya Merzario-Inamilikiwa na Nzanga Ngbangawe Mobutu, anaishi Rabat-Morocco ambae ni mtoto wa kwanza wa mke wa pili wa Mobutu aitwae Bobi Ladawa).
Miongoni mwa vimada wa Rais Mobutu ni Kosia Ladawa (huyu ni pacha wa kuzaliwa pamoja na Bobi Ladawa ambae aliletwa kama yaya wa kulea watoto wa dada yake hatimae alizaa watoto 4 kwa Rais Mobutu Sessesseko.)
 
alinufaika na ugomvi uliokuwepo baina ya Waziri mkuu Wa wakati huo Patrice Lumumba na Rais Wa wakati huo Joseph kasavubu yeye akajitokeza katikati na kufanikiwa kuwaondoa wote na alimuua Lumumba ndo maana mpaka Leo inasemekana alikuwa akipewa Msaada na nchi ya Belgium na nchi za magharibi wakiwemo marekani....
 
Nashukru sana kaka [HASHTAG]#lucas[/HASHTAG] Mobutu kiukwel umenifungua kwa hili! Be blessed sana bro
 
Kwanini majivu ya Habyermana yalihifadhiwa na Mobutu?
Alikuwa rafiki yake mkubwa Sana, wakati hayati Habyarimana akiwa Dar kabla ndege yao haijatunguliwa, Mobutu alimpigia simu kumwonya asipande ndege hiyo, Habyarimana akachanganyikiwa, wakati akihangaika kuingia na kutoka nje ya ndege, vijana maalumu wa TISS, wakampigia simu Nyerere kumwambia, ndipo Nyerere akatoa agizo kuwa, akiingia tu tena ndani ya ndege mlango ufungwe haraka na kisha ndege iondoke hata kabla hajafunga mkanda.
Ndivyo ilivyokuwa, Na kweli ndege ikaondoka.
Mobutu alikuwa na taarifa za kiintelijensi kuwa ndege ingelipuliwa na alizipata mara tu baada ya Habyarimana kuondoka Kigali kuja Dar.
Kuna mengi mno ya kutisha ila acha tu niishie hapa.
 

Roho yake imemvaa mtu flani
 

Hiyo Ikibinda nkoy imetoka mbali kumbe
 
Katika kuiprote Zaire duniani Mobutu aliitisha shindano la ngumi kati ya Mohamed Ali na mpiganaji mwingine mshindi aliondoka na $ 50 million huo ulikuwa mwaka 1976. Dunia nzima ilitune TV kuangalia ngumi za Kinshasa

Ali bomayeni
 
Mkuu huyu wajeruman wanamuona shujaa aliyetukuka
 
Mobutu, Idd Amin, Kamuzu Banda na Basiste wa Central Africa ninawajua vizuri sana
naomba ukipata muda tuwekee uzi wa kila mmoja na sisi wahenga wa 90's tujifunze, napenda sana kujua ya kale kabla sijakuwepo duniani.
 
Katika kuiprote Zaire duniani Mobutu aliitisha shindano la ngumi kati ya Mohamed Ali na mpiganaji mwingine mshindi aliondoka na $ 50 million huo ulikuwa mwaka 1976. Dunia nzima ilitune TV kuangalia ngumi za Kinshasa
alaaa kumbe hii ndio sababu ya M.A kwenda zaire kipindi kule.!!?
kuna video nimeona mohammed alienda zaire, aisee.!
 
ebu funguka chief...
kwanini nyerer aliamuru huyo jamaa aingie na ndege iondoke ilhali kulikuwa na tetesi za kutunguliwa?
TISS walihusika vipi?
 
Safi sana mkuu,nina swali,je ni kweli kwamba mobutu nae alitakiwa kuja arusha kuhudhulia kile kikao na baadae apande hiyo hiyo ndege na kina habyarmana ?
 
Muachage vya kuzua. Habyarimana aliuawa mwaka 1994. Wakati huo Nyerere alikuwa mstaafu analima kijijini kwake Butiama, na akiwa Dar aliishi kwake Msasani, hakuwa na mamlaka tena juu ya hiyo TISS.
 
Hata Nyerere, miaka miwili kabla ya kifo chake, katika sherehe ya kuadhimisha miaka 75 ya kuzaliwa, alisema ana afya nzuri sana na kwamba ANA UHAKIKA ataishi kumuona rais wa awamu ya nne! Naye pia alipougua hakupona. Mungu hadhihakiwi!
Ila hakusema kwa kujiamini, kama utakumbuka alisema labda mnitilie fitna(sikumbuki neno kwa neno) ndio sitaweza kuishi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…