IKARAHANSI
JF-Expert Member
- Jul 30, 2019
- 398
- 479
Habari za muda huu waheshimiwa
Jana nimeona video clip inayomuonyesha Mwanaume aliyekatwa masikio baada ya kufumaniwa akizini na mke wa mtu ikisambaa kupitia mitandao ya kijamii, video clip hiyo ilisindikizwa na maneno ya Wakili (nimemsahau jina) aliyekuwa akifafanua kuwa kosa la kumfumania mkeo au mumeo kisheria adhabu yake ni kulipa faini kwa aliyefumaniwa au kufungua shauri la talaka endapo mume/mke atajisikia kufanya hivyo.
Sasa nikajiuliza namna mke anavyouma (kwa jinsi mapenzi yalivyo) halafu nimemfumania na jamaa nikaamua kufuata sheria kwa kwenda mahakamani, sote tunaujukiritimba wa mahakamani ikiwemo kupigwa kalenda, kuacha kazi/shughuli ya kuniingizia kipato kwa ajili ya kuhudhuria shauri mahakamani (upotevu wa muda) kumbe hatimaye ni kulipwa faini (ikiwa atakutwa na hatia). Sasa nikajiuliza zaidi mgoni wangu akinilipa fidia si ni kama ametoa mahari?
Kwa maana nyingine ni kuwa mtu mwenye ukwasi anaweza kucheza na ndoa yako anavyotaka maana anajua ukimfumania fedha ya kulipa faini anayo hivyo atakuwa mke wenu na siyo mke wako hapo bado sijajua akizaa naye itakuwa vipi. Kwa hukumu ya namna hii ni bora kumuacha mke au kumtia ulemavu mgoni wako ili hata kama utakwenda jela umuache na kumbukumbu ya kusimulia wajukuu zake.
Binafsi nilidhani kuwa kosa la kufumaniwa na mke/mume wa mtu adhabu yake ni kifungo cha jela kuanzia miaka kumi na tano (15 Yrs) na kuendelea, maana ukikutwa na mwanafunzi ni miaka thelathini (30 Yrs) hivyo hii ilitakiwa kuwa nusu yake maana wahusika wanajitambua na wapo juu ya miaka 18.
Binafsi naona adhabu ya kulipa faini haitoshi au wakuu mnasemaje. karibuni kuchangia na povu ruksa mradi tuelimishane.