Leo ni miezi mitatu imepita tokea niachane na betting (kamari)

Leo ni miezi mitatu imepita tokea niachane na betting (kamari)

Sun is Sun

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2024
Posts
1,254
Reaction score
2,014
Leo ni miezi mitatu tangu nilipoamua kuacha betting.

Believe me, nimejifunza mengi sana kwenye safari hii. Betting ilinifanya nipoteze pesa, muda na vitu ambavyo nilipaswa kutumia kujijenga. Inachakaza maisha taratibu mpaka unaweza kufika mahali unashindwa hata kununua nguo zako mwenyewe, kwa sababu pesa nyingi zinaishia kwenye betting.

Na kitu kingine nilichogundua ni kwamba, mara nyingi pesa unazoshinda leo ni zilezile pesa ulizokuwa umeliwa jana. Unashinda kidogo, unafurahi, unaendelea kucheza, mwisho wa siku unarudisha kila kitu na zaidi.

Tokea niache nimesevu hela ya kutosha, na nikiendelea hivi naenda kufanya makubwa.

Kwa vijana wenzangu msidanganywe na zile screenshots za ushindi. Kuna watu wengi wanaonyesha walichoshinda, lakini hawaonyeshi walichopoteza.

Betting inaweza kuonekana kama njia rahisi ya kupata pesa, lakini inaweza kukuchukua pesa nyingi zaidi kuliko unavyofikiria.
Acha betting. Jenga maisha yako. Tafuta kipato, jifunze, fanya kazi na vumilia.

Mabadiliko yanawezekana. IKATAE KAMARI.

Soma pia Chanzo cha umasikini kwa vijana wengi si wanawake ni kamari( betting)
 
Umeacha au umepumzika?
Mkuu nimeacha kabisa, hela nilizoliwa tokea nianze kubeti 2023 ni hela nyingi kuliko nilizoshinda... Imagine kila hela unayopata unaweka kwenye mkeka unaliwa, huku ukibaki umechakaa.

Kwa maamuzi niliyofanya, sioni WA kunirudisha kwenye KAMARI.
 
  • Thanks
Reactions: 627
Aliyekua video graphics mkubwa dr Hanskana sasa iv kazi yake kubwa ni mikeka
Kama kwake ina faida sawa, mimi tokea niache betting mwezi wa 7 nimesevu sana hela, na naona future yangu ikirudi.
 
  • Thanks
Reactions: 627
Ulianza mwaka gani kubet?
Na kila siku ulikuwa ukibet shiling ngapi?
 
  • Thanks
Reactions: 627
Leo ni miezi mitatu tangu nilipoamua kuacha betting.

Believe me, nimejifunza mengi sana kwenye safari hii. Betting ilinifanya nipoteze pesa, muda na vitu ambavyo nilipaswa kutumia kujijenga. Inachakaza maisha taratibu mpaka unaweza kufika mahali unashindwa hata kununua nguo zako mwenyewe, kwa sababu pesa nyingi zinaishia kwenye betting.

Na kitu kingine nilichogundua ni kwamba, mara nyingi pesa unazoshinda leo ni zilezile pesa ulizokuwa umeliwa jana. Unashinda kidogo, unafurahi, unaendelea kucheza, mwisho wa siku unarudisha kila kitu na zaidi.

Tokea niache nimesevu hela ya kutosha, na nikiendelea hivi naenda kufanya makubwa.

Kwa vijana wenzangu msidanganywe na zile screenshots za ushindi. Kuna watu wengi wanaonyesha walichoshinda, lakini hawaonyeshi walichopoteza.

Betting inaweza kuonekana kama njia rahisi ya kupata pesa, lakini inaweza kukuchukua pesa nyingi zaidi kuliko unavyofikiria.
Acha betting. Jenga maisha yako. Tafuta kipato, jifunze, fanya kazi na vumilia.

Mabadiliko yanawezekana. IKATAE KAMARI.
Ndo nataka nami nianze kubet nipe abc z
 
Ndo nataka nami nianze kubet nipe abc z
Tafadhali Kijana, kama unapenda future yako usiingie huko, utachakaa, utakonda, utashindwa kuelewana na familia, hutojenga, utakuwa omba omba, utakopa kila mahali, utadharaulika, utajichukia, na mwisho utatamani kujiua.. Achana na KAMARI.
 
  • Thanks
Reactions: 627
Tatizo lako uliingia kwa miguu miwili na ulitaka kuifanya kama ajira.
Na miaka 2 nimepoteza kama laki na 30 ila nilizokula ni kama milioni 4 na zaidi
Mimi nilishakimbia chama, kurudi labda nirogwe. Mabadiliko ni makubwa sana.
 
  • Thanks
Reactions: 627
Nashukuru nina mwaka sasa toka niache kubeti. Ilikuwa imefikia hatua mbaya kiasi kwamba mpaka hela ya kula unaweka mzigo ukitegemea kushinda mamillioni.
 
Mambo yote yanayotengeneza uraibu sijawahi kugusa ningali kijana,kuna wakati nahisi nitakuja kubet uzeeni.
 
Back
Top Bottom