Sun is Sun
JF-Expert Member
- Mar 13, 2024
- 1,254
- 2,014
Mkuu nimeacha kabisa, hela nilizoliwa tokea nianze kubeti 2023 ni hela nyingi kuliko nilizoshinda... Imagine kila hela unayopata unaweka kwenye mkeka unaliwa, huku ukibaki umechakaa.Umeacha au umepumzika?
Nina miaka mitatu kwenye betting, hasara, kupauka, kupoteza mda, kupoteza uhusiano na familia. Betting hasara kuliko faida.Ulianza lini betting? Ushawahi piga pesa kubwa? Kiasi gani? Mi uwa sijumlishi nilizopoteza, ni kama nimelewea tu,
Huyu amepumzika tuUmeacha au umepumzika?
Kama kwake ina faida sawa, mimi tokea niache betting mwezi wa 7 nimesevu sana hela, na naona future yangu ikirudi.Aliyekua video graphics mkubwa dr Hanskana sasa iv kazi yake kubwa ni mikeka
Ndo nataka nami nianze kubet nipe abc zLeo ni miezi mitatu tangu nilipoamua kuacha betting.
Believe me, nimejifunza mengi sana kwenye safari hii. Betting ilinifanya nipoteze pesa, muda na vitu ambavyo nilipaswa kutumia kujijenga. Inachakaza maisha taratibu mpaka unaweza kufika mahali unashindwa hata kununua nguo zako mwenyewe, kwa sababu pesa nyingi zinaishia kwenye betting.
Na kitu kingine nilichogundua ni kwamba, mara nyingi pesa unazoshinda leo ni zilezile pesa ulizokuwa umeliwa jana. Unashinda kidogo, unafurahi, unaendelea kucheza, mwisho wa siku unarudisha kila kitu na zaidi.
Tokea niache nimesevu hela ya kutosha, na nikiendelea hivi naenda kufanya makubwa.
Kwa vijana wenzangu msidanganywe na zile screenshots za ushindi. Kuna watu wengi wanaonyesha walichoshinda, lakini hawaonyeshi walichopoteza.
Betting inaweza kuonekana kama njia rahisi ya kupata pesa, lakini inaweza kukuchukua pesa nyingi zaidi kuliko unavyofikiria.
Acha betting. Jenga maisha yako. Tafuta kipato, jifunze, fanya kazi na vumilia.
Mabadiliko yanawezekana. IKATAE KAMARI.
Kama nimepumzika ni sawa.Huyu amepumzika tu
Tafadhali Kijana, kama unapenda future yako usiingie huko, utachakaa, utakonda, utashindwa kuelewana na familia, hutojenga, utakuwa omba omba, utakopa kila mahali, utadharaulika, utajichukia, na mwisho utatamani kujiua.. Achana na KAMARI.Ndo nataka nami nianze kubet nipe abc z
Mimi nilishakimbia chama, kurudi labda nirogwe. Mabadiliko ni makubwa sana.Tatizo lako uliingia kwa miguu miwili na ulitaka kuifanya kama ajira.
Na miaka 2 nimepoteza kama laki na 30 ila nilizokula ni kama milioni 4 na zaidi
Wenye roho ngumu, endeleeni kupoteza pesa na mda.Betting is not for the weak .
Sisi bado tupo sana betting Ina bajeti yake Kama ilivyo tu bajet ya bia na kuhongaWenye roho ngumu, endeleeni kupoteza pesa na mda.