Leo ni mwaka mmoja kamili toka kifo cha Shangazi wetu kilipotokea kwa kutumbuliwa utumishi Serikalini. Inasikitisha

Leo ni mwaka mmoja kamili toka kifo cha Shangazi wetu kilipotokea kwa kutumbuliwa utumishi Serikalini. Inasikitisha

Huu utaratibu wa Kila mtu kujiona anapaswa kufikiriwa ndiyo ulokua unalalamikiwa miaka nenda rudi,unajisikiaje mtu anafanya kazi kwa Vyeti vya ujanja janja then wewe mwenye Vyeti visivyo na shaka unahangaika upo uraiani.

Hili fagio bado lilipaswa kuendelea tu na hakuna huruma iwe umefanya kazi hata miaka100,lazma uwajibishwe.

We huoni kiasi gani manesi feki wanavyokatiza maisha ya wagonjwa wangapi mahospitali?

Nimeshuhudia watu wakitengeneza Vyeti feki na hata Mimi nishaombwa cheti changu kieditiwe mtu aingizwe kwenye system na Mkubwa mmoja bwana wake mdada aliyekua rafiki yangu.

Haya Mambo ukiangalia kijujuu na kihuruma huruma nchi haitoenda na utaishiwa kulaumiwa tu Kama utawala wa J.k
Sawa muondoe lakini amekufanyia kazi kwa mika 33 ameokoa maisha ya wazazi wangapi? Amezalisha kinamama wajawazito wangapi? Je kwa miaka yote hyo anastahili kuondoka bila mafao?
 
Family nyingi tuliguswa hapa ila nae ameenda tumsameeh t
 
Zoezi hili lilikuwa lakibaguzi mtu kafanya kazi miaka zaidi ya 30 unakuja kumuita ni mtumishi hewa zoezi likaendeshwa kiupendeleo wengine wakaendelea Kula mema ya nchi kama wanajeshi na mapolisi hawakuguswa
 
Back
Top Bottom