Leo nimefukuzwa kazi rasmi

Dah! Ndiyo ukubwa huo. Pole sana. 🙁

Na kama ulikuwa hujajiandaa kwa chochote, basi tegemea kupitia kipindi kigumu sana cha mpito.
 
Pole mzee. Kama ni mtu wa ibada tafuta kanisa/msikiti uwe unaenda kushinda na kuabudu. mkimaliza ibada nenda kazurure free beach ambayo kuna kiti na meza unajisomee vitabu vya dini na sio lazima ununue kinywaji au chakula. Kaa hapo mpaka jioni saa 12 kasoro rudi nyumbani kama una hg hawezi kujua kimewaka ofisini. Wakati huohuo tafuta sehemu barabarani anza kuuza matunda uanze kupata income stress itapungua. Kama mke wako ameajiriwa, jitahidi sana utafute hela kwa marafiki wa kweli ili majukumu nyumbani yaendelee umeme, maji, taka, mtungi wa gesi nk ama sivyo mkeo ataanza kukuchoka akianza kuvifanya yeye
 
Pole mkuu..kila kitu kina mwanzo na mwisho wake..baada ya mwezi 1 anza kufatilia mafao yako.
 
Pole sana ndugu. Hapo kama una mke mwema ndio utamuona sasa, manake wanawake huwa hawapendi mwanaume asiye na kazi. Ataanza kukunyanyasa jiandae kisaikolojia.
Lakini kama una mke mwema hiyo pesa inatosha kabisa mtaji wa biashara kwako na yeye pia. Kama mke wako anajituma basi mpe laki 2 tu inatosha biashara ya vitafunwa kwa maana ya maandazi, vitumbua, chapati n.k awe anauza asb kila siku. Akipata eneo lililochangamka atauza vizuri tu. Hapo hatakosa elf 10 lama faida kila siku ambayo itasaidia msosi.
Wewe jipange hata saidia fundi huko kwenye sites za ujenzi mpaka utakapopata kazi inayoeleweka. Na ukiweza kama hauna aibu hapa mjini
fanya biashara ya kuchoma mahindi au mahindi ya kuchemsha mtaji wake ni mdogo tu ni jiko na mahindi yako unatafuta site hukosi buku 10 had 20 kila siku. Mamangu alishafanyaga hii biashara ya mahindi ya kuchoma na alikuwa anatulisha na analipa kodi ya nyumba.

Mwisho Muombe sana Mungu na pole sana maisha yana mengi ila amini kuwa yatapita tu
 
Umefukuzwa ajira sio kazi. Kazi bado zipo nyingi tu, moja wapo ipo kwako. Hukuubwa uwe copy ya mtu, ukiacha panic utaona cha kufanya na hicho ndio kitakupa kazi. Pole kwa changamoto.
 
Umefukuzwa ajira sio kazi. Kazi bado zipo nyingi tu, moja wapo ipo kwako. Hukuubwa uwe copy ya mtu, ukiacha panic utaona cha kufanya na hicho ndio kitakupa kazi. Pole kwa changamoto.
nimefurahi sana kuita hiyo ni changamoto (challenge), ni neno kubwa sana la faraja kama mtoa mada atalielewa.
 
Umefukuzwa na kesi mahakamani au ni kufukuzwa tu?? Kama ni kufukuzwa tu, bas jipange upige mishe zingine…!!! Haya mambo yanatokea na sana …!! Ni ishu za mpito. Wapo wanaofukuzwa kazi plus kesi mahakamani, so wanajikuta hata hicho kidogo walichonacho kinaishia kwa mawakili kusimamia kesi….!!!!
 

Nimefukuzwa tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…