Huu utaratibu wa Kila mtu kujiona anapaswa kufikiriwa ndiyo ulokua unalalamikiwa miaka nenda rudi,unajisikiaje mtu anafanya kazi kwa Vyeti vya ujanja janja then wewe mwenye Vyeti visivyo na shaka unahangaika upo uraiani.
Hili fagio bado lilipaswa kuendelea tu na hakuna huruma iwe umefanya kazi hata miaka100,lazma uwajibishwe.
We huoni kiasi gani manesi feki wanavyokatiza maisha ya wagonjwa wangapi mahospitali?
Nimeshuhudia watu wakitengeneza Vyeti feki na hata Mimi nishaombwa cheti changu kieditiwe mtu aingizwe kwenye system na Mkubwa mmoja bwana wake mdada aliyekua rafiki yangu.
Haya Mambo ukiangalia kijujuu na kihuruma huruma nchi haitoenda na utaishiwa kulaumiwa tu Kama utawala wa J.k