Leo ni siku ya Redio Duniani, Kituo gani cha Redio unasikiliza zaidi?

Hivi ni nini kilichangia kuvuruga tasnia ya utangazi? Mpaka redio kwa sasa hazisikilizwi sana, tutasema maendeleo ya teknolojia lakini hapana mbona huko nje pia takwimu zinasema wanasikiliza sana redio?

Ukikumbuka enzi zile Kiss Fm, Radio Free, Clouds, Eatv n.k zilikuwa moto sana na vipaji vikubwa sana vilipatikana wakati ule, sasa hivi unasikiliza interview yaani mtangazaji hana kabisa uelewa wa kuuliza maswali na kuchambua mambo achilia mbali kutangaza, you know nyingi na ujuaji kibao, inafurahisha sana.

Nina muda sana sijasikiliza redio kiukweli
 
Radio Maria Tanzania,Sauti ya Kikristo nyumbani Mwako.Amina
 

RFA the sound of Afrika hasa dw,voa na bbc swahili.
Pia Sibuku fm kusikiliza vipindi vya Dr mtume na nabii mwamposa the bulldoza,sema ayayaa
 
Mimi mara nyingi nasikiliza vipindi tu katika redio tofauti.

EA Radio - SPorts Extra/Plannet/Mama Mia/Morning Break Fast Often/Jumapili saa 10 mpaka 12 Old School.

RFA - Asubuhi(6:00 -07:30) ,Usiku kuanzia saa mbili na pia Hakuna Kulala /SIntosahau /Ushauri wako/Je wajua/Je huu Uungwana/BBC/DW

Radio One - Hoja ya Leo / Mambo Mseto / Rafiki

EFM - Kunyambua na Kunyambulisha /SPorts HQ

CLouds - Njia Panda /Sports Bar
 
Nasikiliza Ufm kipindi cha U-live, kipindi pekee cha michezo ambacho mtangazaji hatokutajia kumbukumbu namba Wala hutomsimkia akikushauri utume buku, upate milioni
 
Hiki ambacho Dijaro Arungu anatangaza, nipo nakula ngoma za best naso tu hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…