Leo nimeanza siku yangu na balaa

Leo nimeanza siku yangu na balaa

hahaha wale walinzi wanaosinzia wangeniweka korokoroni masaa kadhaa kuna siku niliwahi kulianznisha upuuzi huohuo wa crdb na mifoleni na network halafu nimesimama masaa 5 kisha nafika mbele teller ananiambia kitambulisho hakitambuliki wakati ni cha kazi na ndio mshahara nilienda kuchukua hahahaha kisha nilikuwa na hangoner maana ilikuwa jumamosi hakuna aliyeweza kunitoa nje si askari wala wahudumu mpaka walinihudumia swain kwana hakuna viti pili network ilikata yaani saa 2 mpaka 6 halafu teller ananirudisha nyuma hahaha siku moja nilikutana naye mitaani akaniuliza eti mwanamke ninakuwaje mbabe namna ile ?/
nikacheka tu na kumwambia hela nihangaike kuipata kisha huku mabenk mnajifanya miungu watu kutuhangaisha na nyodo tena crdb wanga kweli...............

back to the topic huyo mwanamke angechezea vitasa nadhani tungetupwa nje wote wawili
Mie mwenzio ni mwoga kweli kupigana! naogopa kupigwa
 
MI SINA TOFAUTI NA ASHA NGEDERE NIKO NA HASIRA ZA PAPO KWA HAPO NA SIKUBALI KUSHINDWA KALE KA UKOO KETU SI UNAJUA WAMAMA WALIVYO JEURI?
vasophe! hahahaahahh huo pia ni ukoo wa mama yangu, hahahahah
 
hahahaah, niliamua tu kumuacha, tena dada mwenyewe katoboa pua!
Ulifanya jambo jema huenda sasa mngekuwa polisi kwa kesi ya ugomvi.
Kisheria. Mtu aliwahi kwenye foleni, i.e kupanga mstari unabid umuheshimu. Huyo dada hana hekima. Ulifanya jambo jema sana.
 
Leo sijisikii kuwasalimia, ngoja niende kwenye hicho nilidhamiria kuwashirikisha.

Leo asubuhi muda wa saa 2.28 nilifika eneo la benki ya CRDB Tawi la Nyerere hapa Mwanza. Ilikuwa imebaki kama dakika mbili hivi wafungue milango. Nilikuta baadhi ya wateja wengine wameshafika wanasubiria muda ufike waingie ndani ya Benki kwa ajili ya kupata huduma.

Milango ilivyofunguliwa nikawa wa kwanza kuingia na kwenda moja kwa moja kwenye foleni. Tellers wakati huo walikuwa hawajaanza kuhudumia walikuwa bado wanaweka weka mambo yao sawa.

Hamadi! nikamwona dada mmoja ambaye wakati milango imefunguliwa alienda kaunta (bila shaka alikuwa anaomba kujulishwa salio lake), akaja moja kwa moja akasimama mbele yangu. Nikamuuliza vipi dada mbona unanipita? akajibu kwa shari kubwa, "unasema ninakupita, naona umechanganyikiwa wewe, hivi unajifanya hukumbuki kuwa mimi ndie nimekutangulia kufika hapa kwenye jengo la Benki, wee si umekuja umenikuta hapo nje nasubiri milango ifunguliwe!, mimi na wewe na nani amempita mwenzie?"

Niliamua kukaa kimya sikumjibu, moyoni nikasema huyu dada anataka kunianzishia siku yangu vibaya. Nikamwacha akapita akahudumiwa baadae na mie nikahudumiwa.

Niliamua kukaa tu kimya, hivi ingekuwa ni nyie wenzangu Miss Natafuta, Joseverest na wengineo mngemfanya nini huyu dada ambaye ana onesha wazi kuwa ana kisirani cha asubuhi asubuhi.
Kusamehe ni miongoni mwa sifa kubwa za mwanaume aliyekamilika.

Sent from my HUAWEI CUN-U29 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu samahan lakin,juz watu walikua wanajadili wanahis wew ndio bikira wa kisukuma,je una taarifa hiz,wakawa wanaskilizia kama utakua active hum
Mkuu hizi taarifa nilizipata na niliandika uzi wa kuelezea kwamba mimi siye Seth.
Ahsante kwa kunijuza bytheway
 
Back
Top Bottom