Leo ni Siku ya Babu na Wajukuu......Karibuni!

Leo ni Siku ya Babu na Wajukuu......Karibuni!

wewe Mohamedi Shoshi, Mbishi kama Osama?

Kila siku tunasali, Kwa Mungu twajiombea,
Ukisali jumapili, Jumatatu wezi achia,
Jumanne unasali, hata ijumaa pia,
Ila ipo siku moja, Ya kuswali kwa pamoja.

Isilamu Ijumaa, Wakristu ni Jumapili,
Hii hiwezi zuia, hakuna tena kusali,
Mungu tunamsalia, Siku zote tunaswali,
Ila ipo siku moja, ya kusali kwa pamoja.

Iko hivyo valentini, kila siku twapendana,
Ila kwa utamaduni, Siku moja inafana,
Hatoki mtu kundini, kwenye kupendana,
Siku ya valentini, ni kama siku ishara.

Wewe ni kama kibwetere suje kutumaliza
Sala si mapenzi hili mkuu nakueleza
Mapenzi ya moyo daima hata kwavilaza

Sala ina wakati mapenzi ni kila saa
Mungu twampenda hatungoji ijumaa
Ila kumuabudu ndio yataka jamaa
Mapenzi yake hudumu kuliko mshumaa
Japo wewe ni babu sitakuita mnaa

Babu huna hoja um-limbukeni wa mapenzi
Usiwe na akili finyu kama mdudu inzi
Mapenzi ni kila siku acha ubazazi
Inabidi tukubali yetu mema malezi
Yaliyotufundisha mila zetu kuzienzi
 
Mkuu haka ka-grandi faza kanajitakia balaa tu, hivyo vijukuu alivyovitaja vitam-babua mpaka mkongojo nao ubabuke

Aisee nyie vijana, hebu kaeni kando kidogo!~
 
:laugh::laugh::laugh::laugh:You two guys makes laugh every now and then mmenikumbusha wimbo wa 50 Cent -DO YOU THINK ABOUT ME na ule wa BUSTA RHYMES - I LOVE MY CHICK

I love my man yup yup!!!
I know he thinks about me!!!
 
Babu leo kweli valentine mpaka umepata muda wa kupanga vina!!
Happy Valentine to you too sweetheart!!


Nifikishie Valentine Spesho kwa Matesha..........zatoka kwa My One and Only
 
LOL! hapana mkuu nimekuja kumchukulia babu ugoro tu

Babu wake ugoro sie vyetu vimanzi
ajinasibu kwa nahau pamoja na tenzi
Awapumbaze wajukuu wajawe mapenzi

Babu kajichokea bila busta hawezi
Babu utajidhalilisha waachie wajuzi
Babu huna haya umri wako si wajuzi
Au wewe ni fataki tukupige makwenzi
Usituharibie wana wangali wanafunzi
 
:laugh::laugh::laugh::laugh:you two guys makes laugh every now and then mmenikumbusha wimbo wa 50 cent -do you think about me na ule wa busta rhymes - i love my chick

sisi ni kama mr and mrs smith!
 
Babu leo kweli valentine mpaka umepata muda wa kupanga vina!!
Happy Valentine to you too sweetheart!!


Nifikishie Valentine Spesho kwa Matesha..........zatoka kwa My One and Only

Zimefika......

Am veeeeeeeeeeeeery happpppy today!

Wapi Marunyag?
 
Babu wake ugoro sie vyetu vimanzi
ajinasibu kwa nahau pamoja na tenzi
Awapumbaze wajukuu wajawe mapenzi

Babu kajichokea bila busta hawezi
Babu utajidhalilisha waachie wajuzi
Babu huna haya umri wako si wajuzi
Au wewe ni fataki tukupige makwenzi
Usituharibie wana wangali wanafunzi

I will be right back....ngoja nikapige desa kwenye TUKI

Naona we mbishi kama Hosni Mubarak!
 
Hii Sredi inaenda mpaka nimesahau tuko wapi?
Hivi ma-valentine mvua imeisha kipande yenu ???
 
Back
Top Bottom