Leo ni miaka 6 tangu Tundu Antipas Lissu ashambuliwe kwa risasi na Watu wasiojulikana

Leo ni miaka 6 tangu Tundu Antipas Lissu ashambuliwe kwa risasi na Watu wasiojulikana

Miaka 6 tangu tukio. Lakini bado kuna siri kubwa kuhusu dereva. Hivi ni mimi peke yangu nisiyejua dereva alipo muda wote huo? Mwanzoni tuliambiwa anatibiwa (anapewa psychological treatment) Nairobi. Baadaye akaenda Ubelgiji pamoja na Lisu. Lisu mwenyewe akawa anarudi Tanzania mara kwa mara na hivi sasa anadiriki hata kufanya mikutano ya hadhara bila kudhuriwa na yo yote. Ni kitu gani kizito hicho kinachomfanya dereva asite kurudi Tanzania? Ni nani anayemgharamia kuishi huko ughaibuni siku zote hizo?
Ungekuwa mkubwa wa Polisi halafu ushindwe kupeleleza tukio kubwa la ujambazi wa kupiga risasi mtu mchana kweupe, halafu utoe kisingizio Cha dreva kutoonekana, basi ungekuwa mkubwa wa Polisi mjinga kupita maelezo.
 
Huenda nikawa mjinga kweli. Lakini ni raia tu wa kawaida na si Polisi. Ninavyoelewa, atakaye kujifunza ndiye mwerevu. Mjinga ni yule asiyetaka kujifunza. Tafadhali, naomba unijuze suala hilo ili nitoe ujinga wangu.
 
Shujaa aliagiza, akifa asipitishwe bungeni kupewa heshima za mwisho, pelekeni haraka Singida kuzika, kinyume chake, Mungu kaagiza yeye apelekww Chato haraka kuzikwa...kwa kweli Mungu ni fundi
Muongo
 
Inasikitisha sana mpaka sasa hakuna hata assailant mmoja aliyekamatwa.
 
Back
Top Bottom