Leo ni mwaka mmoja kamili toka kifo cha Shangazi wetu kilipotokea kwa kutumbuliwa utumishi Serikalini. Inasikitisha

Leo ni mwaka mmoja kamili toka kifo cha Shangazi wetu kilipotokea kwa kutumbuliwa utumishi Serikalini. Inasikitisha

DATAZ

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2012
Posts
3,799
Reaction score
10,196
Huyu Mama alikuwa Afisa Muuguzi Mkunga, mwenye elimu ya stashahada toka KCMC COLLEGE na shahada Muhimbili university.
Alifariki akiwa na miaka 58 (miaka 2 kabla ya umri wa kustaafu), kwa shinikizo la damu na heart stroke.

Kabla ya kupata maradhi haya alitumbuliwa UTUMISHI wake na serikali kutokana na "INCONSISTENCY" kwenye cheti chake cha form four

Kutumbuliwa kwake kukaenda sambamba na kukosa mafao yake kwa utumishi wa miaka 33 ndani ya serikali.

FUNZO:
Sio kila hukumu kwa mujibu wa sheria ni hukumu kwa mujibu wa haki.

RIP - SHANGAZI
 
Poleni sana! Wapo wengi sana walioumia na hata kupoteza maisha kutokana na huo uhakiki na kutumbuliwa kwa wafanyakazi waliobatizwa kuwa wafanyakazi hewa. Pia wapo wengine waliokufa kwa kusubiri mafao, ajira, nyongeza ya mishahara na kupanda madaraja.

Ila pia kuna wanafunzi wa ST. JOSEPH, UDOM (special diploma) walipoteza uhai kwa mshtuko wa moyo na hata presha kupanda kisa tu waliamriwa kupotea chuoni ndani ya masaa 24 na kuitwa vilaza

All in all haya ni mapito aliyoandikiwa kila mmoja wetu hivyo ni jambo la kumshukuru Mungu
 
Huu utaratibu wa Kila mtu kujiona anapaswa kufikiriwa ndiyo ulokua unalalamikiwa miaka nenda rudi,unajisikiaje mtu anafanya kazi kwa Vyeti vya ujanja janja then wewe mwenye Vyeti visivyo na shaka unahangaika upo uraiani.

Hili fagio bado lilipaswa kuendelea tu na hakuna huruma iwe umefanya kazi hata miaka100,lazma uwajibishwe.

We huoni kiasi gani manesi feki wanavyokatiza maisha ya wagonjwa wangapi mahospitali?

Nimeshuhudia watu wakitengeneza Vyeti feki na hata Mimi nishaombwa cheti changu kieditiwe mtu aingizwe kwenye system na Mkubwa mmoja bwana wake mdada aliyekua rafiki yangu.

Haya Mambo ukiangalia kijujuu na kihuruma huruma nchi haitoenda na utaishiwa kulaumiwa tu Kama utawala wa J.k
 
Unatumbua watu na wala hufanyi replacement , na unawanyima stahiki zao , hii nchi yetu sote , hata kama kuna makosa yalifanyika , wapewe stahiki zao , yeye Maghufuli kwenye uchaguzi alitenda haki? Yeye alijiona yupo juu ya sheria.....Mungu akiamua amhukumu Sawa Sawa na matendo yake tutafika ??

Jamaa alikuwa na mission yake tuu ya hovyo , apumzike Tu Kwa amani......kaumiza watu wengi Sana tena kundi aliloumiza ni la middle income people na high income unatamka wazi wazi unataka matajiri waishi kama mashetani how comes ? Wamekukosea nini ?na amesababisha kuwe na mlundikano wa mabanda kwenye miji watu wakiishi kwenye ufukara mkubwa .....

Kwa kisingizio cha Raisi wa wanyonge
 
Unapowanyima watu haki zao & kuwapa mateso basi moja kwa moja unajiondolea ulinzi wa nafsi yako na kuwa kwenye hatari kubwa ya umauti..maana roho wa Mungu anajitenga mbali na nafsi yako huku roho chafu ya umauti inakuwa tayari ishapewa kibali ya mashambulizi...

Hii ni sheria katika ulimwengu usioonekana.
 
Pole Sana Mkuu, nami nina Dada yangu ambae yeye ilikuwa imebaki miaka 8 astaafu. Yeye alitumia cheti kisicho chake kujiunga na Chuo cha Ualimu, pamoja na kwamba hii Kozi ya Ualimu alisoma yeye mwenyewe. Huyu ajafariki lakini maisha anayoishi yanatia Simanzi.
 
Mh: "Nimtumbue? Nisimtumbueeee?
Wananchi: Mtumbueeeeee!
Hizi ndo tutazimisi sana japo jamaa alikufa kwa presha baada ya kutumbuliwa
 
Back
Top Bottom