Leo ni sikukuu ya kuzaliwa ya mama yangu

Leo ni sikukuu ya kuzaliwa ya mama yangu

aliyetegwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
313
Reaction score
486
Wana jukwaa, baada ya kukua nimejifunza:

Mama ni mtu aliyekaa na uhai ndani yake, akauleta duniani na kuutetea

Mama ni mtu aliyetoa uhai wake, damu, akili na jasho kwaajili ya mtoto ama watoto wake.

Nikiangalia kichanga changu ambacho hakina uwezo wa kujihudumia kwa namna yeyote namheshimu na mapenzi juu ya mama yangu yanaendelea kujengeka zaidi

Hakuna zawadi yeyote wala chochote mtoto anachoweza kumlipa mamaye kwa yale aliyotendewa ama anayotendewa maana mama hufanya yote hayo akitegemea kutokulipwa chochote na hufanya kwa furaha akijua ni majukumu yake.

Naomba tuungane kusherekea zawadi ya maisha ya mama yetu maana kwa maisha yake nasi tumeishi pia
 
Mwangalie, mheshimu na mtunze sana. Usipitishe wiki bila kumpigia kumjulia hali hata kama uko bize namna gani. Hata kama huna zawadi ya kumpa ile tu sauti yako na kumwambia kuwa mamangu nakupenda ni zawadi tosha. Wakija kuondoka inauma sana mkuu hata uwe na utajiri wa aina gani utauona bure tu; na majuto kibao. Hakuna mtu atakayekupenda hapa duniani kama mama....

Namuombea mama yako maisha marefu na yenye furaha, afya njema na amani mkuu [emoji1545][emoji1545][emoji1545]
 
Mwangalie, mheshimu na mtunze sana. Usipitishe wiki bila kumpigia kumjulia hali hata kama uko bize namna gani. Hata kama huna zawadi ya kumpa ile tu sauti yako na kumwambia kuwa mamangu nakupenda ni zawadi tosha. Wakija kuondoka inauma sana mkuu hata uwe na utajiri wa aina gani utauona bure tu; na majuto kibao. Hakuna mtu atakayekupenda hapa duniani kama mama....

Namuombea mama yako maisha marefu na yenye furaha na amani mkuu [emoji1545][emoji1545][emoji1545]
Amen, macho yangu yametokwa machozi kwa coment yako, kwa hakika nitayaishi maneno yako.
 
Tuwaombee baraka na kheri nyingi Mama zetu na wazazi wetu wote wakiwemo baba pia, kwani nao wanamchango mkubwa katika ustawi wetu hapa duniani.

Mama ni tunu, ni rafiki.
Tuwajali, tuwathamini, tuwapende.
Hakika tutaendelea kupata baraka zao.
 
Back
Top Bottom