Nina jirani yangu ana watoto wanne. Last born amemzaa ukubwani(5yrs old)
Leo ametembelewa na wajukuu zake. Mtoto wake last born hakuwepo. Mara akaingia paap! Mazungumzo yalikuwa kama ifuatavyo:
Last born: "Shikamoo baba"
Baba: "Marahaba mwanangu, ulikuwa wapi?"
Wajukuu kwa last born: "Aa aa! Siyo baba, sema babuu!!"
Baba: Akaduwaa, akawa ananideku kajicho kwa pembeni. Nikajifanya sijamuona. Sikuchekea pale. Nikaaga haraka.
Laa! Kufika nyumbani nimecheka vibaya sana!!