Leo nimeanza siku yangu na balaa

NAKWEDE

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2007
Posts
27,970
Reaction score
35,168
Leo sijisikii kuwasalimia, ngoja niende kwenye hicho nilidhamiria kuwashirikisha.

Leo asubuhi muda wa saa 2.28 nilifika eneo la benki ya CRDB Tawi la Nyerere hapa Mwanza. Ilikuwa imebaki kama dakika mbili hivi wafungue milango. Nilikuta baadhi ya wateja wengine wameshafika wanasubiria muda ufike waingie ndani ya Benki kwa ajili ya kupata huduma.

Milango ilivyofunguliwa nikawa wa kwanza kuingia na kwenda moja kwa moja kwenye foleni. Tellers wakati huo walikuwa hawajaanza kuhudumia walikuwa bado wanaweka weka mambo yao sawa.

Hamadi! nikamwona dada mmoja ambaye wakati milango imefunguliwa alienda kaunta (bila shaka alikuwa anaomba kujulishwa salio lake), akaja moja kwa moja akasimama mbele yangu. Nikamuuliza vipi dada mbona unanipita? akajibu kwa shari kubwa, "unasema ninakupita, naona umechanganyikiwa wewe, hivi unajifanya hukumbuki kuwa mimi ndie nimekutangulia kufika hapa kwenye jengo la Benki, wee si umekuja umenikuta hapo nje nasubiri milango ifunguliwe!, mimi na wewe na nani amempita mwenzie?"

Niliamua kukaa kimya sikumjibu, moyoni nikasema huyu dada anataka kunianzishia siku yangu vibaya. Nikamwacha akapita akahudumiwa baadae na mie nikahudumiwa.

Niliamua kukaa tu kimya, hivi ingekuwa ni nyie wenzangu Miss Natafuta, Joseverest na wengineo mngemfanya nini huyu dada ambaye ana onesha wazi kuwa ana kisirani cha asubuhi asubuhi.
 
Mkuu we kama cyo muoga basi umekua mtumwa wa busara...kama ni mimi walinzi ndio wangeamua

Sent from my TECNO-J8 using JamiiForums mobile app
hahahaah, niliamua tu kumuacha, tena dada mwenyewe katoboa pua!
 
Pole sana na hongera kwa kubarikiwa hekima.

Kwakua amejibu kwa shari, haswa hapo kwenye "...umechanganyikiwa..." Mimi ningekua nisharusha ngumi.
 
Nilivyosoma heading Nikadhani umeanza siku zako zile wachezaji wa simba wanazofanyaga mazoezi
hahahahah ila wewe naye hapana niko fresh kabisa, mkavuuuuu hahahahah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…